nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Habari
Deus Bugaywa
Toleo la 268 14 Nov 2012
WAKATI wakazi wa Jiji la Mwanza, hususan, wakazi Manispaa mpya ya Ilemela wakiwa katika sintofahamu juu ya utata wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, sasa aingilie kunusuru mambo.
Kinataka Pinda amchukulie hatua Mkurugenzi na kutengua matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita uliomweka katika madaraka ya Meya, Diwani wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata, aliyefukuzwa na chama chake, akarejeshewa uanachama kwa amri ya Mahakama, akisubiri kesi ya msingi kupinga kufukuzwa imalizike, ili kuepusha mgogoro mkubwa unaoweza kujitokeza na kudumaza maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Uchaguzi huo uliompa Matata umefanywa na madiwani sita wakiwemo wanne wa CCM mmoja wa CUF (Mbunge wa Viti Maalumu) na Matata mwenyewe, huku madiwani wanane wa CHADEMA wakiususia kwa madai kuwa ulikiuka taratibu. Matata alipata kura zote sita.
Meya Matata ameleta mkanganyiko miongoni mwa wananchi, wanashindwa kujua hasa anatokana na chama gani kwa kuwa alipigiwa kura na madiwani wa CCM na CUF wakati wale wa chama chake walisusa.
Akizungumzia uchaguzi huo Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge na Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema, amesema ni wakati sasa wa Waziri Mkuu Pinda kuonyesha kwa vitendo umuhimu wa kuzingatia sheria kama alivyosisitiza katika hotuba yake ya kuahirisha Bunge aliyoitoa mwishoni mwa wiki jana.
"Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria, aanze na kutengua matokeo hayo na kumchukulia hatua za kinidhamu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kwa kuwa amevunja sheria za nchi makusudi", alisema.
Alisema CHADEMA kinaalani kitendo hicho kwa kuwa kilichofanyika Ilemela ni uhuni ambao hauwezi kuwa na nafasi katika nchi inayojiita inafuata demokrasia ya vyama vingi kwa kuwa kitendo hicho ni kuwadharau wananchi walioamua katika Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwachagua madiwani wengi wa chama chake.
Akifafanua kilichotokea Mrema alisema Mkurugenzi wa Halmashuri ya Ilemela aliamua kwa makusudi kupuuza barua mbili halali za chama hicho na kuikubali barua anayosema si halali iliyokuwa ikimtambulisha Diwani wa Kitangiri Henry Matata aliye na mgogoro na chama hicho.
"Tulipata taarifa kuwa tarehe 3, Novemba Mkurugenzi alipokea barua iliyokuwa inamteua Matata iliyokuwa imsainiwa na Abel Mwasa (Katibu wa zamani wa wilaya ya Ilemela) tarehe 5, Kaimu Katibu wa Ilemela Carlos Majura alimwandikia Mkurugenzi kumjulisha Abel alishaondoka na kuwa katibu wa wilaya yuko masomoni nafasi hiyo imekaimishwa kwake (Majura)" alisema.
Anaeleza kuwa baada ya mkanganyiko huo, Makao Makuu ilibidi kungilia kati ili kuweka mambo sawa, Katibu Mkuu alimtambulisha John Mrema kwa Mkurugenzi kuwa ndiye aliyetumwa na chama kusimamia mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama hicho. Baadaye Mrema alimwandikia Mkurugenzi barua ya kuwatambulisha wagombea wa chama hicho, barua ambayo anasema Mkurugenzi aliamua kuipuuza kwa sababu zisizojulikana.
Pamoja kupuuzwa huko kwa barua hiyo Mrema anaeleza kuwa uchaguzi huu umefanywa kwa mbinu chafu ambazo zilikuwa zimedhamiria kudhulumu haki ya wakazi wa Ilemela kwa kuwa hata akidhi ya idadi ya madiwani wanaoweza kuendesha kikao cha uchaguzi au bajeti haikutimia.
Kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1979, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 1984, akidhi ya kikao cha Baraza la Madiwani ili kupitisha bajeti ya halmashauri au kufanya uchaguzi inatakiwa kuwa theluthi mbili ya wajumbe wote.
Lakini kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela Zuberi Mbyana akifafanua kilichotokea alisema kuwa alipokea barua mbili zote kutoka CHADEMA, moja ilikuwa imesainiwa na Katibu wa Wilaya ya Ilemela Anajus John iliyokuwa ikimtambulisha Henry Matata kama mgombea Umeya na Marietha Chenyege kama mgombea wa naibu Meya.
