Meseji za comrade Lowasa zanaswa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meseji za comrade Lowasa zanaswa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joseph Peter, Mar 8, 2012.

 1. J

  Joseph Peter Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Meseji za komredi Lowassa zanaswa  • Chadema kumng'oa mgombea ubunge CCM, mikakati yasukwa


  • Wengine kortini, meneja kampeni asema ‘nilijua tu'


  Na Waandishi Wetu, Arusha, Dar

  WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiwa kimempitisha mgombea wake wa ubunge Arumeru Mashariki, Siyoi Sumari, kwa kuegemea kigezo cha manufaa ya kisiasa (political expediency) badala ya misingi ya kanuni za maadili (principles), upepo umegeuka kwa mgombea huyo na sasa, anaweza kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho kwa njia mbili, ama kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa au kwa pingamizi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Raia Mwema, limeelezwa.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kimemsimamisha mwanachama wake, Joshua Nassari, sasa kinaendelea kukusanya ushahidi wa matumizi ya rushwa yanayoelekezwa kwa Sumari, ili kumuwekea pingamizi NEC, ambako, mgombea anaweza kuenguliwa kama anahusishwa na tuhuma za rushwa.

  Kwa mujibu wa taratibu za NEC, pingamizi huwekwa mara baada ya tume hiyo kuteua rasmi wa wagombea wa vyama kwa kuzingatia majina yaliyowasilishwa kwao na vyama husika.

  Kuhusu mkakati huo wa Chadema, Mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri wa chama hicho, John Mrema, amemueleza mwandishi wetu kwamba chama chake kinakusanya ushahidi na kikijiridhisha, kitaweka pingamizi.

  Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa Chadema kuvizia kumuwekea pingamizi Sumari (baada ya tume kufanya uteuzi rasmi wa wagombea), taarifa zaidi zinaeleza kuwa Takukuru inaweza kuwafikisha mahakamani baadhi ya wanachama wa CCM, wanaohusishwa na matumizi ya rushwa wakati wa mchakato wa upigaji kura za maoni ndani ya CCM, Arumeru Mashariki.

  Katika taarifa hizo za Takukuru, mgombea Sumari naye anahusishwa katika uwezekano wa kufikishwa mahakamani pamoja na baadhi ya wanaCCM wanaotajwa kuwamo katika harakati za kumsaidia kushinda.

  Meneja wa Kampeni za CCM Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba, amelieleza Raia Mwema; "Tunatarajia mambo matatu katika uchaguzi huu. Kwanza, tutawekewa pingamizi, hasa na Chadema, si kwa sababu mgombea wetu ana matatizo bali kwa wao kuhofia kushindwa.

  "Pili, tunataraji kushinda na tatu, tunajua wao watakwenda mahakamani kufungua kesi ya kupinga matokeo kwa sababu ni kawaida yao, wagombea wengi walioshindwa wamekuwa wakifungua kesi."

  Juu ya taarifa za yeye kuhojiwa na Takukuru kuhusu sakata la rushwa linalohusishwa na Sumari na wenzake, Mwigulu alisema: "Nimehojiwa kwa dakika kati ya 40 na 60 lakini na mimi pia nimewahoji baadhi ya mambo nikiwa kama kiongozi wa kampeni. Lakini najua mgombea wetu hana tatizo kama hao anaohusishwa nao ni wao, hakuna jambo linalomuunganisha nao kwamba aliwaelekeza kufanya hivyo."

  Katika hatua nyingine, mawasiliano ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi yaliyonaswa na vyombo
  vya dola wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM, Arumeru Mashariki "yamewaumbua" baadhi ya vigogo wa juu wa chama hicho, namna walivyoshiriki vitendo vya rushwa kumpitisha mgombea Siyoi Sumari.

  Mawasiliano hayo ni ya vigogo na makada wanaoelezwa kuwa ni wa mtandao wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, Edward Lowassa, ndani ya CCM, ambaye anadaiwa kumuunga mkono Siyoi Sumari,ambaye pia ni mkwe wake.

