Meir Dagan na ujasusi wa Mossad dhidi ya Iran kumiliki silaha za nyuklia

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Wageni wenye ruhusa tu na wafanyakazi wanafika katika ghorofa ya tatu ndani ya Makao makuu ya shirika la kijasusi la Mossad ndani ya eneo lenye ulinzi mkali sana katika makutano ya barabara kuu kaskazini mwa mji wa Tel Aviv herufi nne za kiyunani katika ukuta zinasomeka Ramsad ikiwa ni kifupi cha maneno Rosh ha-Mossad(Mkuu wa Mossad), ofisi ya Meir Dagan aliyeshika wadhifa huo kwa miaka 8 (2002-2010).

Dagan kipaumbele chake namba moja ilikuwa ni kuidhibiti Iran ili kuhakikisha haimiliki silaha za nyuklia. Dhamira ya ya Iran kumiliki silaha za nyuklia iliongezeka mara dufu baada ya kuinuka kwa utawala wa viongozi wa kishia wa kina Ayatollah miaka ya tisini, waliposhika madaraka baada ya kumpindua kiongozi wa Iran Shah Mohd Pahlavi,ambaye kwa miaka mingi alikuwa kipenzi cha Marekani, Israel na mataifa ya magharibi kwa ujumla.

Moja ya jitihada za bwana Dagan ilikuwa kutumia nchi nyingine ya tatu kuifikishia Iran ujumbe wa kuionya na kuitaka iachane na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia, onyo liliambatanishwa na vitisho vya hatua kali kama hawatafanya hivyo. Hatua nyingine ilikuwa ni kuwashawishi washirika wa kibiashara wa Iran (hasa mataifa ya ulaya) katika kumuwezesha kurutubisha nyuklia kuwa waache kushirikiana nayo na ikiwezekana wamuwekee vikwazo vya kibiashara. Bwana Dagan alifanya kazi kubwa kuzishawishi nchi za ulaya kuwa kuiruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia ilikuwa ni hatari pia kwa usalama wa mataifa yao na dunia kwa ujumla.

Israel iliamini kuwa vikwazo vya uingizaji bidhaa muhimu, miamala ya pesa na zuio la kusafiri kungewafanya raia wa Iran wapate shida na adha kubwa ya kimaishi na hali hiyo ingepelekea mgogoro na kutoelewana kati ya serikali ya Iran na raia wake. Hali hiyo ingepelekea kuzuka kwa vurugu za ndani ya nchi ili kuifanya Iran kutumia mda mwingi kushughulika na matatizo ya ndani na kupunguza nguvu na jitihada za kujiendeleza kinyuklia.

Dagan pia akaamuru shughuli za ujasusi zikihusisha kuwarubuni na kuwageuza upande wao watu walio katika nyadhifa za juu za utawala serikalini na taasisi zake nyeti,watu waliokuwa katika mradi wa nyuklia, kuhujumu mradi wa nyukilia na mwisho kuuwa watu mashuhuri ndani ya mradi huo. Kwa uchambuzi wake bwana Dagan aliona hatua hizi zitaifanya
Iran kubadili mawazo yake na kuachana na ndoto za kumiliki silaha za nyuklia. Aliona pis ni lazima viongozi wakubwa wa Iran washawishiwe sio tu kwa maneno na vitendo kwamba kuhangaikia kumiliki silaha za nyuklia kungewatokea puani na kung'olewa kwa utawala wao.


KUISHAWISHI IAEA,WAKUTANA NA CHANGAMOTO

Moja ya changamoto kubwa kwa Dagan ilikuwa ni kuyashawishi mashirika ya kijasusi ya nchi zingine kuwa Iran ilikuwa ikiendea mbio hatua za umiliki silaha za nyuklia. Kwake hii ilikuwa kazi ngumu kwani uchambuzi wa mataifa mengi ulionesha kuwa iran haikuwa karibu kabisa kumiliki silaha za nyuklia.


Lakini Dagan na Mossad kwa ujumla walikuwa na mshirika mmoja wa kufa na kupona waliyekuwa wakizungumza lugha moja,shirika la kijausi la marekani CIA. Dagan aliiva na wakurugenzi wakuu wa wanne wa CIA katika miaka yake nane ya ukuu wa mossad. Mossad pia kama shirika waliiva vizuri na mashirika mengine makubwa ya kijasusi ya MI6 ya Uingereza, BND ya Ujerumani na DGSE ya Ufaransa.

