Meya wa jiji la Tanga ametia aibu ya kuanzia mwaka

Meya wa JIJI la Tanga yuko sawa. Kwanza Mwalimu anaonyesha dharau sana. Mtoto mdogo, hakuvaa nguo za maadili ya ualimu, nyondo nyingi. Sio sawa. Alichokisema Mhe. Diwani ni sawa lakni hakuwa na sababu kukisema kwa wakati huu. Angetetea hoja yake tu. Msimtwishe mzigo Mhe. Waziri wa Elimu, pambaneni na hali zenu.
Ulitaka avae vazi gani?? Unajua anavyoishi mpaka akapata hilo vazi aliyovaa. Nyodo gani alionyesha?? Kwani kuongea na meya lazima usimame ebu acha hizo. Kila mtu yuko huru. Hakuna sheria ya elimu inayosema unapoongea na meya au waziri lazima usimame
 
Uyo dada kaonyesha dharau gani hapo zaidi ya woga nakukosa kujiamini kwasababu yakufokewa fokewa.na huo muda wakumuelimisha uyo muheshimiwa angeutoa wapi kwa mfano au ulitaka aitwe mkorofi na mbishi.Tatizo ni kwamba hawa wanasiasa wanapenda kunyenyekewa nakuogopwa kama miungu watu.
Ki msingi ni bahati mbaya kuwa mfumo wa uandaaji wa walimu na sisi sote kwa ujumla una mapungufu mengi. Diwani ana mapungufu yake na hata mtaalam wetu hajiamini. Hapa pa kujiamini ndipo tunapotakiwa kujikita na kusisitiza zaidi. Kujiamini kunatokana na uelewa mpana- kujua haki zake za kibinadamu kwa mujibu wa katiba yetu, kujua haki zake za kitaaluma na kujua haki zake kama mwajiriwa wa Halmashauri na kujua haki zake kama raia mwema wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama uelewa haupo, kujimini hakutakuwepo na uoga utatamalaki.

Nimalizie kwa kusema, nimejifunza mengi katika mjadala huu yawezekana sikuchagua matumizi bora ya baadhi ya maneno niliyotumia lakini kwa hakika na heshima haitakiwi umbatane na uoga. Kujiamini ni suala muhimu.
 
Dah,
Niliona hii video clip. Huyu jamaa ni mtupu kabisa kichwani, sijui ana elimu gani. Ila pia nimewaza hata huyu mwalimu ne ni kilaza pia, maana alichotakiwa kujibu ni kua akichosaini yeye na anachosema huyu jamaa ni kitu hicho hicho kimoja.

Hivi unamtuma mtoto akuletee maji yaliyojaa nusu, anakuja unamuuliza mbona umeleta maji yaliyopungua nusu na wakati nilitaka yaliyojaa nusu halafu anashindwa kujibu, hapo si ni wote vilaza tu?
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na kuchanganua mambo
 
... kaka, hebu tutumie akili kidogo tu! Tulicholetewa humu ni clip ya majibizano kati ya Meya na Mwalimu; hatukuletewa maandishi ya muda humu. Majibizano yenyewe yalikuwa hivi:-

Mwalimu: "... saa moja kasoro dakika ishirini na tano ..."
Meya: "... sasa mbona umeandika saa kumi na mbili na dakika thelathini na tano?".

Bado hujaelewa logic ya huu uzi? Duh!
Huyo atakuwa ndugu yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
we umeona wapi ameandika 12:35? na namna ya kusoma saa kama ni english time si inajulikana?, sita itamaanisha 12 na 12 itamaanisha sita, kama kosa lake ni hilo basi Meya alitakiwa amuulize 'kwa nini umeandika saa sita dk thelathini na tano?' yaani yeye alipaswa aisome kama inavyotakiwa(kiusahihi) na sio kusoma makosa, kwaio kama kweli mwl kaandika 12:35 basi mwl ana makosa ya kiuandish na Meya ana makosa ya kiusomaji, na wakienda mahakaman mwl anaweza hata ajitetee kama alimaanisha swahili time not english time na huna sheria ya kumbana
Tanzania maofisini kote tunatumia English time na siyo Swahili time
 
