Meja jenerali wa Israel: Nguvu ya Iran imeongezeka tunahofu sana

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Meja Jenerali Mzayuni: Nguvu ya Iran dhidi ya Israel imeongezeka mara mia kadhaa; tunahofia jibu la Iran

Apr 20, 2023 04:04 UTC

[https://media]

Meja Jenerali katika jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa Tel Aviv haina uwezo wa kukabiliana kijeshi na miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani na kusema: Nguvu ya Iran dhidi ya utawala wa Israel imeongezeka mara mia kadhaa. Amesema, hujuma yoyote dhidi ya Iran itapelekea kuangamizwa kikamilifu utawala huo.

Yitzhak Brick Meja Jenerali katika kikosi cha akiba ndani ya jeshi la utawala wa Kizayuni amefichua utambulisho halisi na wa kupenda vita wa utawala huo katika eneo la Magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa: Mwaka 2009 Tel Aviv iliamua kutekeleza hujuma ya kijeshi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran na kwa ajili hiyo ilikadiria kiasi cha fedha cha karibu dola bilioni nne katika uwanja huo.

[https://media]Miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani

Meja Jenerali Brick ameashiria pia kushindwa utawala wa Kizayuni kutekeleza hujuma hiyo ya kijeshi kwa kuhofia taathira zake na kueleza kuwa, pamoja na hayo, shambulizi hilo halikutekelezwa, na sababu yake ni kwamba, makamanda wa jeshi walikubaliana kuwa shambulio hilo kama litafaulu, linaweza kuvuruga mpango wa nyuklia wa Iran kwa kipindi cha kwa uchache cha miezi kadhaa tu; na katika upande mwingine, pigo ambalo Iran litaisababishia Israel litasababisha maafa na hasara kubwa kwa utawala huo.

Meja Jenerali huyo wa kikosi cha akiba katika jeshi la Israel amekiri pia kwamba tishio la Iran dhidi ya Israel leo hii ni la hatari zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma na kwamba uwezo wa makombora wa Iran ni mkubwa kiasi kwamba nchi hiyo ina uwezo wa kutekeleza mashambulizi ya kistratejia dhidi ya Israel. "Makombora hayo yanaweza kusababisha hasara na maafa makubwa kwa miundombinu na taasisi muhimu za Israel na kuturejesha miaka nyuma," amesema Meja Jenerali Brick wa kikosi cha akiba katika jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

View attachment 2594626
4c3k776f102ab529uts_800C450.jpg
 
View attachment 2594626View attachment 2594627
SI WANA IRON DOME sasa wanaogopa nini? 🤣🤣
 
Iran hana tofauti na mswahili labda rangi tu. Maneno mengi hamna lolote, walisema wataifuta Israel kwenye ramani ya dunia lakini wapi.
 
Yaani nilitegemea wavaa kobaz wajaze comments zao humu za kumshukuru huyo sijui jenerali kwa kuwapa matumaini.
 
Hawakusema mpaka wachokozwe, walisema ni taifa haramu hivyo wangeifutilia mbali lakini kumbe yalikuwa ni maneno tu ya kwenye khanga.
Weka ushahidi msiwalishe maneno.
Lile ni taifa la Kiislamu linafuata Sheria za Kiislamu. Sheria moja wapo ni hiyo ya kukatazwa kupigana bila kuchokozwa.
Sheria inakataza kuchokoza lakini inaruhusu kujihami.
 
Sasa mbona wanafadhili magaidi?
 
Mental slavery
Keep calm wait and see...Saddam Hussein naye alikuwa hivyo hivyo majamaa yaliruka na ndege kutoka Israel kwenda kupiga nuclear plant Iraq na kurudi salama nyumbani bila bugdha yoyote.

Hao sio watu wa kawaida, wanaitwa wazee wa six days war.
 
Back
Top Bottom