MELI YA IRAN: Rais mstaafu atajwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MELI YA IRAN: Rais mstaafu atajwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 19, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu

  Toleo la 250
  18 Jul 2012


  [​IMG]


  WAKATI uchunguzi wa kimataifa ungali ukiendelea,Raia Mwema limethibitishiwa kuwa Rais mstaafu aliyepata kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na mmoja wa kigogo wa juu wa sasa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wanahusika.

  Mtandao huo wa kiongozi huyo mstaafu ambaye anazo ndoto za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mwenzake ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wamefanya mpango huo na aliyepata kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia amepata kuwa mbunge wa moja ya majimbo ya uchaguzi mkoani Tabora.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, tayari vyombo vya kimataifa vinaelekea kukamilisha uchunguzi wake na kwamba, majina ya wahusika hao yatawasilishwa serikalini kwa hatua zaidi.


  Kwa ushirikiano maalumu, viongozi hao wanadaiwa kufanikisha meli za Iran kusajiliwa na kisha kupeperusha bendera ya Tanzania kwa lengo la kukwepa vikwazo vya kimataifa vilivyoweka kupitia Umoja wa Mataifa (UN).


  Vigogo hao wanadaiwa kufanikisha mpango wao kupitia kwa kampuni ya Philtex ya
  Dubai, inayodaiwa kusajili meli za mafuta za Iran ili kupeperusha bendera ya Tanzania kwa lengo la kukwepa vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa nchi ya Iran.


  Katika toleo lake namba 248, gazeti hili liliripoti kuwapo kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya maofisa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa zikibainisha kuwa, baadhi ya viongozi Zanzibar wamekuwa na maslahi katika masuala ya usajili wa meli hizo za kimataifa jijini Dubai.


  Katika habari hiyo kwenye gazeti hili, mwandishi wetu alinukuu moja ya chanzo chetu cha habari akisema; "Unajua kuna hali ya kuzidiana ujanja, awali huku Zanzibar walikataa SUMATRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Maji na Nchi Kavu) kufanya shughuli zake na wakaunda Wakala wa Meli Zanzibar (ZMA) lakini wakala huyu akatoa zabuni ya kusajili meli kwa kampuni iliyoko Dubai (Philtex),"

  "Baadhi ya viongozi hapa Zanzibar hawakujua ujanja uliopangwa na wenzao, ujanja wa kuikataa SUMATRA Zanzibar na kuanzisha ZMA lakini pia ujanja wa kutoa zabuni kwa kampuni ya Philtex ya Dubai. Sasa hivi ndiyo wanashituka kwamba wapo wenzao wanaodaiwa kuhusishwa na kampuni hiyo," kilieleza chanzo chetu cha habari kutoka Serikali ya Zanzibar.

  Tulieleza katika habari hiyo kwamba, licha ya Zanzibar kuanzisha wakala wake lakini ada za kimataifa za usajili wa meli zimekuwa zikilipwa na SUMATRA kwenda International Maritime Organisation (IMO) bila kuzingatia ukweli kwamba, Zanzibar pia imekuwa ikisajili meli kwa kutoza ada na kwa hiyo, ilipaswa ama kuchangia malipo ya ada ya kimataifa kwa SUMATRA au kulipa moja kwa moja kupitia utaratibu ambao ungekubaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Tayari taarifa za Serikali ya Zanzibar zinathibitisha kwamba ZMA imesajili meli 399, ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, meli za mizigo ya jumla na zile za abiria.


  Lakini wakati usajili wa meli hizo za kimataifa Visiwani humo ukiwa wa kasi kubwa kiasi hicho, taarifa za SUMATRA zinaonyesha kuwa mamlaka hiyo hadi sasa imesajili meli zisizozidi 100 tu tangu kuanzishwa kwake. Inaelezwa kuwa, sababu za meli chache kusajiliwa na SUMATRA kunatokana na udhibiti mkali.