  Imedaiwa kuwa mawasiliano hayo yalifanyika kati yaFebruari 20 na Machi mosi, mwaka huu, ikiwa ni kipindi ambacho kulikuwa na mchakato wa kumpata mgombea wa ubunge kupitia chama hicho.

  Taarifa zinasema miongoni mwa mawasiliano hayo ni kati ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya Monduli, Ezekiel Joseph Mollel, ambaye alinaswa na Takukuru katika baa ya Levis, iliyoko eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, akiwa katika harakati zinazodaiwa ni za kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Takukuru Arusha, Mbengwa Kasumambuto, pamoja na Mollel, wengine waliotiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa ni aliyekuwa mgombea wa nafasi ya ubunge Arumeru Mashariki, Elirehema Kaaya ambaye ni katibumwenezi wa CCM, wilaya ya Nyamagana, Mwanza, nadiwani wa kata ya Mbuguni ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini ya tanzanite Thomas Mollel "Askofu" na katibu wa hamasa wa UVCCM, wilaya ya Arumeru, John Nyiti.

  Kasumambuto alisema Takukuru bado inaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine zaidi ya watatu waliokimbia na kutelekeza pikipiki walizokuwa wakizitumia baada ya kukurupushwa na wenzao wakakamatwa, ambao majina yao yanahifadhiwa ili kuepuka kuingilia uchunguzi.

  Wana-CCM ambao simu zao zimenaswa katika mtandao wa mawasiliano hayo ni pamoja na Hussein Bashe; mwenyekiti UVCCM Arusha, James Millya, katibu UVCCM Arusha Abdalah Mpokwa, katibu UVCCM Monduli, Ezekiel Mollel na Siyoi Sumari mwenyewe, pamoja na makada wengine.

  Taarifa lilizopewa Raia Mwema kutoka vyanzo kadhaa zinaoonyesha kuwa kwa nyakati tofauti, kati ya Februari 20 hadi alipokamatwa, katibu huyo wa UVCCM Monduli amekuwa na mawasiliano nabaadhi ya makada ambao wengine si wakazi wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia simu
  yake (namba inahifadhiwa).

  Taarifa hizo zilidai kuwa katibu huyo ambaye kituo chake cha kazi ni Monduli alikwenda Arumeru kwa maelekezo ya kinachodaiwa kuwa mtandao wa Lowassa kusaidiakumpitisha Siyoi.

  Moja ya mawasiliano ya ujumbe wa simu unaodaiwakutoka kwa James Millya kwenda kwa katibu huyo unaeleza: "Pole sana nipo Nairobi lakini hebu onana naMheshimiwa (jina linahifadhiwa) umwambie haya mambo atakusadia. Ninakupa namba zake muda huu, Yeye ni mtu anafanya kazi serikalini na ana uwezo wa kusaidia kama jambo hili lina uonevu wa aina yoyote".

  Ujumbe huo wa Millya ambao hata hivyo haukuweka bayana ni msaada upi Katibu huyo wa UVCCM alikuwa anauhitaji, ulirekodiwa Februari 26 saa 8:46 mchana, na baada ya dakika mbili, Millya alituma ujumbe wa kumpelekea namba ya simu ya ofisa huyo wa Serikali ambaye anafanya kazi katika moja ya idara nyeti.

  Mawasiliano mengine ambayo yanaelekeza kumpa maelekezo Katibu huyo ni kutoka kwa mtu anayeitwa"Comrade Lowassa" ambaye alifanya mawasiliano ya ujumbe mfupi (sms) Februari 29 saa (9:45).

  Ujumbe huo kutoka simu (namba inahifadhiwa) ulisomeka: "COMRADE hatuna muda tena wa kupoteza. Kuna mambo mawili makubwa, moja kuendelea kuwapanga vijana, kuomba kura na kuwahamasisha wajumbe kuendelea kujitokeza mkutanoni."

