Mercenaries Barani Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mercenaries Barani Afrika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Estmeed Reader, Apr 22, 2010.

 1. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miaka ya miongo ya 60 na 70 ilikuwa ni ya kutamalaki kwa askari wa kukodiwa (mercenaries au kwa jina lingine, the dogs of war) kwenye uwanja eti wa “vita” wa Afrika. Waliokuwa macho miaka hiyo waliona askari hao wakitamba katika Bara la Afrika, kusini mwa Sahara.

  Waliokuwa wakiwalipa hao askari ni nchi za Magharibi, hususan Amerika, Uingereza na Ufaransa. Tulishuhudia watawala/viongozi-ota vibaraka wa Afrika wakila njama na nchi hizo ili kuiweka Afrika chini ya himaya zao dhidi ya Warusi na Wachina (makomunisti) na nchi nyinginezo za majamaa!

  Askari wa kukodiwa walionekana mbele ya nchi hizo za Magharibi kuwa ni askari “watakatifu” (“Twendeni askari...watu wa Mungu...Yesu yuko mbele...ametangulia...tumwandame juu”.

  Mpaka leo hii, hakuna hata nchi moja iliyo huru ya Afrika iliyoibua suala la kuzishitaki Nchi za Magharibi kwa kupanga, kukuza, kuendleza na kusaidia kwa hali/mali na saikolojia na kuwatuma hao mercenaries au kwa jina lingine, the dogs of war!

  Kwa nini nasema haya yote? Jibu: Hao askari wa kukodiwa (mercenaries au kwa jina lingine, the dogs of war) kwa lugha ya leo walikuwa ni ma-“terrorists”.

  Kweli, wahenga walisema, “Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu ni mchungu.” Ona jinsi wanavyoweweska na kuhangaika kudhibiti ma-“terrorists” wa leo! Juzi tu Amerika imeitisha na kuwaleta viongozi wengi wa dunia kubadilisha mawazo na kutoa msimamo wa kudhibitiwa ma-“terrorists” wa leo!

  Baadhi ya viongozi/watawala wa Afrika nao walikaribishwa na Rais Obama bila ya kuibua hilo la askari wa kukodiwa (mercenaries au kwa jina lingine, the dogs of war) walivyodororesha maendelo ya Bara la Afrika!

  Tuamke!
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Walikuwa wanaitwa Mamruki.
   
Loading...