JacobMushi
Member
- Sep 18, 2018
- 22
- 30
Pole sana!Ahsante kwa ushauri mzuri dada Lizzy.
Ahsante sana.
Ningependa kukusahisha kuwa silalamiki juu ya tatizo langu anymore,kuna kipindi fulani nililalamika lakini sasa najitambua hivyo katika thread hii sijalalamika pia.
Ni kweli Volunteer,field na ajira nimeshindwa kupata kutokana na tatizo langu.
Nataka kukomboa cheti baada ya kupata watu wenye uelewa juu ya ajira maalumu za serikali,ambapo wapo willing kunisaidia kuapply ajira hizo ndiyo maana nataka nipate cheti niweze kufanya mchakato huo,hatimaye ajira iweze kunikomboa kimaisha.
Vilevile kujiendeleza kielimu nitahitaji cheti hiko pia.
Mimi si mnyonge,nina amani sana even licha ya kuwa na hili tatizo nilipata marafiki wenye busara walionisaidia kujitambua zaidi na najitambua sana.
Kipindi fulani nilikata tamaa ya kuendelea na masomo,it was Wakonta na Aneth gerana walioniinspire kukaza moyo hadi nikarudi shuleni na kumaliza masomo.
Nakiri Wakonta hakuwahi kuwa mnyonge,she was always bright,thats why aliniinspire sana.
Wakati mwingine maisha yalinisukuma kulalamika na kuwa mnyonge kwa sababu...katika hali ya kawaida kuwa rejected kwa kosa ambalo halikuwa kusudi lako inaumiza pia,mimi ni binadamu tu hisia ninazo.
.hali halisi ya maisha mfano kulala na njaa,kula mlo mmoja,kulala sehemu isiyo salama,kuugua na kuonekana like si kitu si mtu hata kwa familia yako mwenyewe haya yalipelekea kuwa dhaifu sana kiasi nisimudu vibarua vya kutumia nguvu,miguu inaishiwa nguvu,kutetemeka mikono na kizunguzungu kikali.
Hivyo ni baadhi ya vitu vilivyoninyima amani na kunifanya niwe vile(kulalamika sana) lakini sasa silalamiki tena.
Suala la kujiajiri ni kipaumbele changu pia,lakini sina kitu kwa sasa kuweza kujiajiri nimefanya juhudi nyingi na jitihada nyingi sana lakini sijafanikiwa.
Kadhalika napambana sana dada natamani mafanikio ya watu kama Wakonta na Aneth,wapo wengi wa aina hii waliofanikiwa na wanaoendelea na mapambano.
Lakini hawakufanikiwa peke yao,kama ilivyo kwangu nipo peke yangu si ndugu si marafiki,hii inaniwia ugumu lakini si sababu ya mimi kuacha kupambana,bado najaribu.
Ndio maana nipo hapa leo,silalamiki bali najaribu kujikwamua.
Nashukuru sana kaka,nakuja katika email yako.Naomba kufahamu unachoweza kukifanya vizuri zaidi wewe mwenyewe. Kimoja ambacho nimekiona ni kwamba unajua na unaweza Kuandika labda kama kuna mtu anakuandikia. Kama umeweza kuitumia hii JF Kuandika tatizo lako unaweza pia kuanzia na Kuandika huku ukiandelea na hustle zingine. Kwa kupitia Kuandika unaweza kupiga hatua kadhaa pia ishu kuchagua kile unachopenda kuandika.
Angalia vile ambavyo unaweza kufanya kama unaona havitoshi viongeze, jiboreshe wewe mwenyewe kwenye vitu mbalimbali ambavyo viko kwenye uwezo wako. Naamini kuna kitu Kikubwa unaweza kufanya.
Tunaweza kuwasiliana kwa ushauri zaidi kwa email wisdom@jacobmushi.com
Kamwene kamwene take no 7 tuendeleeHilo tangazo lipo sawa kweli mkuu,?
Hujaweka namba za simu,
Hujaweka account za bank
Hujaweka physical adress
Mtu kama anakuchangia anakuchangia vipi ?
Ishu ndo mtaji...utapata tu
Ishu ni utapenda kufanya kipi kama kujiajiri ukiwa utapata mtaji?
Andika business idea ambayo utaimudu,ikikamilika waonyeshe watu,itawavutia zaidi kukuchangia ufikie lengo.pia ukishapata mtaji utawaonyesha biashara ulofungua kama uthibitisho
good comment ever, kijana anapenda kulalamika sana badala ya kupambana zaidi, by the way kwanini watu wa kuchukie, vijembe na dharau bila sababu yoyote??
Naomba mkuu Maxence Melo na MOD wengine watuongoze kupata taarifa za taasisi inayoshikilia chetu cha mhusika yaani kiasi chote anachodaiwa na njia wanazopokea malipo kama hayo e.g Account halafu uongozi utusaidie kupokea michango yetu na itakapotimia waiwakilishe kwa wahusika (Taasisi husika). Nadhani hili likifanikiwa itakuwa sehemu ya mchango wa JF kwa jamii.
Ahsante
Naomba mkuu Maxence Melo na MOD wengine watuongoze kupata taarifa za taasisi inayoshikilia chetu cha mhusika yaani kiasi chote anachodaiwa na njia wanazopokea malipo kama hayo e.g Account halafu uongozi utusaidie kupokea michango yetu na itakapotimia waiwakilishe kwa wahusika (Taasisi husika). Nadhani hili likifanikiwa itakuwa sehemu ya mchango wa JF kwa jamii.
Ahsante
Ahsante sana kaka naandaa sasa.Nahisi hili ndilo la msingi sana kaka. Andaa business plan ilete jamvini watu waisome na ikiwa vzuri tutakusaidia tu, Binafs naahidi kukusaidia kwa chochote Mungu alichonijalia. Natamani kukusaidia ila fanya kuandaa business plan. Fanya Biashara cheti utakifuata baadae kaka.
Polee sana, Mungu akufanikishie hili.
Mie ninamashaka na suala la kusema watu walimchukia na kumkebehi, kitu hiki hakiniingii akilini kabisa. Na watu unaosema walikukejeri ni wanafunzi na wakufunzi, kuna kitu hakipo sawa kwa ndugu yangu. Jikubali wewe binafsi kuwa pamoja na udhaifu wako bado unanafasi ku wa ya kufanikiwa. Kuna watu ni walemavu kulivo hata yeye ila wamekomaa. Hebu basi afanye kutengeneza business plan na watu watamsaidia ukizingatia yeye amesomea mambo hayo. Atanisamehe kama nitamkwaza
Hapana hujanikwaza.
Hakuna mahali nimesema nilichukiwa,bali dharau na kebehi..hizi haziwakilishi chuki na hawawez kuwa wote kaka.
Najikubali sana katka hali hii hii na ndio maana nakumbana na mengi sana kwa sababu sijawahi ona masikio kama sababu yakutotimiza ndoto zangu.
Kujiajiri natamani sana pia,nakumbuka nimewahi kuomba mtaji ila nilichotendewa ckurudia tena kufanya hvyo
Business plan,nimefurahi kwa maoni yenu,naanza leo kuandaa na nitafurahi sana kuona kwa pamoja tumefanya kitu.