Meya wa Manispaa ya S u m b a w a n g a , Samweli Kisabwiti kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kulinda heshima yake binafsi na ya chama chake. Akizungumza nyumbani kwake jana mjini hapa, Kisabwiti alisema amefikia uamuzi huo baada ya kutambua kwamba meya ni mtu muhimu sana katika kufanya kazi kwa ufanisi na anahitaji muda wa kutosha ili ajifunze. ''Kwa hiyo nimeona nipate muda wa kujifunza na kupata uzoefu kupitia nafasi yangu ya udiwani wa Kata ya Katandala na kupitia vikao mbalimbali.
"Nimeona ni vema nikaachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine wenye uzoefu kwani nafasi hiyo ni nyeti sana na inahitaji uzoefu na elimu ya kutosha,'' alisema.