MEYA KIMBE AJITATHMINI,ASIOGOPE FEDHEHA KWA KUWA MKWELI

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
*KIMBE AJITATHMINI; ASIOGOPE FEDHEHA KWA KUWA MKWELI*

Na. Dady Igogo.

Nimemsikiliza mtuhumiwa wa rushwa Mh. Alex Boniphace Kimbe akitoa ufafanuzi. Kimsingi amejaribu kujitetea tu na kuhamisha hoja ya jinai kuwa suala la kisiasa.

1. Siyo mara ya kwanza kwa Kimbe kutuhumiwa rushwa. Mimi na yeye tulishatuhumiwa na Diwani wa kata ya Mshindo Mh. Ibrahim Ngwada kwamba tuliomba rushwa kwa wakandarasi wa barabara kabla hazijahamishiwa kwenda TARURA. Alishatuhumiwa kwenye sakata la viwanja kwa kujinilikisha viwanja vya Mzee Japan kata ya Mwangata hadi Waziri wa Ardhi aliamua kufuta viwanja vile. Alishatuhumiwa kuhusu kutoa vibali vya ujenzi na kuwakinga baadhi ya watumishi. Amelalamikiwa mara kadhaa na wakandarasi kwa kile kinachoitwa "kulazimisha fedha". Ameshalalamikiwa na baadhi ya madiwani ndani ya chama chake kwa tuhuma hizi hizi. Tuhuma hizi ni jambo moja, ukweli wake ni jambo lingine. Hatimaye hadi aliponaswa kwa mtego wa TAKUKURU kwa kusaidiana na raia mwema na mtoa taarifa.

2. Kwamba mtoa taarifa alipewa zabuni miezi sita. Namuomba akasome Prevention and Combating of Corruption Act, 2007. Kip cha 18. 1(a). Asome tafsiri ya dhana nzima ya rushwa. Arejee rushwa katika local govt authorities zinazovyofanywa ikiwa ni pamoja na kuchelewesha hati ya malipo kwa wazabuni waliokwisha kupewa tender, ikiwa ni pamoja na ahadi zote hata kama mzabuni alipewa tender.

Ukisoma kanuni za kudumu za halmashauri ya Manispaa ya Iringa za mwaka 2015 kipengele cha 66 _"....halmashauri itakua na haki kusitisha mkataba na kumdai mkandarasi malipo ya fidia kutokana na kusimamishwa kwa mkataba huo endapo mkandarasi atabainika kuwa ameahidi kutoa au ametoa au amekubali kutoa kwa mtu yeyote zawadi yoyote...."_ Hapa utagundua kuwa mkandarasi amefanya jambo muhimu sana.

3. *Kwamba ni mpango wa kumtoa nafasi ya Umeya.* Mtuhumiwa amehamishia masuala ya jinai kwenye siasa. Let say kuwa ni mtego. Kila mtu huwekewa mtego kwenye kile anachokipenda. Angekua anapenda uzinzi angewekewa mtego wa wa wanawake. Kuna weakness tayari ilionekana kisha ikatumiwa hapo hapo (kama ni mtego)

Kanuni ya kudumu ya IMC ya mwaka 2015 kip. cha 83 (1) imetoa masharti makubwa mawili. Sharti la kwanza ni azimio kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe/madiwani. Sharti la pili ni tuhuma zenye ushahidi wa kutosha. Ukiangalia sababu za kumtoa meya zimeainishwa sababu tano. Kimbe anazo sababu nne.
a/. Kutumia nafasi yake vibaya. (rejea viwanja vya mzee Japan)
b/. Kushiriki vitendo vya rushwa (ushahidi upo kutoka mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa)
d/ Kushindwa kutekeleza vibaya majukumu yake. (kuruhusu agenda zenye migogoro ya kimaslahi kwenye vikao na mikutano ya Baraza)
e/. Mwenendo mbaya na ukosefu wa adabu.

Hivyo utagundua kuwa zipo hoja za kumtoa Mstahiki Meya. Issues ni akidi ya asilimia 75% ya hoja kuungwa mkono.

4. *Suala la tamko la RC Hapi kuwa ameingilia uhuru wa mahakama*

Ieleweke kuwa RC ni msimamizi wa taasisi zote za serikali katika mkoa wake. Ndiye msemaji wa mkoa. Yeye ndiye ni kiranja mkuu wa mamlaka ya serikali za mitaa kwenye mkoa wake. RC anapata taarifa nyingi za kiusalama kuliko wananchi. Ndiyo maana kwenye muundo wa kamati yake ya ulinzi na usalama wa mkoa Kamanda wa PCCB ngazi ya mkoa ni mjumbe.

