Melchizedek na utata unaomzunguka

Kama mkristo, hapa ndio hua naumiza kichwa. Watu kadhaa wenye elimu ya dini wameshindwa kunipa jibu sahihi nikaridhika..!
 
Kama mkristo, hapa ndio hua naumiza kichwa. Watu kadhaa wenye elimu ya dini wameshindwa kunipa jibu sahihi nikaridhika..!

Huna sababu ya kuogopa ndugu Baazigar, wapo wakiristo mamilioni duniani wasiomchukulia Yesu kuwa ni Mungu, Hawa ndiyo wapo kwenye haki, hawa ndiyo wapo kwenye ukweli katika suala hili, Hawa wanaitwa UNITARIAN CHURCH (Yaani Kanisa la Upekee wa Mungu), mfano mmojawapo wa waliowahi kuwa waumini wa Kanisa hili ni Sir Isaack Newton (Genius wa Physics), Hawa wamebase Theolojia yao kwenye Mafunzo ya Yesu mwenyewe na kauli za Yesu mwenyewe siyo kauli za Wanafalsafa wa kidini waliokuja baadae na kujifanya wanaconnect dots kumbe ndo kwanza wanakwenda mbali na kauli halisi za Yesu mwenyewe!

Nakushauri bwana Baazigar, mpe BABA haki yake maana yeye ndiye YEHOVA, hakuna kama Yeye, Yeye anatuma wala hatumwi. Yeye ndiye Mungu wa Kweli na wa Pekee

Na YESU mwana wa Maria mpe haki yake anayostahili maana yeye ni MWANA WA MTU , ni KRISTO wa nyumba ya Daudi, Ni NABII lakini siyo Mungu. Maana kama Hajui muda wala saa ya siku ya mwisho basi huyo siyo Mungu bali ni mtu
 
Kama nilivyojaribu kuelezea Mara moja pale juu.
Kwamba Yesu Kristo yupo mara moja na yote ni sahihi kwani si vema kulazimisha Dhana moja.

Kwanza Kuna Binadamu Yesu Kristo, Mtoto wa Yusufu, mtoto wa Yakobo Mtoto wa Matani, Mtoto wa Eleazari, mtoto wa Eliudi, Mtoto wa Akimu, mtoto wa Sadoki, Mtoto wa Azori hao ni vizazi vya Ibrahimu.
Yesu hiyo ni Mwisraeli na alijishighulisha na kazi za Fundi seremala na kuhubiri Imani ya watu wake,na mwishowe akafa ana akazikwa Kama Binadamu wengine.

Pili Yupo Yesu Kristo Masihi Mwana wa Mungu.
Huyo Hana Mwanzo Wala Mwisho, na alijiita kuwa ni Alfa na Omega.
Maandiko yote ya Imani Yana mtaja kuwa huyo Yesu yupo hazaliwi wala hafi.
Yanasema kuna kipindi alikuja duniani alihubiri Imani kwa watu wake na hatimaye alirudi Mbinguni kwa kupaa angani.
Alipokuwa dunia aliweza kufufua wafu, na kusamehe watu dhambi, mambo ambayo hayajawahi wala hayatawahi kufanywa na Binadamu.
Maandiko yanasema atarudi tena duniani kuja kuutawala ulimwengu.

Nabii Isaya anajaribu kumwelezea kidogo kwa kusema.
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume,
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake, Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.

Sasa hapa naona wengine wanajaribu kumwelezea Yesu wa kwanza kwa usahihi kabisa na wengine wanamweleza Yesu wa pili kwa ufasaha kabisa.
Na wengine wanamweleza Yesu kwa kutomjua Yesu katika dhana zote mbili.
 
Hawa wanatumia bible tofauti na zilizo sambaa kitaa?.
 
umejibu vizuri sana mkuu
 
Kwamba Yesu ana relation na melkisedeki au....?
Maana hapo naona neno KWA MFANO wa melkisedeki...
Issue naona ni sifa alizopewa zinafanana na Yesu mf; Mfalme wa amani....

Otherwise ungetusaidia je Melkizedeki ni nani hasa hadi aishi milele, sijui hakua na baba wala mama.

Who was this mysterious figure?
 
Ivi kwa nini lakini hawa waandishi walitumia lugha ya mafumboo..!!??
Vichwa panzi hapa unatoka kapaaa...!!

But why?...Whyyy??
Mambo yapo Hadharani hakuna kilichofumbwa ila ukiingiza imani kuyachambua yanakuwa na utata kulingana na unachoamini.
 
icho kitabu cha ENOCK kinapatikana wapi..kama unayoPDF Send me @johnsamwelelias@gmail.com
 
Safi Sana!

Kristulojia inakujakuwa maarifa muafaka humu JF...

Inaweza kuwa mapana ya somo na visomo bora kuliko yote humu JF.