  Kutokana na tofauti hizo za idadi ya meli zinazosajiliwa, baadhi ya viongozi waandamizi katika Serikali ya Muungano wanabainisha kuwa ni udhibiti huo ndio uliosababisha baadhi ya viongozi visiwani humo kuhakikisha SUMATRA inasimamisha shughuli zake visiwani, nao kuanzisha ZMA.


  Katika habari hiyo tulikariri Gazeti la Lebanon la "The Daily Star" ambalo limefichua mbinu inayotumiwa na Iran kwa kuzipa meli zake nyingi za mafuta majina mapya ya Kiingereza, kama inavyotuhumiwa kufanyika katika sakata la sasa linaloihusisha Tanzania.


  Kwa mujibu wa habari hiyo mifano ya meli ambazo zimebadilishwa majina ni pamoja na Freedom ambayo awali ilifahamika kama Haraz, Truth (awali iliitwa Nesa), Blossom ambayo awali iliitwa Sima. Theluthi moja ya meli za Iran hivi sasa zimesajiliwa nchi nyingine na kati ya nchi hizo ni Tanzania pamoja na Tuvalu.


  Meli hizo zilizosajiliwa nchi nyingine mbali na kubadilishwa majina lakini pia zimepewa namba za usajili kama ifuatavyo Blossom (IMO 9357353), Camellia (IMO 9171462) na Clove (IMO 9171450).


  Nyingine ni Companion (IMO 9357717), Courage (IMO 9357389), Daisy (IMO 9172038), Freedom (IMO 9357406), Justice (IMO 9357729), Lantana (IMO 9172040), Leadership (IMO 9356593), Magnolia (IMO 9172052) na Truth (IMO 9079107).


  Tovuti ya Umoja wa Mataifa inaweka bayana kuwa nchi ambazo zilikataa kufanya mchezo huo mchafu ni nchi za Brazil na Uturuki tu.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wow... Karume? Kazi ipo...
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  kamata mwizi meeeen
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  anawasaidia waarabu wenzake..blood is thicker than H2O
   
 5. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh, nasubiri mzee wa magogoni term yake itakapoisha sijui atakuwa associated na issue gani.
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ndio maana wanataka kutoka kwenye muungano!
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeah, na Unajua Mkwewe ni Muingereza... Msiria waliohamia Uingereza Muda Mrefuu sana... Kwahiyo wanaiangalia hiyo

  Familia kama wananunua majumba LONDON, Huyo Mama alikuwa ananunua Nguo UFARANSA kaisha pigwa chini;

  Akaanza kutumia Dada yake from London, send stuff to DUBAI then Damascus... Wakazima hiyo Connection; JASHO

  HAPO usicheze na CIA...
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakati Meli zetu zinazama na uchunguzi haufanyiki mnatafuta maswala mengine ambayo kwanza hayana athari kwa wananchi isipokuwa kuwaridhisha mabwana zetu nchi za magharibi..Sasa kama Karume ameiwezesha Meli ya Iran kubeba bendera yetu kuna kosa gani?. Ebu tupeni list ya meli zote zinazotumia bendera yetu na tuzichunguze. Ni mashirika mangapi ya nje yako registered Tanzania wakati wenye mali hizo sii Watanzania?.
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tz kiboko
   
 11. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  hii habari iwekwe kwenye jukwa la intelejensia
   
 12. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,195
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  huyo aliekuwa mbunge wa huko tabora na mjumbe wa halmashauri@kamat kuu ya chama alieshirikiana na huyo rais mstaafu atakua ndugu yetu mpendwa ROst TAMu..
   
