Meja Jenerali Kingu atinga TAKUKURU kuhojiwa

Meja Jenerali Kingu atinga TAKUKURU kuhojiwa

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Meja Jenerali Jacob Kingu ameshawasili Ofisi za Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma kwa mahojiano.

Kingu amefika Takukuru leo Ijumaa Januari 31, 2020 akiwa ametanguliwa kwa saa 1.21 na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola.
Hata hivyo, tofauti na Lugola alivyoingia leo Ijumaa saa 1.24 asubuhi, Kingu ambaye ni balozi mteule ameingia moja kwa moja na gari ndani ya uzio wa jengo la Takukuru na hata aliposhuka, gari hilo lenye namba za serikali liliegeshwa ndani kumsubiri.

Kingu alikuwa na simu moja mkononi mwake lakini msaidizi wake alikuwa na begi jeusi na waliingia wote ndani kisha msaidizi akatoka akiwa hana begi hilo ishara kuwa lilikuwa la kiongozi huyo.

Alivalia shati la batiki lenye ramani na maandishi ya Afrika na licha ya kuwa na dereva, lakini alikuwa na msaidizi ambaye alivalia suti nyeusi ya mikono mirefu aliyetangulia kushuka kisha akamfungulia mlango.

Wakati wote gari la kiongozi huyo lilibaki katika muungurumo bila kuzimwa huku dereva na msaidizi wake wakiwa ndani ya gari.

Balozi huyo aliingia ndani ya jengo la Takukuru wakati Lugola akiwa hajatoka ndani huku maofisa wa taasisi hiyo wakiwa ni wengi katika geti la kuingilia.
Takukuru inawahoji Lugola, Kingu na wengine baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutengua nyadhifa zao Januari 23, 2020 kwa kile alichodai kuhusika na mkataba wa zaidi ya Sh1 trilioni.

Wengine watakaohojiwa ni aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, Naibu waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo, Ramadhan Kailima, watumishi wa jeshi hilo, wizara ya mambo ya ndani pamoja na kampuni ya Romani iliyoingia mkataba na jeshi hilo wa kununua vifaa za zima moto.

CHANZO: Mwananchi
 
Huyo Kingu ni mwaminifu sana pia bila shaka ni undercover agent, ameenda pale na data za kwafungulia mashataka hao maninja, na huyo amepewa ubalozi akapumzike kwa muda na ajiandae kuwa Mkuu wa majeshi baada ya Mabeyo kustaafu, yupo vizuri sana, ni mtanzania wa Singida aiyependa mambo ya deals za wizi.,
Huyo jenerali hajaitwa kuhojiwa amepeleka ushahidi wa kumning'iniza ninja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingu Ni meja jenerali,lazima heshima yake itunzwe Sana.
Siku hizi ma Meja General wa kawaida sana

Enzi zile ukiskia Meja General Muhidin Kimario lazima usikie Matukio ya Kijasiri jasiri aliyofanya SIJUI Israel,sijui Uganda sijui Mozambique,

Siku hizi ukiulizia sifa Special za Maluten General na Ma Major General utaskia 'Mwaminifu sana na Muadilifu'

Akina Hashim Mbita ukiulizia habari zao utaskia Umafia waliofanya Shelisheli kuzima Mapinduzi ya Kijeshi na kumrudisha Kibabe Rais madarakan na kuteka kundi zima la Wana Mapinduzi

Jwtz ilikuwa Jwtz kweli kweli
Sent using Jamii Forums mobile app
 
pic+kingu.jpg

cc: Wazeee wa weka picha
 
Back
Top Bottom