Meya wa Ubungo, Boniface Jacob: Wenyeviti wa serikali za Mitaa Dar waitana Sabasaba

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Baada ya siku nane kupita tangu kuandika kwa ujumbe huu wa kuamsha wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa.
Leo january 16-2017 wenyeviti wote wa serikali za mitaa na wajumbe wao wanakutana ukumbi wa sabasaba,kupeana muafaka wa juu ya kupokonywa mihuri yao,na kuondoka na msimamo.

Nawaongezea haya

1.Watake pia serikali kupokonya mihuri madiwani wote nchi nzima kwa maana sheria inayotajwa kutotamka kumiliki kwa wenyeviti wa serikali za mitaa mihuri ni hiyohiyo haitamki pia kwa madiwani.

2.wapeane misimamo ya juu ya udharirishaji unaofanywa na Ma Dc na Ma Rc dhidi ya wenyeviti serikali za mitaaa na ikiwezekana wakubaliane kufungulia kesi Ma Dc na Ma Rc waliokwisha nyanyasa viongozi wenzao.

3.Wenyeviti wa selikali za mitaa pia leo waondoke na uamuzi juu ya kama waendeleee kuwepo ofisini au wasusuie shughuli zao mpaka muafaka utakapo patikana.

4.Wahoji uhalali wa zoezi hili kuanza Dar maramoja uporaji wa mihuri wakati mikoani bado wakiendelea kishikilia mihuri.

6.Wafufue vita yao ya kudai maslahi rasmi dhidi ya serikali na kuachana na utamaduni wa kulipwa 50,000/= hamsini elfu kwa mwezi na wajumbe seeikali za mitaa wakilipwa 5000/= elfu tano tuh kwa mwezi.

6.wadhibitishiwe ni kwa namna gani VEO,MEO,na WEO watendaji wa mitaa na ngazi zingine watakuwa na wakazi wa eneo hilo kiasi kwamba wataweza kutoa huduma za dharula kama,barua za dhamana, na zinginezo.

7.Wenyeviti wa serikali za mitaa wapate msaada wa kisheria kama serikali itaendelea kushupalia msimamo wake basi wakafungue kesi ya kuomba ufafanuzi wa kikatiba ibara ya 145,146,147 juu ya muingiliano wa mamlaka za serikali za mitaa na serikali kuu.

8.wenyeviti wa serikali za mitaa katika kulielezea jambo lao kama tatizo waunde uongozi imara wa mkoa wa DSM kwa ajili ya kipindi hiki cha kuwaunganisha na kuwa na sauti na kwajili moja tuh.

9.wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wao kwa Ummoja na hasa kipindi hiki bila kujali itikadi Zao za vyama wasigawanyike wala kugawanywa na wanasiasa wa ngazi za wilaya ama mkoa kwamba kama kesi za kutotenda sawa na mahitaji ya mihuri zipo kwa watendaji na mashauri yao mengi yapo TAKUKURU

10.Watangaze kuwa 2020 "kila mtu atabeba msalaba wake" na kwamba kwa kadiri wanavyo nyanyasa serikali za mitaa tunahaidi kulipa visasi vyetu uchaguzi mkuu 2020.

MKIFANYA HAYA
MTAKUWA NA MWANZO MZURI.

SENIOR COUNCILOR UBUNGO
MSTAHIKI MEYA UBUNGO
BONIFACE JACOB
 
Kwa Mara ya kwanza serikali ya magufuli inaweza kuingia kwenye majaribio kupitia wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa jijini dar es salaam

Kikao cha kuamua liwalo na liwe kinaendelee hapa TCC changombe, pamoja na jitihada za mkuu wa wilaya temeke kujaribu kuzui kikao hicho zimegonga mwamba.

Subiri tamko zito linakucha, wajumbe wote bila kujari vyama vyao wako ukumbini.

# sijaribiwi sasa wajumbe waamua kumjaribu
 
Ndio hapo CCM wajue kuwa tunakopelekwa siko. Sio wawe wanaitikia ndio mzee ndio mzee...
JK mjanja sana kaona mbali. Kawategeshea mtu ambaye chama litamfia mikononi mwake...

Mimi naombea mambo yazidi kuwa magumu ili watu waamke.
Na so far mambo yalishakua tait mkuu,hata watetezi wa chama wenyewe hali hio wanaisema wazi wazi.
 
Naona kunyang'anywa mihuri kumewaunganisha wote CCM+UKAWA


Uhalali na mamlaka ya ofisi ni muhuri, sasa ukiandika waraka au azimio au barua ukasaini bila muhuri hiyo document ni sawa na karatasi la kufungia maandazi tu! Wakomae mpk kieleweke.
 
Huyo DC wa Temeke akishindwa kuzuia hicho kikao kisifanyike basi kazi hana
 
Huyu Meya anapenda sana Kesi, dah
Nini maana ya ofisi? Itaje ofisi unayoifahamu isiyokuwa na muhuri.
Kama viongozi hao wapo kwa mujibu wa katiba na kazi zao za kila siku zinatajwa kwenye katiba na pia ofisi zao zipo kwa mujibu wa sheria inayowabainisha ni kwanini mihuri ya ofisi zao inyang'anywe?
Wagome au wajiuzulu nafasi zao uuitishwe uchaguzi upya.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Uhalali na mamlaka ya ofisi ni muhuri, sasa ukiandika waraka au azimio au barua ukasaini bila muhuri hiyo document ni sawa na karatasi la kufungia maandazi tu! Wakomae mpk kieleweke.
Kuandika balua ni kazi ya mwenyekiti wa mtaa au katibu? Ni nani mwajiriwa kati katibu na mwenyekiti?
 
Back
Top Bottom