  Ujumbe huo uliendelea: "Mbili kuhamasisha vijana wengi wa kutosha kujitokeza kesho maeneo ya ukumbini kulinda kura kwa sababu wamejipanga kuchakachua.Naomba wewe unipe mpango-kazi sasa hivi"

  Mawasiliano hayo yanaoonyesha kuwa siku hiyo hiyo saa 9:53 "Comrade Lowassa" alituma ujumbe: "Sawa,kiasi gani? Mpokwa anasemaje? (Mpokwa ni katibu wa UVCCM mkoa wa Arusha) na saa 11:04 alituma ujumbe mwingine uliosomeka; "Usimweleze Mpokwa, endelea na kazi"

  Aidha, katika ujumbe mwingine "Comrade Lowassa"anamtahadharisha katibu huyo wa UVCCM kuhusu kuwapo maofisa wa Takukuru ambao walikuwa wanamfuatilia mgombea Siyoi Sumari na ujumbe huo ulisomeka: "Maafisa wa Takukuru waliopo Arumeru Mashariki kwa kumfuatilia Siyoi ni Adam Bwana, Seleman Mtunda, wafupi weusi,na Jacline Kapile"

  Mawasilaino hayo yanaoonyesha zaidi kuwa katibu huyo pia aliwasiliana na mtu anayedhaniwa kuwa ni naibuwaziri Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri na ujumbe wa mwanri ulisomeka: "Kaka,suala lako ni zito, na kuna viongozi wenzangu wa mkoa huu. Ungekuwa Moshi sawa. Na suala lenyewe ni la siasa, lingekuwa lako binafsi pia ungeweza.Unataka kunitia kitanzi?" Ujumbe huo wa Mwanri ulitumwa Februari 20 saa 9:15.

  Aidha, katibu huyo katika simu yake sehemu ya kutuma ujumbe (sent) inaonyesha kuwa alimtumia ujumbe mtu anayeitwa "Comrade Lowassa" na H.BASHE kuhusu hatua mbalimbali walizofikia katika mchakato wa uchaguzi huo hasa kuwafikia wajumbe wa mkutano mkuu.

  Ujumbe kwenda kwa "Comrade Lowassa" Februari 28 unasomeka: "Comrade nakushukuru sana kwa kunisadia simu, Bananga ameniambia umenitumia 150,000 japo bado nadaiwa 80,000 iliyotumika.

  Na tarehe 29 alituma tena ujumbe kwa "Comrade Lowassa" akieleza kuwa: "Nimewasiliana na Nyiti(katibu hamasa wa Vijana wilaya ya Arumeru) pamoja na kundi lake wapo 10. Wanasubiri, wameniambia wanahitaji mafuta ya pikipiki sita na hadi sasa kata sita ndiyo korofi ila Mbuguni nitakwenda na Nyiti.

  Ujumbe mwingine ulisomeka: "Pili amenipa 500 (500,000)? Na tumekubaliana mimi nimbane Nyiti, Je niwaeleze akina Mpokwa au niendelee na mchakato kaka?" na baada ya muda mfupi alituma ujumbe mwingine "Niko na Nyiti na wenzake tunapeana maelekezo nikimaliza nitakujulisha.

  Aidha ujumbe mwingine ulitumwa kwa H.BASHE (Hussein Bashe?) mwenye simu (namba inahifadhiwa) na ujumbe huo ulisomeka: "Hadi sasa kata za Kikwe, Ngarenanyuki, Songoro, Leguruki, Nkoarangandizo zinazonitesa."

  Akizunguzmia taarifa hizo, Kamanda wa Takukuru Mbengwa Kasumambuto, alieleza kuwa taasisi hiyo bado inafanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ni mapema mno kujenga mazingira ya kesi na kupeleka suala hilo mahakamani.

  Mgombea wa CCM anayetuhumiwa, Siyoi Sumari,amekanusha kuwa wanachama wa CCM waliokamatwa walikuwa wanamfanyia kampeni katika uchaguzi huo.

