Meya wa Canada aasi Ulevi na kuokoka!

Meya wa Canada aasi Ulevi na kuokoka!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Meya wa mji wa Toronto nchini Canada, Rob Ford, ameasi ulevi baada ya ‘kuokoka’. Jambo hili limetokea baada ya makansela wa baraza la jiji kumpunguzia madaraka yake.

Bwana Rob Ford mwenye umri wa miaka 22 anasema ameamua kuasi pombe, baada ya kuokoka na kumtambua Yesu huku akisema kuwa kamwe hatawahi kuonja tone la pombe.

Kabla ya kumtambua Yesu, bwana Rob aliahidi kuwapiga vita makansela waliopiga kura kumpunguzia mamlaka.

Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper alisema kuwa madai dhidi ya Bwana Ford ni ya kusikitisha sana .

Meya huyo alikabiliwa na shinikizo kujiuzlu baada ya kukiri kuwa aliwahi kutumia dawa ya kulevya aina ya cocaine wakati alipokuwa mlevi chakari.

Pia anakabiliwa na madai ya kumtongoza mfanyakazi wake mmoja wa kike pamoja na kutumia lugha chafu, kuwatisha wafanyakazi wake na kuwa na uhusiano wa kimapanzi na kahaba.

Kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari nchini humo, Ford alisema hajaonja mvinyo kwa wiki tatu na kuwa hatawahi kamwe kunywa pombe.

"Nimeweza kumtambua Yesu kama mwokozi wangu.,’’ alisema Ford.bbc
 
Namkubali sana Ford maana anaafadhali kuliko Meya Jerry Silaa wa Ilala aliyekwenda kuporomosha mitusi pale EATV
 
Jamani Ndugu zetu Kanada vumilieni maana sisi huku kwetu Bongo Kuna waziri wa zamani amekapuya kajukuu kake na atazikwa nako maana amekaunganishia gridi ya elekitilisite ya huku....
 
Hakuna kitu kama "Meya wa Canada" hebu badilisha heading.
Nafikiri ulimaanisha Meya wa Toronto , Canada.
 
Jamani Ndugu zetu Kanada vumilieni maana sisi huku kwetu Bongo Kuna waziri wa zamani amekapuya kajukuu kake na atazikwa nako maana amekaunganishia gridi ya elekitilisite ya huku....

Na huyu Waziri wa zamani anadunda mtaani na anaangaliwa kana kwamba amefanya jambo la kishujaa na kuendelea kuinyima amani familia ya hicho kijukuu chake alichoki-kapuya na kukimilikisha gridi ya taifa,
 
Back
Top Bottom