Ushirikiano wa mashirika haya na mengine ya mataifa mbalimbali yalisaidia kuingiliwa na kukamatwa kwa mtandao wa manunuzi wa virutibisho vya silaha za nyuklia wa Iran kupitia meli zilizokamatwa nchini Tanzania,Italy,Belgium,Spain,Ukraine,Azerbaijan na Turkmenistan na kuwawezesha Israel kulipatia taarifa muhimu shirika la kimataifa la nguvu ya atomiki chini ya U.N (IAEA) na hatimae likaanza kufanya ufatiliaji wa mwenendo wa programu ya nyuklia wa Iran (ambao wao walidai ni kwa ajili tu ya tafiti na uzalishaji nishati).

Uchunguzi uliofanywa na IAEA chini ya mkurugenzi Mohamed EL Baradei ulionesha hakukuwa na dalili zinazoonesha Iran inatengeneza silaha za nyuklia. Hatua hii ikawaudhi Israel wakaona mkurugenzi huyo ni kikwazo katika harakati zao. El baradei machale yalimcheza kuwa shirika lake linataka kutumika vibaya kwa maslahi ya mataifa ya magharibi na alikinzana na presha iliyokuwa ikielekezwa kwake kuwa ainyooshee kidole na kuituhumu iran bila ushahidi mzito. Kuwepo kwa watumishi wairan 20 katika shirika hilo kuliwafanya Israel iamini kuwa shirika limeingiliwa hivyo iliwabidi kufanya kitu kukabili vikwazo hivyo.


KUMTENGENEZEA SKENDO MKURUGENZI IAEA NA KUPIKA USHAIDI DHIDI YA IRAN

Mossad wakaandaa mpango kabambe wa kupika taarifa ili kuonesha kuwa El baradei alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Iran. Taarifa hiyo wakampatia bwana Omar Suleiman aliyekuwa mkuu wa usalama Misri chini ya Hosni Mubarak. El baradei alikuwa mpinzani na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Hosni Mubaarak ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa Israel na hakuwa mwenye kuipenda iran pia hivyo Mubaarak alitoa ushirikiano wa hali ya juu dhidi Iran.

Baada ya kuona hakuna mafanikio katika operesheni hiyo,Mossad wakafikiria namna nyingine ya kumdhalilisha mkuu huyo wa shirika la nguvu ya atomiki duniani ili ipelekee kujiuzulu kwake. Moja ya mipango hiyo ilikuwa kuingilia akaunti yake ya benki na kuweka kiasi kikubwa cha pesa ambacho kingeshangaza na angeshindwa kuelezea amezipata vipi huku idara ya kimapambano ya mambo ya kisaikolojia ikisambaza uvumi kwa waandishi wa habari kuwa El baradei alikuwa akipokea rushwa na kutumika na serikali ya Iran. Mwisho wa siku yote hayo hayakutokea na kinyume chake El baradei akaokea tuzo ya Nobel mwaka 2005 kwa utendaji kazi mzuri. Tuzo hiyo hasa ilitokana na yeye kuiwekea ngumu Iran baada ya kuridhishwa na taarifa mbalimbali kutoka mashirika mengi ya kijasusi ya mataifa ya magharibi zilizoonesha Iran ilikuwa ikirutubisha uranium kwa kiasi kikubwa kuliko kile kinachotakiwa kwa ajili ya uzalishaji nishati na masuala ya utafiti,hivyo ilikuwa ikikiuka makubaliano ya kutozalisha silaha za nyuklia.