  "Nawashangaa wanaonihusisha mimi na suala hilo la rushwa. Mimi kama Siyoi sijawahi kupanga wala kumtuma mtu yeyote kumshawishi ye yote kwa fedha ili anifanyie kampeni. Hayo ni mambo yanayozushwa kwa lengo la kuniharibia kwa wananchi," alisema Siyoi.

  Uchaguzi wa marudio kumpata mgombea wa CCM katika jimbo hilo ulifanyika Machi Mosi kwa mgombeaSiyoi Sumari kupata kura 761 na kumtupa mbali mpinzani wake, William Sarakikya aliyepata kura 361.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  haki itatendeka kweli??
   
 3. C

  Cupid 50mg Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh napita tu hapa!!.
   
 4. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yetu macho,ila wananchi tutakapochoshwa na adaha hizi za watoa rushwa wakubwa kujulikana na bila kuchukuliwa hatua na kuamua kuwaadhibu sisi wenyewe zisijetoka lawama kua ni uvunjifu wa amani,hawa watu wanaotoa rushwa wanatugharimu sana
   
 5. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa haraka haraka tu mtu makini anatambua kabisa hata uunganishe vipi hizi meseji hamna kesi yeyote ya mambo ya rushwa hapa.
   
 6. Chihuahua

  Chihuahua New Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kamba hukatikia pembamba, na siku ya kufa nyani miti yote huteleza
   
 7. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhh. kazi kweli kweli..
   
 8. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Gazeti la Raia Mwema limefilisika, linaandika mabaya ya upande mmoja na mazuri ya upande mwingine, last week walikuwa wanastory nzuri kuhusu serikali, halafu picha wakaweka ya Sitta wakati hakukuwa na link yoyote kati ya Sitta na hiyo story, nikajua limegeuka Propaganda mashine ya Sitta na Genge lake, Ulimwengu should think again!
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  hadi sasa sionirushwa.. Naona mikakati Mbayo vyama vyote wanatumia
   
 10. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kuna kesi gani hapo? Simply a distraction!
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  thanks eliphaz
   
 12. m

  mzizi dawa Senior Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa upofu wako nikweli.
   
 13. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nini maana halisi ya kufilisika mkuu
   
 14. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Rushwa iko wapi hapa? Jamani! mbona ni mikakati tu! hizi dots itabidi ziungwe kwa gundi ya mbao ili zilete maana!
   
 15. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Huu utaratibu wa vyombo vya dola kufanya kazi kupitia vyombo vya habari umeanza lini? Mtu unaruhusu "ushahidi na vielelezo vyake" kuanikwa hadharani kabla hata ya kumaliza uchunguzi na kufungua kesi kama "ushahidi" unatosheleza ina maana gani?

  Itapendeza CCM wakigaragazwa kupitia sanduku la kura na sio mahakamani ili wajue upepo ulivyobadilika
   
 16. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Magamba, wot's cookin'?:lol:
   
 17. +255

  +255 JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Bashe na Lowassa ni watu wa Rostam, Rostam mtu wa Voda, ka ni kweli mbona ni virahisi kwa wao kupoteza ushahidi kama walikuwa wanatumia mtandao huo.
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Raia Mwema limeanza kupoteza dira, hebu unganisheni na hii hapa chini;

  Update: Kura ziliporudiwa William Sarakikya hakuweza kuambulia hata nusu ya kura alizopata Sioi Sumari! Sasa hii habari Raia Mwema waliitoa wapi? Poleni Raia Mwema kwa kukubali kutumiwa!
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  TAKUKURU ingekuwa siyo taasisi ya chama cha mapinduzi tungesema vinginevyo.
  Lakini kwa kuwa ni taasisi yao tukae tukiangalia.
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,098
  Likes Received: 6,562
  Trophy Points: 280
  huyu EL kumbe ana dhambi nyingi hivi,
  huko nigeria anamfuata mungu gani.
   
Loading...