Ieleweke pia RC ndiye anayeunda kamati ya uchunguzi ya kubaini tuhuma kwenye hoja za kumuondoa Meya madarakani. Sheria haimtaki RC kusubiria hukumu ya mahakama ndiyo maana kuna kamati. Ila busara ya kamati inaweza ikasubiria hukumu ya mahakama.

Kwanini RC alizungumzia issue ya Meya sababu ukianza ku deal na viongozi wakubwa hawa wakuu wa idaea wataogopa. RC Ally Hapi alikua sahihi.

5. *Kwamba Mtuhumiwa alikua anamdai Mtoa taarifa* Mahakama itaamua hapo. Suala hili liko mahakamani. Ila inaleta shaka kwanini mtuhumiwa alitoa taarifa ya kuomba msaada kwa DC kama ilikua ni deni? Bila kujua kuwa DC amekua mstari wa mbele katika kupinga na kuzuia rushwa kwenye wilaya yake.

Ni vyema kujua kuwa masuala ya rushwa ni kosa la jinai. Lakini pia inaondoa mamlaka ya kimaadili kwenye uongozi wa umma sababu mtuhumiwa anapaswa kuwa kiongozi wa mfano. Mimi ningekua yeye NINGEJIUZULU UMEYA NA KUBAKI NA UDIWANI PEKEE ila kwa sababu ambazo zisingekua za moyoni.

_Dady Igogo_
Diwani mstaafu
Manispaa ya Iringa
 
Huyu Dadi Igogo ndiye yule walimkimbiza na bodaboda akaona gari inamchekewesha akashuka na kukimbia kwa miguu kuelekea vichochoroni kufika huko wakamkamata na kumtoa sarawili baada ya hapo akaamua kujivua huo udiwani!!! au ni mwingine?
 
Em ukuje ujibu na wewe tuuma zako
Wewe si ndie unatuhumiwa na wananchi uliwasaliti kwa kufika bei upande wa pili,na hujawambia wananchi waliokuchagua ulipewa rushwa kiasi gani leo unatuaminisha Kimbe kuchukua rushwa,acheni kupotosha watu kwa maslai yenu nchi ni yetu sote hii
 
Huyu Dadi Igogo ndiye yule walimkimbiza na bodaboda akaona gari inamchekewesha akashuka na kukimbia kwa miguu kuelekea vichochoroni kufika huko wakamkamata na kumtoa sarawili baada ya hapo akaamua kujivua huo udiwani!!! au ni mwingine?
Ndio huyo huyo walimla kiboga
 
*KIMBE AJITATHMINI; ASIOGOPE FEDHEHA KWA KUWA MKWELI*

Na. Dady Igogo.

Nimemsikiliza mtuhumiwa wa rushwa Mh. Alex Boniphace Kimbe akitoa ufafanuzi. Kimsingi amejaribu kujitetea tu na kuhamisha hoja ya jinai kuwa suala la kisiasa.

1. Siyo mara ya kwanza kwa Kimbe kutuhumiwa rushwa. Mimi na yeye tulishatuhumiwa na Diwani wa kata ya Mshindo Mh. Ibrahim Ngwada kwamba tuliomba rushwa kwa wakandarasi wa barabara kabla hazijahamishiwa kwenda TARURA. Alishatuhumiwa kwenye sakata la viwanja kwa kujinilikisha viwanja vya Mzee Japan kata ya Mwangata hadi Waziri wa Ardhi aliamua kufuta viwanja vile. Alishatuhumiwa kuhusu kutoa vibali vya ujenzi na kuwakinga baadhi ya watumishi. Amelalamikiwa mara kadhaa na wakandarasi kwa kile kinachoitwa "kulazimisha fedha". Ameshalalamikiwa na baadhi ya madiwani ndani ya chama chake kwa tuhuma hizi hizi. Tuhuma hizi ni jambo moja, ukweli wake ni jambo lingine. Hatimaye hadi aliponaswa kwa mtego wa TAKUKURU kwa kusaidiana na raia mwema na mtoa taarifa.

2. Kwamba mtoa taarifa alipewa zabuni miezi sita. Namuomba akasome Prevention and Combating of Corruption Act, 2007. Kip cha 18. 1(a). Asome tafsiri ya dhana nzima ya rushwa. Arejee rushwa katika local govt authorities zinazovyofanywa ikiwa ni pamoja na kuchelewesha hati ya malipo kwa wazabuni waliokwisha kupewa tender, ikiwa ni pamoja na ahadi zote hata kama mzabuni alipewa tender.

