Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Lets go back to 1950, when it was Tanganyika African Association, then Tanganyika African National Union and later Chama Cha Mapinduzi..
Like wise from Shirazi Party and later Afro Shirazi Party to Chama Cha Mapinduzi..
CCM kilianza kama Chama cha kupigania Uhuru, kisha kikawa Chama cha kujenga Taifa na Utaifa ambao uliambatana na Muungano, kikageuka kuwa Chama cha Kijamaa (Nationalistic and African Socialism), kikaendelea kuwa Chama cha kukomboa nchi zingine za Afrika (liberation movement), kisha kikabadilika na kuegemea kwenye sera za kiliberali za kiuchumi n sasa ni kibepari.
Je chama hiki kina Legacy na Identity gani? Je ni watu ambao hungia humo na kukibadilisha badilisha bila na kuwa na lengo maalumu au kushikilia misingi na mihimili halisi ya tangu TAA, TANU na hata ASP kuwa ni chama cha kumkomboa mnyonge?
Je chama cha Mapinduzi kina itikadi gani itakayokifanya kionekane kwa upekee bila kuonekana kana kwamba ni chama ambacho kipokipo na hakina itikadi, sura au mwelekeo?
Je tukifanyia uchambuzi na tathmini ya tangu asili ya CCM miaka karibu 70 iliyopita mpaka leo hii, tunaweza kudai ni chama madhubuti kinachosimamia misingi yake ya kiitikadi bila kuyumba au ni sawa na gome a pango ambalo kila anayeingia huligeuza na kulirembesha anavyotaka?
Je kutafakari kwetu huku, kunaweza kutupa taswira fasihi ya mfumo wa kisiasa Tanzania na vyama vya kisiasa kuwa ni vyama visivyo na itikadi inayoeleweka na kuishia ni vyama vinavyofanana ila tofauti ni za kibinafsi za kibinaadamu na si za kiitikadi na kifalsafa?
Je misingi ya awali ya kuanzisha CCM itaweza kupimwa vipi kwa kufananishwa na vyama kama Labour na Conservative vya Uoingereza au Republicans na Democtrats vya Marekani?
Je CCM ni chama kinachoelea na kwenda na wakati bila kuwa na mfumo, falsafa na itikadi imara ambayo itawafanya wanachama wake wafuate misingi ya chama na si chama kufuata matakwa ya Wanachama walio na nguvu au kwenye utawala wake?