msemakwelitz
Member
- Sep 23, 2016
- 15
- 38
Meya alifungua rasmi daraja hilo tarehe 27/02/2017 akiambatana na Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku aliyemwakilisha mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ndugu Msongela Nitu Palela, Madiwani mbalimbali, wabunge, watendaji wa Kata husika, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kisiwani (CCM) ndugu Peter Clement, viongozi wa vyama vya siasa na wananchi.
Daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka mmoja chini ya usimamizi wa Diwani wa kata ya Bonyokwa ambaye pia niMstahiki Meya wa Ilala Mhe Kuyeko na kugharimu takribani Tsh.million 478 fedha Manispaa ya Ilala.
Mhe. Kuyeko amemtaka mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutokushiriki kuanzisha vita na mgogoro wa kiitikadi za kisiasa ndani ya Manispaa ya Ilala kwani hawezi kuzindua mradi ambao tayari Meya alishauzindua, kufanya hivyo ni kuonyesha dharau na kutoheshimu mamlaka ya serikali za mitaa ambayo yapo kwa mujibu wa katiba ya nchi. Hivyo nashauri Mhe. Makonda afute ratiba ya kwenda kufungua/kuzindua daraja hilo.
Meya pia amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Msongela Nitu Palela kumshauri mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutokubali kuingizwa mkenge na Mhe. Bonah M. Kaluwa kwenda kufungua/kuzindua mradi ambao tayari Manispaa tumeshaufungua rasmi Mbele ya vyombo vya habari. Aidha, asingependa kuona Mkurugenzi ama mtumishi yeyote akishiriki kuanzisha mgogoro huo wa kiitikadi. Sisi Ilala tumekubaliana kuwahudumia wananchi wetu bila ubaguzi wa aina yeyote ya kiitikadi sisi ni wamoja hatuna sababu ya kugombani fito wakati tunajenga nyumba moja. Miradi iko mingi ni vema Makonda akazindua miradi ambayo hatujaizindua alisema Kuyeko.
Mhe. Kuyeko pia amemtaka Mhe Bonah kuachana na siasa za maji taka za kutaka kuwatumia viongozi wa ngazi ya juu kutumika kuanzisha vita za kisiasa kwenye Manispaa ya Ilala.
Mstahiki Meya ametumia nafasi hii kuwaomba wananchi wa Ilala na viongozi wote kuendelea kuwa na ushirikiano na kutokubali kuvurugwa na mtu yeyote kwa njia ya itikadi za kisiasa.