Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,439
- 10,780
Mwaka 2004 pale Fallujah paligeuka machinjio baada ya kuwa pametulia kitambo! Askari wanne Mamluki Scott, Jerry, Wesley na Mike, waajiriwa wa kampuni ya Kijeshi ya Marekani Black water walikodiwa Kwa mkataba maalumu kusafirisha chakula. Wakati huo Iraq ilikuwa inawaka Moto Kwa Vita. Misafara mingi ya kigeni ilikuwa ikilindwa Kwa uthabiti na Askari wageni au wa kiarabu.
Kikundi cha Al Qaeda adui mkubwa wa Marekani kilijipenyeza maeneo kadhaa ya Iraq Kwa mwavuli wa kuwasaidia waislamu waliokuwa wakionewa na uvamizi wa kigeni. Kiongozi shupavu wa kundi hili la kigaidi eneo hili aliitwa Ahmad Hashim Al Isawi. Alikuwa ni mtaalamu wa logistics za Kijeshi na mpiganaji mwenye ushupavu wa utumiaji wa siraha na human toucher mpaka akapewa jina la The Butcherer (mcharanga nyama). Katika harakati zake za kimikakati aliwasoma wamarekani na king'amua maeneo mahsusi ya kuvamia Kwa mafanikio. Moja ya maeneo ilikuwa ni misafara ya Kijeshi au misaada.
Kikundi chake kikiwa kimejizatiti Kwa maguruneti, Rocket launchers, AK 47 na mapanga kilifanya mauaji kadhaa ya adui.
March 2004, msafara wa Wamarekani wenye chakula na vifaa vingine ukiwa unalindwa na Mamluki wa Black water ulivamiwa na Kikundi cha Al Isawi. Askari wa kimarekani walijaribu kujitetea lakini vijana wa Al Isawi walikuwa wamejipanga vizuri. Kila walipogeuka walipewa kipigo kikali mpaka wakapoteza pambano. Mchinjaji Al Isawi baada ya kudhibiti Uwanja wa mapambano aliwaua kikatili Askari wanne wa Black water. Kikundi cha Wairaq wenye hasira walijitokeza wakishangilia. Waliiburuta miili ya Wamarekani na kuanza kuitandika bakora Kwa hasira na kuikojolea au kuikanyaga kanyaga. Baada ya hapo, miili iliunguzwa. Ikiwa bado inafuka moshi, Al Isawi na Al Qaeda wenzake waliiburuza mitaani huku watu wakishangilia Sana!
Safari hii ya kutisha iliishia mto Euphrates kisha ikaning'inizwa kwenye daraja la zamani.
Picha za miili iliyoharibika ya Askari hao zilisambaa ulimwenguni kote. USA wakaamua kutuma Askari Fallujah, hapa ndo ukawa mwanzo wa machafuko zaidi.
Mwaka 2009 makomandoo Seal Team walifanikiwa kumkamata Al Ilawi na akahukumiwa Kijeshi na mahakama za Seal. Alirudishwa Iraq na kunyongwa kwa kutundikwa na serikali.
Askari wa kukodiwa wamekuwa wakitumika hata kabla ya Kristo. Ni ajira ambayo Askari toka nchi moja wanakodiwa kupigana nchi nyingine au ndani ya nchi hisika. Wao hupigana Kwa pesa na hawawi sehemu ya mgogoro.
Pale Libya Askari wengi wa mbabe wa kivita Khalifa Haftar ni wakukodiwa. Wengi hutoka Urusi, Libya, Lebanon na nchi nyingine.
Ni ajira nyingine inayoingiza pesa nyingi duniani. Black water ya USA inaaminika kuwa na Mamluki nchi nyingi kama Askari au wapelelezi. Viongozi kadhaa wa mataifa wamekuwa wakiuliwa (assassination) na Askari wa kukodiwa ili kupoteza ushahidi
Tuwe na siku njema!
Sent using Jamii Forums mobile app