Humu nimeona mengi na nimeona wengi ambao uwezo wao kuja kufanyika 'Walawi' wa siku za leo ni mkubwa.

Tutamulika kuhusu hili la Melkizedeki, Mungu Aliye Juu Kabisa, Miungu, Malaika, Uumbaji, na Viumbe watu --mahala fulani muafaka katika uzi wa 'Kusafiri Kiwakati 101...'

Kwa kuwa haya yote ya Melkizedeki ni mfano wa mengi yaliyo ni mafundisho yalivunjikavunjika katika biblia kuhusiana na Roho, nafsi na mwili...

Haleluya!
 
Labda sijaelewa ndugu! Biblia inasema, Ebrania 7:2-3, kuwa TAFSIRI YA JINA LAKE! Siyo kwamba hakuwa na baba wala mama....ila ni TAFSIRI ya jina lake!
 
habari ndugu,

japo nimechelewa kusoma uzi huu naomba nikujibu kwa ninavoelewa. kabla sijaandika chochote naomba niwie radhi kama maelezo nitayoyaandika yalishatolea na mdau mwingine maana ndio niko page ya pili kati ya nyingi za hii page. huenda ushajibiwa.

muandishi wa waebrania ni nani na kwa nini hajulikani?

kama unavyojua waebrania/ hebrews ndio waisraeli wenyewe waliyemsulubisha Yesu. Hiyo ilikuwa clear sign kuwa hawamtaki hata kidogo na wanafunzi wake wengi walikua prosecuted. Imagine wewe ni mwebrania, je ungesign your name kwenye manuscript ambayo walengwa wanaweza kukupiga mawe mpaka ufe? exactly...

kumbuka hata kwenye bible Yesu alikuwa na wanafunzi wengi wa siri ikiwemo baadhi ya mafarisayo na kuhani kama kina nikodemo kama sijakosea. yeyote anaweza kuandika hiki kitabu.

Muandishi mwingine anayesadikika kuandika ni paul. kama unaijua historia ya huyu mwamba ni obvious asingeweza kuandika jina lake. Paulo alikuwa jasiri hakuogopa kuuawa ila wayahudi hawakumkubali hata kidogo. walimuona farisayo aliyeasi, kumbuka alijiita farisayo wa mafarisayo, myahudi wa wayahudi myahudi kweli. hii betrayal ingefanya kitabu kisiwe credible kwa wengi. Wengi walimjua kama muderer na some of them walimuexperiance kwa udhalimu mkubwa aliofanya hapo awali.

mwandishi mwingine inasemekana alikuwa ni mwanamke. kitabu kilichoandikwa na wanawake kisingebeba uzito mkubwa. Hata vile vya agano la kale kina ester havikuandikwa na wanawake ila na waandishi ambao walipenda historia za wanawake hawa zisipotee.


kuhusu kitabu chenyewe. ebwana ni kitabu kitamu sana jamaa yangu ukikisoma utaona mambo makuu sana ya Mungu yalioandikwa kwa undani kidogo kwani waliandikiwa kitabu hicho walikuwa wataalamu wa agano la kale. huandiki tu kizembe zembe ndio maana kulikuwa na references nyingi sana za matukio agano la zaman na jipya.

food for thought:

1) je wajua kuwa waebrania ndio kitabu pekee kilichoandikwa kwa ajili ya watu ambao tayari wanaijua agano la kale? vingine vyote vilikuwa ni kwa gentiles, na gentiles hawakuwa expected kuwa wamesoma torati na manabii. in other words unaweza kumuamini Yesu na kwenda mbinguni bila torati. just faith.

2) inasemekana kabla ya umri wa miaka saba watoto wakiebrania wote walikuwa wameshakariri torati yote.

3) makuhani wa agano la kale walikariri vitabu vyote vya sheria na manabii.

ahsante.
 
Mzee context ndio kila kitu.

ukisoma biblia angalia imeandikwa na nani, wakati gani na kwa nani?

Yesu ni mwana wa Mungu kweli, Mungu ni baba yake kweli kabisa. Ila context inasemaje? Je Mungu ni baba yake Yesu kama ilivyo wewe na baba yako wa duniani? Unajua wenzetu wa upande wa pili wanakwama wapi? wanachukulia mahusiano haya yakireproduction ambayo siyo kweli.

unapoambiwa Melkizedeck hakuwa na mama wala baba anamaanisha kwa jinsi ya kibinadamu. Sperm haikufertilize egg ili yeye apatikane.

unajua kwa nini wayahudi walimsulibsha Yesu? kwa sababu alijiita yeye ni mwana wa Mungu, kwa jinsi hiyo hiyo unayowaza wewe. kwao hawakuona kuwa Mungu anaweza kuwa na mtoto.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…