Membe awavaa wanasiasa, wafanyabiashara

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
Sadick Mtulya
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amewataka wanasiasa na wafanyabiashara, kuacha tabia ya kuingilia utendaji wa vyombo vya habari nchini.
Kauli ya Membe inaungana na kauli nyingine za wadau wa kada tofauti kuwa, utendaji wa vyombo vingi vya habari nchini, unaathiriwa kiutendaji kutokana na utashi wa kisiasa na maslahi binafsi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, Membe alisema anachukizwa na tabia ya wanasiasa, wafanyabiashara na wamiliki kuingilia utendaji vyombo hivyo.

“Utendaji wa vyombo vingi vya habari nchini kwa kiasi kikubwa unaathiriwa na maamuzi ya utashi wa wanasiasia, wafanyabiashara na hata wamiliki. Tabia yao ya kupiga simu kwa wahariri kushinikiza waandike wanavyotaka wao, ni kati ya mambo yanayonichukiza sana,’’ alisema Membe
Membe alikwenda mbali akisema kama tabia na mwenendo huo ukiendelea, utaathiri mustakabali wa baadaye wa taifa.
Membe alisema kutokana na maslahi binafsi, watu hao hutumia vyombo vya habari kumjenga mtu au kumbomoa ikiwamo kueneza propaganda chafu dhidi ya hasimu wake.
“Kibaya zaidi yule aliyeenezewa propaganda chafu au aliyejengwa kwa maslahi fulani, kisha akakosa anaumia sana kisaikolojia na anaweza kufanya uamuzi wowote. Pia, inajenga dhana na hisia tofauti kwa wananchi,’’ alisema.
Waziri huyo ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Mtwara, alisema kama vyombo vya habari vikitumika vizuri na katika muktadha wa kutoa habari za ukweli, kwa kufuata maadili bila kuingiliwa na maamuzi kutoka nje, vitajenga misingi imara ya Watanzania kuendelea na utamaduni wa kupendana, kuaminiana, kutobaguana na wataweza kufikia maendeleo wanayotaka kwa urahisi.

Alifafanua iwapo vitafanya kazi kwa uhuru kama ilivyo kwa vyombo vya habari vya nje, vitaondoa hisia, licha ya dhana mbaya iliyojenga kwa wananchi katika masuala mbalimbali nchini.
“Nimekaa nje ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 10, nimeona vyombo vya habari vya huko vinavyofanya kazi kwa uhuru. Kwa kiasi kikubwa vimesaidia kuelimisha, pamoja na kujenga uchumi wa nchi hizo kwa kuwa vinafichua tatizo, vinakosoa mwenendo wa serikali na kutoa suluhisho la tatizo,’’ alisema.
 
mikakati ya 2015 ndio tumeanza/imeanza , kama kama suala udini tuelezane kwa wazi ni akina nani hao wana taka mambo yao yatangazwe na mct/baraza la habari au mahakama ifanye kazi yake?
 
Kabla ya yote mbele ya vyombo vya habari atamke wazi au akemee radio uhuru na habari leo otherwise ahame chama ili apate urais kama anautaka
 
anachosema ni kweli kabisa rostam na magazeti yake wana kazi ya kuwachafua watu wote wanaowahisi kwamba wanataka urais,hivi rostam na kundi lake wakipata huo urais si watatuuza mpaka raia wao. Maana hawa kina membe rostam jk sita lowasa na wengineo ndiyo walikuwa wana mtandao sasa interest zimetofautiana kina el na rostam wamekuja madarakani kwa nia ya kujilimbikizia mali wawe mabilionea kina membe sita mwakyembe wapo kwa maslahi ya wananchi wao hiyo ndiyi tofauti yao mwenye kujua zaidi atujuze
 
Wanakula matunda ya fitina zao. Kwa hili simuonei huruma kama wamemsema yeye, sio sabb simpendi bali sababu ya unafiki wao kama ccm.

Wakati habari leo,mtanzania,uhuru,dailynes,rai n.k walipoungana kumchafua Slaa na CHADEMA walikaa kimya, hata pale dailnewz lilipotangaza matokeo ya urais hata kabla ya kura hazijaisha wote walikaa kimya na kufurahia, magazeti yao yalipoingilia maisha binafsi ya mgombea aliyekuwa anahubiri sera za matumaini na za kulikomboa taifa wao walikaa kimya na walijitahidi kila walivyoweza kuzipotosha.

Kuna wakati Nyerere alisema hakuna dhambi mbaya kama ya ubaguzi, baada ya vyombo vyao vikiwemo vike vinavyoendeshwa kwa kodi zetu kuwabagua upinzani, sasa ubaguzi huo unaendelea na bado mengi tutayasikia maana wote sasa agenda ni 2015.

Ninachoweza kumshauri Membe asiume maneno, kama anaweza awataje majina maana hiyo ndo dawa.
 
Membe Majuto mjuukuu anaya ona leo waliyajenga na yamejikita kwenye jamii wananchi tumelalamika wao hawakujali sasa yatawatokea puani
 
:whoo:Hasira za Mkisi furaha kwa mvuvi. It is too late kwa mbio za uprez.... Change.
 
Hypocrisy. Mwenyewe anatumia gazeti la Mwananchi kujipanga. Hii article benefit wote wawili, Membe na Mwananchi. Mwananchi plays to be independent and Membe is trying hard to be presidential.

Mheshimiwa Membe anaanza kampeni mapema. You will peak to soon. Shauri yako. And you won't become the nominee.
 
Ni mnafiki kama amechukizwa sana kiasi hicho si angelitaja kabisa na vyombo vya habari husika?
 
Kama ndio Mbio za Urais 2015 inawezekana ukawa umechelewa maana labda ungemwambia mjomba wa Masasi akuachie ili hata umalizie Barabara za kule kwani Mjomba alkujengea Daraja la mto Rufiji sasa nafikiri mbio zako zaweza kuwa zimechelewa.

kwanini hukusema haya kipindi hicho hivyo vyombo vya hbr vikifanya hayo?
 
Back
Top Bottom