Tetesi: Meya Kinondoni ni Jipu

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,204
18,543
Japo ukawa wanajisifu kushinda uchaguzi lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote.

Nadhani mayor wa kinondoni aachane na majigambo yasiyo na maana badala yake tuone mipango uliyo nayo.

Sijaona manispaa yenye barabara mbovu ukiacha zile za Tanroad kama kinondoni.

Kuna siku nimepita njia ya hospitali ya mwananyamala sitasahau, nilihisi nimepotea njia.

Barabara ni mbovu lakini utakuta kinamama bado wanazifagia na watu wanapiga pesa kama kawaida.

Mr Bonface tunataka kuona vitendo maneno tumesha yazoea.

Hadi sasa naona mnaziba viraka vya lami kwa odongo , kweli ukawa ni jipu.
 
Amekusikia.

Ila kumuita jipu ili hali hajamaliza hata miezi 2 ofisini ni U JIPU pia.

Hata mimi, nakwazika na hiyo barabara, naamini UKAWA watalifanyia kazi hili mapema kabla mwaka haujaisha.
Mbona Magufuli ameingia miezi michache iliyo pita lakini walau kuna mambo kayafanyia kazi.
Huyu mayor zake maneno, lakini hakuna anacho fanya, kwangu bado ni jipu tuu.
 
Nina amini Halmashauri na manispaa zinazoongozwa na UKAWA hazina jambo jipya la kusukuna maendeleo, kwa kuwa walioteuliwa kuziongoza wana mawazo mgando na wamejaa mipasho na kejeli tu vichwani mwao. Nasubiri, kusahihishwa kwa hili, kwa kuwa katika siku 100 za uongozi wa Rais Magufuli, hawajathubutu wao wenyewe kutoa tathmini ya maeneo yao wanayotawala, wamefanya vizuri kiasi gani.
 
Mambo gani aliyofanya yakanigusa mimi "end user?"

Usijitoe ufahamu kwa vitu vya msingi na kuleta ligi zisizo na maana hapa.

By the way, kwani hiyo barabara haimhusu Rais na waziri wake wa ujenzi?!
 
barabara hiyo nimetolea mfano, lakini barabara chini ya manispaa ya kinondoni ni mbaya na ukipita sasa ivi utakuta wanaziba mashimo kwa udongo.
 
li
Mbona Magufuli ameingia miezi michache iliyo pita lakini walau kuna mambo kayafanyia kazi.
Huyu mayor zake maneno, lakini hakuna anacho fanya, kwangu bado ni jipu tuu.
kili cha maendeleo ambacho magufuli amefanyia kazi
 
mkuu wewe ndo jipu,,sasa mtu ndani ya manispaa hata nusu mwaka hana unataka uone miradi imekamilika sasa akili au matope hyo
 
Nina amini Halmashauri na manispaa zinazoongozwa na UKAWA hazina jambo jipya la kusukuna maendeleo, kwa kuwa walioteuliwa kuziongoza wana mawazo mgando na wamejaa mipasho na kejeli tu vichwani mwao. Nasubiri, kusahihishwa kwa hili, kwa kuwa katika siku 100 za uongozi wa Rais Magufuli, hawajathubutu wao wenyewe kutoa tathmini ya maeneo yao wanayotawala, wamefanya vizuri kiasi gani.
leo hiimnajitoa akili kuwa hata chaguzi za mameya figisu zilikuwa nyingi sehemu zote ukawa walipokuwa na wajume
 
Japo ukawa wanajisifu kushinda uchaguzi lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote.

Nadhani mayor wa kinondoni aachane na majigambo yasiyo na maana badala yake tuone mipango uliyo nayo.

Sijaona manispaa yenye barabara mbovu ukiacha zile za Tanroad kama kinondoni.

Kuna siku nimepita njia ya hospitali ya mwananyamala sitasahau, nilihisi nimepotea njia.

Barabara ni mbovu lakini utakuta kinamama bado wanazifagia na watu wanapiga pesa kama kawaida.

Mr Bonface tunataka kuona vitendo maneno tumesha yazoea.

Hadi sasa naona mnaziba viraka vya lami kwa odongo , kweli ukawa ni jipu.

Hizo barabara alijenga Meya aliyepita ,mkurugenzi na mkuu wa wilaya anajuwa ......mnataka barabara hata siku Mia bado???

Mbona wamekopesha wajasiriamali fungu ambalo Miaka yote lipo na hatujui Nani alikuwa anapewa ???
 
Mbona Magufuli ameingia miezi michache iliyo pita lakini walau kuna mambo kayafanyia kazi.
Huyu mayor zake maneno, lakini hakuna anacho fanya, kwangu bado ni jipu tuu.
Magufuli kafanya nini cha maana? Kajenga nini toka aingie madarakani?
 
Watu wengine kwa kutaka maendeleo ya haraka mtu kaingia
Hata miezi mitatu bado ndio mana kuendelea inakua shida tatizo tunataka maendeleo ya haraka
 
Yaani hata hajajua ofisi aipange vipi tayari amekuwa jipu? Naona sasa falsafa ya jipu imepoteza mwelekeo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom