Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko amechangia Tsh.milioni tano katika shule ya msingi Bonyokwa kwaajili ya kuchochea maendeleo ya kitaaluma shuleni hapo.
Aidha,mchango huo aliutoa juzi wakati akishiriki kikao cha wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.
Kikao hicho ambacho kiliitishwa na Kamati ya shule kikiwalenga wazazi wa wanafunzi wanaosoma darasa la saba ambao wanatarajiwa kuhitimu elimu ya darasa la saba (7) mwaka huu.
Lengo la kikao hicho ni kujadili mpango na kuweka mikakati ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Bonyokwa alisema wameamua kuitana ili kupanga mikakati ya pamoja ili tuwasaidie watoto wetu wafaulu mtihani wao wa mwisho. Tumeshutushwa na matokeo ya mwisho ya darasa hili ambao sasa ndio wako darasa la saba. Ili ufaulu mtihani wa taifa mwanafunzi anatakiwa apate maksi 250 lakini matokeo yanaonyesha katika mtihani wao wa kuingia darasa la saba mtu wa kwanza alipata maksi 159 na wa mwisho alipata maksi 48, kwa matokeo haya bila ya sisi wazazi, walimu na watoto kutochukua jitihada maalum basi hakuna matumaini kwa watoto wetu kufaulu mtihani wa taifa, alisema mwenyekiti.
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliwataka wazazi washirikiane kwa pamoja katika kuwasimamia watoto/wanafunzi ikiwemo kukagua madaftari yao wanaporudi nyumbani. Sisi kwa upande wa walimu tumejipanga kuwapa mafunzo ya kiwango cha juu, ikiwemo kuwapa mazoezi na mitihani ya Mara kwa mara ambapo mtihani hiyo itafanyika kwenye karatasi watakazo tumia kwenye mtihani wa mwisho ili wazizoee, alisema Mwalimu.
Hata hivyo, Mstahiki Meya aliwapongeza kamati Kamati ya shule ya Bonyokwa kwa kushutushwa na matokeo hayo na kisha kuamua kuchukua hatua ili kufanikisha wanafunzi hao wa darasa la saba kujiandaa vyema na mtihani wao wa mwisho na mipango na mikakati ya kuboresha elimu kwa ujumla kwa shule hiyo.
Mhe. Kuyeko amewataka pia kudumisha utatu mtakatifu kwa maana ya ushirikiano wa walimu, wazazi na watoto na zaidi ya yote nikupendana. Wazazi wapendeni walimu na muwathamini na kuwapa ushirikiano wa kutosha alisema Mhe. Kuyeko.