Sadick Mtulya
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amewataka wanasiasa na wafanyabiashara, kuacha tabia ya kuingilia utendaji wa vyombo vya habari nchini.
Kauli ya Membe inaungana na kauli nyingine za wadau wa kada tofauti kuwa, utendaji wa vyombo vingi vya habari nchini, unaathiriwa kiutendaji kutokana na utashi wa kisiasa na maslahi binafsi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, Membe alisema anachukizwa na tabia ya wanasiasa, wafanyabiashara na wamiliki kuingilia utendaji vyombo hivyo.
Utendaji wa vyombo vingi vya habari nchini kwa kiasi kikubwa unaathiriwa na maamuzi ya utashi wa wanasiasia, wafanyabiashara na hata wamiliki. Tabia yao ya kupiga simu kwa wahariri kushinikiza waandike wanavyotaka wao, ni kati ya mambo yanayonichukiza sana, alisema Membe
Membe alikwenda mbali akisema kama tabia na mwenendo huo ukiendelea, utaathiri mustakabali wa baadaye wa taifa.
Membe alisema kutokana na maslahi binafsi, watu hao hutumia vyombo vya habari kumjenga mtu au kumbomoa ikiwamo kueneza propaganda chafu dhidi ya hasimu wake.
Kibaya zaidi yule aliyeenezewa propaganda chafu au aliyejengwa kwa maslahi fulani, kisha akakosa anaumia sana kisaikolojia na anaweza kufanya uamuzi wowote. Pia, inajenga dhana na hisia tofauti kwa wananchi, alisema.
Waziri huyo ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Mtwara, alisema kama vyombo vya habari vikitumika vizuri na katika muktadha wa kutoa habari za ukweli, kwa kufuata maadili bila kuingiliwa na maamuzi kutoka nje, vitajenga misingi imara ya Watanzania kuendelea na utamaduni wa kupendana, kuaminiana, kutobaguana na wataweza kufikia maendeleo wanayotaka kwa urahisi.
Alifafanua iwapo vitafanya kazi kwa uhuru kama ilivyo kwa vyombo vya habari vya nje, vitaondoa hisia, licha ya dhana mbaya iliyojenga kwa wananchi katika masuala mbalimbali nchini.
Nimekaa nje ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 10, nimeona vyombo vya habari vya huko vinavyofanya kazi kwa uhuru. Kwa kiasi kikubwa vimesaidia kuelimisha, pamoja na kujenga uchumi wa nchi hizo kwa kuwa vinafichua tatizo, vinakosoa mwenendo wa serikali na kutoa suluhisho la tatizo, alisema.