Ukisoma kanuni za kudumu za halmashauri ya Manispaa ya Iringa za mwaka 2015 kipengele cha 66 _"....halmashauri itakua na haki kusitisha mkataba na kumdai mkandarasi malipo ya fidia kutokana na kusimamishwa kwa mkataba huo endapo mkandarasi atabainika kuwa ameahidi kutoa au ametoa au amekubali kutoa kwa mtu yeyote zawadi yoyote...."_ Hapa utagundua kuwa mkandarasi amefanya jambo muhimu sana.

3. *Kwamba ni mpango wa kumtoa nafasi ya Umeya.* Mtuhumiwa amehamishia masuala ya jinai kwenye siasa. Let say kuwa ni mtego. Kila mtu huwekewa mtego kwenye kile anachokipenda. Angekua anapenda uzinzi angewekewa mtego wa wa wanawake. Kuna weakness tayari ilionekana kisha ikatumiwa hapo hapo (kama ni mtego)

Kanuni ya kudumu ya IMC ya mwaka 2015 kip. cha 83 (1) imetoa masharti makubwa mawili. Sharti la kwanza ni azimio kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe/madiwani. Sharti la pili ni tuhuma zenye ushahidi wa kutosha. Ukiangalia sababu za kumtoa meya zimeainishwa sababu tano. Kimbe anazo sababu nne.
a/. Kutumia nafasi yake vibaya. (rejea viwanja vya mzee Japan)
b/. Kushiriki vitendo vya rushwa (ushahidi upo kutoka mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa)
d/ Kushindwa kutekeleza vibaya majukumu yake. (kuruhusu agenda zenye migogoro ya kimaslahi kwenye vikao na mikutano ya Baraza)
e/. Mwenendo mbaya na ukosefu wa adabu.

Hivyo utagundua kuwa zipo hoja za kumtoa Mstahiki Meya. Issues ni akidi ya asilimia 75% ya hoja kuungwa mkono.

4. *Suala la tamko la RC Hapi kuwa ameingilia uhuru wa mahakama*

Ieleweke kuwa RC ni msimamizi wa taasisi zote za serikali katika mkoa wake. Ndiye msemaji wa mkoa. Yeye ndiye ni kiranja mkuu wa mamlaka ya serikali za mitaa kwenye mkoa wake. RC anapata taarifa nyingi za kiusalama kuliko wananchi. Ndiyo maana kwenye muundo wa kamati yake ya ulinzi na usalama wa mkoa Kamanda wa PCCB ngazi ya mkoa ni mjumbe.

Ieleweke pia RC ndiye anayeunda kamati ya uchunguzi ya kubaini tuhuma kwenye hoja za kumuondoa Meya madarakani. Sheria haimtaki RC kusubiria hukumu ya mahakama ndiyo maana kuna kamati. Ila busara ya kamati inaweza ikasubiria hukumu ya mahakama.

Kwanini RC alizungumzia issue ya Meya sababu ukianza ku deal na viongozi wakubwa hawa wakuu wa idaea wataogopa. RC Ally Hapi alikua sahihi.

5. *Kwamba Mtuhumiwa alikua anamdai Mtoa taarifa* Mahakama itaamua hapo. Suala hili liko mahakamani. Ila inaleta shaka kwanini mtuhumiwa alitoa taarifa ya kuomba msaada kwa DC kama ilikua ni deni? Bila kujua kuwa DC amekua mstari wa mbele katika kupinga na kuzuia rushwa kwenye wilaya yake.

Ni vyema kujua kuwa masuala ya rushwa ni kosa la jinai. Lakini pia inaondoa mamlaka ya kimaadili kwenye uongozi wa umma sababu mtuhumiwa anapaswa kuwa kiongozi wa mfano. Mimi ningekua yeye NINGEJIUZULU UMEYA NA KUBAKI NA UDIWANI PEKEE ila kwa sababu ambazo zisingekua za moyoni.

_Dady Igogo_
Diwani mstaafu
Manispaa ya Iringa
Acha uongo kwani ungenyamaza ungekufa? Angekuwa meya kutoka ccm ungethubutu?
 
Basi kwa kuwa katoka Chadema aendelee kula rushwa hakika sasa Chadema kimekuwa chama cha wala rushwa,nyie wapambe badala ya kuijenga Chadema ndio mnaizika ,mbona rushwa asibambikiwe Msigwa,sababu nae ana nafasi yake .
 
Hivi Unawezaje kumsikiliza Mshamba Ally Hapi ?
 
Back
Top Bottom