Meno

mjambaji

Senior Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
174
Reaction score
98
Hili jambo huwa linasumbua sana ubongo wangu kwa miaka mingi sasa na kila nikijiuliza huwa sipati jibu kwamba kwa nini wanyama kama vile; mbwa, ng'ombe, sokwe n.k huwa hawang'oki wala kupata matatizo ya meno kama sisi binadamu licha ya kwamba wao huwa hawapigi mswaki ? Nahitaji mawazo yenu wadau.
 
Matatizo ya meno huletwa kwa sehemu kubwa na sukari au vyakula vyenye asili hiyo. Acha kula sukari etc nawe utafanana na hao ulio wataja. Either sokwe wa Zoo wanao pewa soda baada ya muda nao huoza meno.

Over.
 
Sawa nimekupata mkuu lakini bado Nina swali, kwa hiyo unamaanisha nikiacha kula vyakula vya aina ya sukari na nisipokuwa napiga mswaki kabisa kama hao wanyama bado ninaweza kuwa na meno imara kama yao?
 
We nawe sasa usipige mswaki ili iweje? au unadhani hayo maharage yanayobaki ktk meno yatajitoa yenyewe, au ndo kusema unataka na Simba nae apige mswaki eh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…