Meli ya MV Mwanza yagonga jiwe ziwa Victoria, Mwanza

Meli ya MV Mwanza yagonga jiwe ziwa Victoria, Mwanza

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
578
Reaction score
1,396
Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha meli ya MV Victoria ikigonga jiwe katika Ziwa Victoria, jijini Mwanza.

Tukio hilo linadaiwa kutokea leo jijini Mwanza. Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha tukio hilo na madhara yaliyoweza kujitokeza bado hazijafahamika.
Meli ya MV Mwanza imegonga mwamba ndani ya Ziwa Victoria leo asubuhi, wakati wadau wa sekta ya uchukuzi walipokuwa wakifanya utalii wa ndani ya ziwa hilo kwa kutumia meli hiyo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano saa 4:30 asubuhi, huku taarifa za awali zikieleza kuwa meli hiyo ilikaribia kugongana na kivuko cha abiria kilichokuwa kikitokea Sengerema.

Akizungumzia tukio hilo, shahidi wa ajali hiyo, Bakari Mwigela amesema nahodha wa kivuko hicho alilazimika kurudi nyuma kwa kasi ili kuepusha mgongano wa moja kwa moja na MV Mwanza, lakini meli hiyo iliishia kugonga mwamba.

“Meli ilitaka kugonga kivuko cha abiria kilichokuwa kinatoka Sengerema. Aliyekuwa anaendesha hicho kivuko akarudi nyuma, ndiyo hiyo MV Mwanza ikagonga mwamba. Asingejiongeza kurudi nyuma kwa kasi, MV Mwanza ingegonga mawe mawili yakaanguka,” amesema Mwigela.

Wakati tukio hilo likitokea, wadau wa sekta ya uchukuzi walikuwa jijini Mwanza kuhudhuria Mkutano wa 19 wa Mapitio ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi, ambao ni sehemu ya tathmini ya maendeleo na changamoto katika sekta hiyo.

 
Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha meli ya MV Victoria ikigonga jiwe katika Ziwa Victoria, jijini Mwanza.

Tukio hilo linadaiwa kutokea leo jijini Mwanza. Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha tukio hilo na madhara yaliyoweza kujitokeza bado hazijafahamika.
Hapo hakuna madhara yanayoweza kuwa yamepoteza Maisha ya watanzania wenzetu.
 

Attachments

  • IMG-20250122-WA0047.jpg
    IMG-20250122-WA0047.jpg
    32.8 KB · Views: 23
  • HQgT1r8WEAAQizI.jpg
    HQgT1r8WEAAQizI.jpg
    88.9 KB · Views: 20
  • IMG-20260824-WA0073.jpg
    IMG-20260824-WA0073.jpg
    38.2 KB · Views: 20
  • 1000020485.jpg
    1000020485.jpg
    12.1 KB · Views: 21
Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha meli ya MV Victoria ikigonga jiwe katika Ziwa Victoria, jijini Mwanza.

Tukio hilo linadaiwa kutokea leo jijini Mwanza. Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha tukio hilo na madhara yaliyoweza kujitokeza bado hazijafahamika.
Ni MV Mwanza mkuu.
 
Back
Top Bottom