Tehe tehe.
Kuna yule Naibu waziri wa elimu aliwahi kusema Tanzania ni muungano wa nchi mbili,Tanganyika na Zimbabwe

Hao ndio wazalendo wa ccm
 
Meya ni kiongozi wa kisiasa kama mkuu wa mkoa sio lazima awe na elimu na uwezo wa kiakili hata akiwa na IQ 0.00000000000001 inatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh, kweli mnalipoteza taifa. Mayor ndio planning officer wa halmashauri. Kubuni njia za kuongeza mapato, maendeleo ya mtu mmoja mmoja, maendeleo ya halmashauri, na kila aina ya ubunifu. Leo mmekengeuka mnasema hata akiwa na IQ 0.000000 jamani acheni unafki watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwanini walimu wengi hawako karibu na haki. Linapokuja suala la CCM na Upinzani na hasa katika chaguguzi, waliowengi wako kuipendelea CCM, tena kwa gharama ya kuukandamiza upizani. Tendeni haki tu
Umeona pale wakati Mwalimu ana kaangwa hakuna hata aliye mtetea. Walimu wanaweza kuwa wengi lakini mmoja mmoja wana mazingira duni sana ya kazi na wako exposed vibaya kwa wakuu wao na wana siasa hivyo sidhani kama wako mbali na haki bali waki ikumbatia haki kwa tawala zisizojua haki hawana watetezi. Nchi nyingine video hiyo inge anzisha maandamano na Meya kuwajibishwa siyo hapa kwetu. Bado tuna safari ndefu sana ya kujikomboa.
 
Meya anamuuliza mwalimu mwalimu umefika kazini saa ngapi?

Mwalimu- nimefika saa moja kasoro dk 25,

Meya- Mbona umeandika kwenye daftari saa 12:35?

Meya akadhani mwalimu amemdanganya,hahahaha.


Tunapotagutaga kiki kupitia makamera tuhakikishe kile tunachotaka kujipatia umaarufu tunakijua vizuri.

Tena kwa jinsi tunavyoelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa tutashuhudia kiki za hovyo sana.

Yaani siku hizi watumishi wa umma ndio kila kiongozi anaona mahala pazuri pa kutafutia kiki kupitia midia.

Sent using Jamii Forums mobile app
huyu jamaa ni zero brain anaitwa Alhaji Mustapha Selebosi ni diwani wa kata ya Majani mapana mie binafsi nimemjua tokea mwaka 2002 nilipokuwa nasoma pale shule ya sekondari Eckenford.Yan jamaa anahistoria mbaya sana alishafumaniwaga na mke wa mtu jamaa wakamla kiboga wakamtangaza mji mzima yani huyu selebobo ni mtu wa kuji show up sana ana tabu ni bonge la zero yani sifuri kichwa sema anakubalika balaa kule Majani mapana
 
Samahani huyo ni ndugu katika chama, tena tulimnunua kwa dau kubwa hivyo mtatusamehe tu. Maana tukimchukulia hatua tutaonekana tulinunua bidhaa mbovu
 
Meya anamuuliza mwalimu mwalimu umefika kazini saa ngapi?

Mwalimu- nimefika saa moja kasoro dk 25,

Meya- Mbona umeandika kwenye daftari saa 12:35?

Meya akadhani mwalimu amemdanganya,hahahaha.


Tunapotagutaga kiki kupitia makamera tuhakikishe kile tunachotaka kujipatia umaarufu tunakijua vizuri.

Tena kwa jinsi tunavyoelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa tutashuhudia kiki za hovyo sana.

Yaani siku hizi watumishi wa umma ndio kila kiongozi anaona mahala pazuri pa kutafutia kiki kupitia midia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu meya ashtakiwe kwakujifananisha na waziri wa elimu,Hanatofauti na matapeli wanaojifananisha na usalama wa taifa au maaskari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom