Habari wakuu, Leo waziri wa mambo ya nje wakati anahitimisha bajeti ya wizara ya mambo ya nje amesema hatarejea tena bungeni kama mbunge, yafuatayo ni maneno ya muheshimiwa;
La mwisho nazungumza hapa leo kama waziri wa mambo ya nje kwenye hotuba yangu ya tisa kwa mara ya mwisho. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru wabunge wenzangu nilioanza nao mwaka 2000 na wabunge wote waliofata wakiwepo wapinzani. Jengo hili ndio linalotoa viongozi mbalimbali wa nchi yetu, sijui ntakua nani lakini siwezi tena kuingia kwenye jengo hili labda nipate nipate hichi nnachokidhamiria, naomba niseme chombo hiki ni cha heshma kubwa katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Nimefanya kazi kama waziri wa mambo ya Nje, kama swala la ushoga hata tulipoenda Comoro kuokoa kisiwa. Ni maslahi ya taifa, tuendelee na moyo huo huo.
Ningependa kuondoka katika bunge hili na impression hii, wale mtakaokuwa na mimi, mtakaokosa kuchaguliwa tutaonana huko nje, mtakaokosa kuchaguliwa na tutapeana taarifa nyingi zaidi. Wale mtakaondelea humu ndani nawatakia kila lakheri.