"Barua ya pili nilipokea kutoka Makau Makuu ya CHADEMA hii haikuwa na muhuri wala nembo ya chama, ilikuwa inamtambulisha Abubakar Kapera Diwani wa Nyamanoro kama mgombea Umeya na Dani Kahungu, Diwani wa Kirumba, kama mgombea Unaibu Meya" alisema.
Alifafanua kuwa baada ya mkanganyiko huo walijaribu kuchugunza na kujiridhisha kuwa saini ya Katibu wa Ilemela ilikuwa sahihi na baada ya kushauriwa na wanasheria na kuipitia katiba ya CHADEMA wakagundua kuwa kikao chenye mamlaka ya kuteua wagombea umeya na naibu wake ni Kamati Tendaji ya Wilaya na hivyo wakaamua kuitambua barua ya Katibu wa Wilaya.
Hata hivyo, maoni hayo yanapingwa na Mrema kwa kuwa barua zilizopelekwa kwa Mkurugenzi huyo zilikuwa na sifa zote za barua ya kiofisi na kwamba hata kama kungekuwa na tatizo hilo ilikuwaje uchaguzi huo uendeshwe wakati akidhi ya wajumbe kwa mujibu wa sheria ilikuwa haijatimia.
Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi Mbyana alisema wanasheria walifafanua vizuri suala hilo la akidhi wakati wa uchaguzi huo. Katika uchaguzi huo Mwanasheria wa Jiji la Mwanza Sarah Savela alifafanua taratibu mbalimbali za kisheria kuhusu uhalali wa uchaguzi huo.
Alipoliulizwa juu ya uhalali wa uchaguzi huo kwa akidhi ya wajumbe sita badala ya wajumbe 9 wanaounda tehuluthi mbili za wajumbe wa mkutano huo ambao ndiyo akidhi halali ya mkutano huo alisistiza kuwa sheria imefuatwa na kwamba akidhi hiyo ilitimia kwa mujibu wa sheria.
Meya wa Halmashuri ya Ilemela Matata akizungumzia kuchaguliwa kwake kwenye mazingira ya utata namna hiyo alisema kuwa suala la akidhi limetimia katika kikako hicho ambapo alisema ya kuwa kwa mujibu wa sheria akidhi ilipaswa kukokotolewa kwa idadi ya madiwani kumi na mbili kwa kuwa wawili tayari wamekutwa na hatia na Mahakama hivyo hawawezi kuhesabiwa kama wajumbe halali wa kikao hicho.
Hata hivyo kwa idadi ya wajumbe wanaotakiwa kukidhi akidhi ya theluthi mbili ya wajumbe hao 12 inakuwa wajumbe 8 hata kama idadi hiyo ikikokotolewa kwa maelezo ya Meya huyo.
Aidha Matata ameeleza kuwa ameteuliwa na kamati halali na hakuna barua aliyoghushi, kikao kilichomteua ni kikao halali kwa mujibu wa chama. Ameendelea kueleza kuwa Meya si lazima ateuliwe na chama, kwa kuwa sheria inasema ni lazima atokane na madiwani, ni mazoea tu ambayo watu wanayatumia kunyima haki wengine.
"Ukishakuwa diwani unawakilisha wananchi, mimi ni diwani wa wananchi na kama kufukuzwa chama, tusubiri kesi yangu iko mahakamani, wasionitaka ni watu kama 30 tu wa Makao Makuu na mmoja tu anatoka Mwanza, lakini watu wa Mwanza wananipenda sana," alisema Meya Matata ambaye wadhifa wake huo mpya umeleta matata kwelikweli hapa.
Akizungumzia ni namna gani ataendesha vikao vya halmashauri katika mazingira hayo alisisitiza kwamba ataongoza vyema tu na kama madiwani wa CHADEMA wakiendelea kususia vikao vikifika vikao vitatu kuanzia walichosusia uchaguzi atawafukuza kama sheria inavyotaka.
"Kuna Halmashauri zina madiwani saba tu , hawa (madiwani wa CHADEMA) wasipohudhuria vikao vitatu mfululizo tunawafukuza, uitwe uchaguzi mpya, Jumatano (leo) naitisha Baraza la Madiwani kuunda kamati, wasipohudhuria watakuwa wanabaki na kikao kimoja wasipohudhuria hicho tunawatimua," alisema