Metacha Mnata punguza matatizo haya

Kalolelo

Senior Member
Oct 17, 2018
164
244
Unadaka vizuri tatizo lako ni hili umeanza makosa ya kupoteza muda wakati timu inahitaji ushindi mfano mechi dhidi ya Zesco far es salaam hata kule Zambia
 
Wachezaji wetu wafundishwe ni wakati gani wa kupoteza muda. Sasa kama huyo Mnata Mechi ya Zesco hapa Dar anadaka mpira anapoteza muda kisa Yanga anaongoza goli moja wakati ilikuwa ni mechi ya Champions League na sio Vodacom Premier league. Ilitakiwa kila anapodaka mpira yeye anaanzisha counter attack aidha kwa kurusha au kupiga mpira mbele haraka ukizingatia Ngasa alikuwa kashaingia na kashawafanya mabeki wa Zesco wamechanganyikiwa na mikimbio yake.

Lakini naangalia ligi kuu ya hapa bongo wachezaji wengi hawajitambui kabisa tena wengine wapo kwenye hivi vilabu vikubwa viwili. Unakuta Simba au Yanga ameshampiga labda Kagera goli tatu basi wachezaji wataanza mbwembwe kibao mara kisigino, kanzu na baadae wanaanza kupoteza muda wanasahau kuwa kwenye ligi ukipata timu dhaifu tena mwanzoni mwa ligi funga hata goli kumi kwani mwishoni mwa ligi bingwa anaweza kuamuliwa kwa magoli ya kufunga na kufungwa. Pia mwishoni hizi timu zinazoonekana dhaifu kuzifunga hata goli moja tu inakuwa ni shida kwa sababu zinakuwa zinakwepa kushuka daraja.

Na siku zote mazoea hujenga tabia, wachezaji wetu wanajizoesha kupoteza muda kwenye michezo ya ligi kuu hata kama timu inaongoza na tabia hiyo inapokomaa wanaipeleka kwenye michezo ya kimataifa wanajikuta wanapoteza muda hata pasipostahili. Hili makocha na viongozi walipigie kelele mpaka liingie vichwani mwa wacheaji wetu waelewe ni wakati gani timu inatakiwa ipoteze muda na wakati gani timu iendelee kupambana.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom