lweitama cosmas jr
Member
- Sep 13, 2015
- 10
- 9
Mtukufu meya wa jiji la Dar es salaam- Mh Isaya Mwita
Mtukufu meya wa jiji la Dar es salaam Mh Isaya Mwita,leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe na kuapishwa kuwa meya wa jiji.
zikiwa zimepita siku 21 tu tangu akabidhiwe madaraka ya umeya amekutana na madudu mengi sana ndani ya ofisi hiyo.akielezea mapungufu hayo anasema inastajabisha kuona jiji la dar es salaam kwa mwaka linakusanya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 11 tu wakati ina vyanzo vingi vya kutosha.
mapato hayo kiduchu yanasababishwa na ufisadi mkubwa uliokua ukiendelea ndani ya ofisi hizo.na hayo ni pamoja makusanyo ya kodi ya vibanda vya ubungo stendi,kariakoo shule ya benjamini mkapa.ambapo ni elfu 30000 tu kwa mwezi inayoingia kwenye akaunti ya jiji kwa kila kibanda.isitoshe anasema ni aibu kubwa kwa soko kuu la kariakoo eti mpaka leo linajiendesha kwa hasara.
"Hayo ni machache tu yanayoonesha ufisadi mkubwa uliokuwa ukiendelea ndani ya jiji hili.lakini yapo mengi likiwemo suala la UDA"
Katika mkutano huo ambao aliambatana nabaadhi ya wajumbe wa baraza la madiwani wakiwemo Mh Halima mdee,mbunge wa kawe na.Mh Said Kubenea,mbunge wa ubungo.
Akiongelea suala la UDA mtukufu meya amesema.kwa ufupi tu ni kuwa jiji halijauza hisa zake kwa SGL..na kumuomba Mh Said Kubenea alifafanue zaidi
Mh Said Kubenea alianza kwa kuonesha nyaraka zilizo kwenye faili la uda ambazo zinathibitsha kuwa mchakato wa uuzwaji wa hisa za uda ulikuwa batili na haukukamilika.kampuni ya simon group limited(SGL) kwanza haikutimiza masharti ya ununuzi wa hisa za uda kwa mujibu wa sheria zilizoanzisha shirika hilo,kifungu 35 mpaka 40.hata hivyo shirika la uda linamilikiwa kwa ubia wa jiji 51% na hazina 49%.ambapo barua ya katibu wa hazina kwenda kwa meya wa jiji kipindi hicho Mh Masaburi ya mwaka 2011 kupingwa uuzwaji wa hisa hizo haukujibiwa na matokeo yake kampuni ya SGL ililipa fedha za awali za ununuzi wa hisa hizo kwa kuchelewa na mbaya zaidi zililipwa kwenye akaunti ya mtu binafsi ya Mh iddi simba.
Akifafanua ziadi Mh kubenea amesema mpaka sasa kampuni ya SGL wamelipa muamala wa shilingi bilioni 5 tu kwenda kwenye akaunti ya jiji.lakini hawatozirudisha ila watazihodhi mpaka SGL watakapojitokeza na kupiga hesabu upya kwa kiasi gani amenufaika kwa kutumia jina la UDA.kwa sababu hata magari alionunua ametumia jina la UDA kukopa benki ya NMB na kuweka dhamana hati za viwanja vya jiji .na katika hili anasema mabilioni yaliochotwa na Simon toka NMB endapo mradi wa DART utafeli basi benki ya NMB itafilisika.hii ni kwa mujibu wa waziri wa Tamisemi alivyolieleza bunge.na tujiulize NMB ikifilisika uchumi wa nchi utayumba kwa kiasi gani.!??
Akihitimisha mkutano huo Mh Halima Mdee anashangaa sana nchii hii sasa inavyoendeshwa bila kuheshimu sheria.amesema Mh rais amekua akivunja sheria na kutoa amri ambazo sasa hata mawaziri wake nao wanaiga hivyohivyo.hivi karibuni Mh Simbachawene waziri wa Tamisemi alitangaza kuivunja bodi ya machinga complex na kulikabidhi jengo hilo kwa mkuu wa mkoa.lakini sheria iliotumika kuruhusu jiji likakope NSSF hela za kujenga jengo hilo zipo na zimeweka wazi muundo wa utawala jengo hilo inayoitwa Dar es salaam city business act .kifungu cha 5 -7 cha sheria hiyo inaelezea muundo na hakuna sehemu inayomtambua waziri na chombo pekeee chenye mamlaka ya kuvunja bodi ni baraza la madiwani.hivyo wanashangaa waziri kapata wapi mamlaka hiyo.? Na hata mkuu wa mkoa ametwaja kwenye sheria hiyo sehemu moja tu,katika uundwaji wa bodi ndio yeye na meya kwa pamoja wataunda bodi hiyo.
Na wakijibu moja ya maswali ya waandishi lililohoji uhamishwaji wa vyanzo vya mapato kwenda serikali kuu.wamesema hilo haliwezekani kirahisi sababu lipo kisheria hivyo ili kuhamusha nilazima lipelekwe bungeni kujadiliwa