Ubalozi wa Tanzania pale Brussels hauna hadhi hiyo kama unavyofikiri. Kwanza huwezi kujua kama kuna ubalozi. Hakuna kiashiria chochote. Wenyeji wanaolizunguka jumba wala hawajui kama kuna ubalozi wa Tanzania eneo hilo. Hii ni kwa sababu ubalozi unamiliki floor moja tu kwenye nyumba ya ghorofa lenye wapangaji wengi. Sheria za Ubelgiji haziruhusu kuningíniza bendera iwapo unamiliki floor moja tu. Isitoshe, kiutendaji, ubalozi wa Ubelgiji unalalamikiwa sana na watanzania waishio huko katika nchi za Ubelgiji, Luxemburg na Uholanzi. Haujitumi kabisa kihuduma na hata kuitangaza nchi ya Tanzania. Watanzania waishio Uholanzi wameshamlalamikia sana Balozi Mlay kuwa analaza mambo mengi japo wanajitahidi sana kumsukuma afanye kitu. Wakati mwingine Watz waishio uholanzi wanafanya kumbukumbu muhimu kama Nyerere day, Muungano, nk., na kumualika balozi ili kumchokoza tu afanye kitu. Wapi bwana!!! jamaa kalala tu! Anatuma wasaidizi!! Kukosekana kwa huduma za heating system kwenye floor hiyo ni dalili wazi za nje za kutowajibika kwa balozi. Sasa, unategemea nini! Ubalozi upo strategic area (makao makuu ya EU, ni kweli) lakini haujitumi!!! Una maana gani?