UJINGA WA MWAFRIKA
Member
- Sep 24, 2013
- 13
- 0
Meya huyu takribani miaka 7 sasa amekuwa anafitinisha wakurugenzi katika ngazi mbalimbali za ccm toka enzi ya mama munuo na hili ni kwa kupigania maslahi yake binafsi ambayo alijijengea mazoea wakati wa kabwe.jiji hili amelivuruga vya kutosha na kinachonishangaza ngazi zote za serikali wilaya na mkoa zimepofoka macho kwa kutokuwa wakweli juu ya diwani huyu wa itiji ambaye mara tu baada ya kupata umeya amenunua magari,mashamba na kufungua biashara.kibaya zaidi amekuwa akijisifu sana mitaani pale wakurugenzi wanaombana kufuja mali za jiji wanapoondolewa.amekuwa anakwamisha mambo mengi ya maendeleo kwa kuwazunguka watendaji kwa kuwafitinisha na wananchi.jk vunja baraza la madiwani ili kunusuru heshima ya serikali yako na uwatimizie wananchi wa jiji hili maendeleo endelevu tarajiwa.mji huu una kila fursa kwa kuwa kitovu cha kibiashara,viwanda na kilimo.jk utapata faida na serikali yako ukilivunja baraza hili na utakuwa umeondoa siasa uchwara amazo zimeendelea ktawala kwa zaidi ya miaka 10 jijini hapa