 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mjomba issue hapa ni kwamba Iran ina vikwazo vya kibiashara, sasa kuzibebesha bendera ya Tanzania Meli zake ilikuwa ni njia ya kuwawezesha kukwepa vikwazo ambalo ni kosa la jinai. Mabwepande mawaka huu wanalo. Dhambi zote walizotutendea Watanzania sasa zinaanza kuwarudi.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kosa la jinai kasema nani?. Kosa ni kusajili meli au kosa ni kununua mafuta yaliyopigwa marufuku. Leo hii wewe uwe Mzanzibar umesajili Meli yako Dar na kufanya kazi baina ya dar na Zanzibar, halafu itokee kuna matatizo kati ya Bara na Zanzibar tukawekeana vikwazo, hivi kweli kosa litakuwa wewe Mzanzibar kusajili Meli Bara? na tuanaze kujiuliza kwa nini Mzanzibar amesajili Meli yake Bara na kutumia bendera ya bara?. Hee sheria ya kutosajili meli za wafanyabiashara wa kiiran imeanza lini kiasi kwamba walio kwisha sajili nao wawe hatiani?

  Mambo mengine jamani ujinga mtupu zuieni meli zisiende Zanzibar au Bara sio kutafuta wafanyabiashara wamesajili wapi meli zao hii ndio tunasema Mfuko Mkristu yaani mmeshikilia jambo kwa sababu mabeberu wenu wamesema hivyo. Kwa nini sisi tuchaguliwe marafiki na kuingizwa ktk vita yao na Wairan wakati haitusaidii kitu kabisa. Tunawauzia Marekani Uranium hivi Iran wakisema tuache mtakubali? maana wao ndio wanauza technologia na uraium za mabomu ya nuklia kwa nchi kama South Afrika, Israel, Pakistan na India..

  Kwa nini Marekani isiwawekee vikwazo China na India wanaonunua mzigo? Au kwa nini wasizishike hizo meli badala yake iwe nchi waliosajili kama mzigo haramu unakamata mzigo na meli sio chombo kiliposajiliwa.. Barricks wanatuibia dhahabu zetu hapa unakumbuka Waziri mkuu alitujibu nini? Kusajiri kwa Barrick nchini Canada hakuwapi mamlaka ya kuvunja mkataba wetu.
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Maneno mazito sana haya.
   
 16. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ni kweli kabisa mkuu...
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mwongozo wa spika!!!!!!
  Enhe! Mwongozo gani tena!
  Mh. Spika ule mk
  taja kifungu cha ngapi.
  Mh. Spika ni kile kifungu cha faida!!!
  Mh. Spika ule mkataba wa anga letu kutumiwa na wamarekani ulikwisha sainiwa au bado!!
  Na kama bad . . .
  Nasema kiti kitatoa ufafanuzi kwenye kamatsi.

  Mh. mukandara jibu kwa kifupi tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hivi Karume ana ndoto za kuja kuwa rais wa Muungano??upi sasa ambao wanautaka??asahau!mimi naona angestaafu tu akiwa kama alivyo asitake asiyoyaweza!!hilo la Meli kama kweli litamchafua vya kutosha na wenzake huko na huyo RA!
   
 19. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 930
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Iran ruksa endelea tu kutumia bendera yetu haina shida,aliyekuwekeeni vikwazo sio UN ILA ni nchi tu kama yenu,hata sisi havituhusu kwani sisi watanzania hatujagombana na nyinyi na wala hatujawahi,wanaopigia kelele wapuuzeni kisha wataacha,kwani wana chuki na uislam na nchi za kiislam kwa ujumla,wenyewe tumewazoea hata hawatupi shida kwani tumewazoea ni kama nyinyi mnavyopigwa mkwara na US na kisha mnawapuuza na kuwaambia wajaribu,wenyewe wamefyata mkia.Wanadhani eti nyinyi ni waarabu hawawajui kuwa ninyi waajemi.Halafu ikumbukwe nchi yetu haifungamani na nchi yoyote,mwenye faida kwetu ndiye rafiki yetu. Mbona wamerekani wako hapa nchini na hatuwapigii kelele?Wapeleke huko ushoga wao.
   
 20. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  kusajili meli nje ya nchi au kuisajili meli ya Iran si kosa ila hizi hatujazisajili bali tumebadili usajili wake wa awali toka Iran hadi Tanzania kwa nia ya kuzikwepesha vikwazo. Kama ni meli mpya sidhani kama ni tatizo lakini sio re-registration.
   
Loading...