Mengi aumiza vichwa vigogo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Mengi aumiza vichwa vigogo

na Deogratius Temba
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI inatafakari hatua za kumchukulia Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, baada ya kutowasilishwa ushahidi kutokana na tuhuma alizotoa kuwa kuna waziri kijana amependekeza abambikiziwe kodi kubwa, ili afilisiwe biashara zake.

Kauli hiyo ilitolewa na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga, alipozungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana.

Alisema kwa sasa serikali ahiitaji tena ushahidi huo, kwani muda aliopewa wa siku saba na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha, baada ya kutoa tuhuma hizo, umeshamalizika.

Serikali ilimpa siku saba Mengi kuwasilisha ushahidi wa tuhuma alizozitoa kuwa kuna waziri kijana ametoa ushauri wenye lengo la kumfilisi biashara zake.

“Siku saba zimepita, ni wazi kuwa haleti tena, na serikali imechukulia kuwa hana ushahidi, maana ukiwa nao unawasilisha unapohitajika, kilichobaki ni kuangalia cha kufanya, serikali haisubiri tena….kama alivyosema waziri, tutachukua hatua.

“Wizara inachofanya ni kuangalia kama ni hatua gani ichukuliwe na jambo gani lifanyike baada ya muda huo kupita na maamuzi ya busara yatafanyika kwa hilo kwani lipo mezani,” alisema Nantanga.

Hata hivyo, alisema serikali ilitoa siku saba kupata ushahidi huo, lakini haikutoa muda ambao itatoa maamuzi iwapo atashindwa kufanya hivyo.

“Sasa hatutaweza kusema wazi kuwa ni lini utaratibu wa kumchukulia Mengi hatua utafanyika kwa sababu inahitaji muda wa kutosha na hata kama angewasilisha ushahidi wake, ingechukua muda kuutolea maamuzi,” alisema.

Alisema suala hilo linafanyiwa kazi kwa uangalifu mkubwa na litakapokamilika, taarifa zitatolewa kwa umma.

Akizungumzia aina ya ushahidi serikali iliyoutaka, alisema wao hawakumweleza Mengi kama ushahidi unaotakiwa ni wa aina gani, kama ni maelezo au ni vielelezo, ilimwachia nafasi na uhuru wa kuangalia mwenyewe na kama angependa kuwasilisha viambatanisho vingi ili kudhibitisha ukweli wa alichokisema, wao walikuwa tayari kuupokea.

Wakati wizara ikitoa msimamo huo, kwa upande wake Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, akizungumzia suala hilo, alisema Jeshi la Polisi halihusiki kwa namna yoyote na siku saba alizopewa Mengi kuleta ushahidi wake wizarani.

Manumba, alisema Mengi alipewa siku saba na Waziri Masha, na si Jeshi la Polisi, hivyo ushahidi unapaswa kuwasilishwa kwa waziri husika.

“Hilo ni suala la itifaki, hatuwezi kuliingilia moja kwa moja, na kumwambia Mengi atuletee sisi ushahidi wake, aliagizwa na waziri atapeleka kwa waziri,” alisema, Manumba na kusisitiza hana taarifa za ushahidi huo.

Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi linahusika na upelelezi wa jalada la kesi iliyofunguliwa na Mengi ya kutishiwa kuuawa kupitia simu yake ya mkononi.

“Sisi tulipokea taarifa kutoka kwa Mengi na akafungua jalada katika kituo cha Polisi Oysterbay kuwa ametishiwa kifo na watu wasiojulikana kupitia simu yake ya mkononi. Polisi wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo na upelelezi ukikamilika, taarifa zaidi zitatolewa na wahusika watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema DCI Manumba.

Alisema jeshi hilo linaendelea kushughulikia na kufanya uchunguzi wa makosa yote yanayohusika na vitisho hasa vya mawasiliano ya kompyuta, simu na aina nyingine za kitekonolojia.

Desemba 3, mwaka huu, Mengi alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa ametishiwa kuuawa na pia kuna waziri kijana amependekeza abambikiziwe kodi kubwa atakayoshindwa kulipa, ili afilisiwe biashara zake. Alidai waziri huyo alitoa pendekezo hilo katika kikao cha juu kinachotambulika.

Kutokana na taarifa hizo, Waziri Masha alitoa muda wa siku saba kwa Mengi apeleke ushahidi wake.

Hata hivyo, siku moja baada ya Waziri Masha kutoa kauli hiyo, Mengi alijibu kuwa siku saba ni nyingi na kwamba yupo tayari kufungwa iwapo itathibitika kuwa kauli aliyotoa ni ya uongo.
 
Na yeye amekuwa kama msanii, jioni hii ametangaza kumsamehe waziri kijana aliyetaka kumhujumu! yalisemwa kuwa huu utaisha kama mchezo wa kuigiza, tunayona sasa
 
This is a game, na hii wizara ya mambo ya ndani kama hawatakuwa careful itaaibishwa sana this time, how do they know kwamba Mengi hana ushaidi. mshika anaweza akawa ata ana tape record, sasa akiweka kwenye ITV itakuwaje?

I think masha has to back off now, he has done enough damage to the trust of the government, and he keeps doing it using so called waongeaji wa wizara...

haaaa i cant wait mengi afanya mambo
 
Back
Top Bottom