Ushahidi mkubwa ilikuwa kukamatwa kwa laptop iliyokuwa na video iliyoonesha mipango ya siri ya utengezaji wa silaha za nyuklia kuanzia michoro,mahesabu na vitendea kazi. Video hiyo iliyokuwa katika lugha ya kifursi ilikuwa ikimilikiwa raia wa Iran na ilikamtwa na Mossad na kupelekwa kwa kwa mashirika rafiki ya kijasusi ya nchi za magharibi na shirika la nguvu la atomic duniani IAEA. Lakini kulikuwa na tetesi miongoni mwa baaadhi ya mashirika rafiki ya kijasusi kuwa video ile ilikuwa imetengenezwa na Mossad wenyewe. Kukamatwa kwa ushahidi huo, kuliwafanya mataifa ya magharibi kuyashawishi mataifa mengine kupitisha la azimio la Umoja wa Mataifa kuituhumu iran kuvunja makubaliano na hitimisho rasmi la shirika la atomiki ni kwamba Iran imekataa kutii makubaliano ya kuacha urutubishaji wa uranium. Ripoti hiyo ikapelekwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2005 na miaka mitano baadae Iran inawekewa vikwazo kwa mara ya kwanza.

Isreal na Marekani wakafanya upembuzi na kuona vikwazo vikubwa zaidi vilihitajika ili kuleta athari zaidi kwa serikali na wananchi wa Iran. walidhamiria kuzuia uuzaji wa mafuta ya Iran lakini ilikuwa ngumu kwani China na Urusi walikataa kwa kuwa ni washirika wakubwa wa kibishara na Iran hasa mafuta na masuala ya nishati.


HUJUMA DHIDI YA MITAMBO YA NYUKLIA

Mwaka 2003 CIA na Mossad waliafikiana kufanya operesheni ya pamoja kuiharibu huduma ya undeshaji mitambo katika kituo muhimu cha nyuklia Iran. Mipango ikawekwa kuweka mabomu kwenye minara ya umeme unaolekea kituoni hapo lakini jambo hilo lilishindikana. CIA wakatoa wazo la kumtumia kwa kumshawishi bila kujua anashawishiwa na nani mtaalamu mwanafunzi mwenye asili ya kirusi akajitolee elimu na ujuzi wake katika kituo hicho lakini CIA walifanya kosa kwa kubadilisha nyaraka za mipango ya mwanafuzni huyo ya utengezaji wa silaha bila kumwambia kuwa wamefanya hiyo. Lengo lilikuwa kuharibu taarifa ili mipangilio mizima ya mitambo iharibike na kuleta athari na uharibu mkubwa lakini bahati mbaya mrusi yule baada kufika Iran na kuona nyaraka zake haziko sawa akawapa taarifa kuwa kuna kitu kimefanywa kwenye nyaraka zake na hivyo mpango huo ukafa.

Safari hii wakiongezeka MI6 wa Uingereza ,wakaamua kutengeza makampuni ambayo yaliweza kutengeza uhusiano wa karibu na mtandao wa manunuzi wa Iran. Ili kujijengea uaminifu walianza kuiuzia iran vifaa bora na halisi kabisa kwa bei nzuri lakini baada ya muda walipenyeza vifaa vibovu vyenye kuleta athari kubwa kwenye mitambo ya nyuklia. Matokea ya hujuma yakaanza kuonekana, Iran ikajikuta inashindwa kuthibiti vifaa iliyonunua kutoka nje na kutokea uharibifu mkubwa.

Kilele cha mfanikio ya hujuma ilikuwa ni mpango wa kabambe kutengezwa computer virus aliyejulikanakwa jina la stuxnet.

Stuxnet ilikuwa operesheni ya pamoja ya CIA,Mossad, kitengo cha teknolojia chini idara ya ujasusi ya jeshi la Israel Amaan. Software hiyo ilitengenezwa ili kuharibu mfumo wa computer katika kituo cha urutubishaji nyuklia huko Natanz,Iran. Operesheni hii pia iliwezeshwa na shirikila la kijasusi la Ujerumani BND ambalo lilikuwa rafiki sana kwa Israel ikiwa ni sehemu ya kufuta kumbukumbu mbaya za mauaji za wayahudi katika utawalawa Hitler. BND ilisaidia kuishinikiza kampuni ya vifaa vya kielectronik ya SIEMENS ambayo ndiyo iliyoiuzia Iran mifumo ya computer ya kuendeshea mitambo ya nyuklia. Wataaamu wa Siemens walitoa ushirikiano ila kupata mwanya kuwezesha kuingiliwa mifumo ya computer katika kituo cha urutubishaji nyuklia Iran.

Israel kwa miaka miwili kupitia maabara maalum inayomilikiwa na Marekani wakawa wanafatilia kirusi hicho jinsi kinavyoweza kuleta madhara na kwa kiasi gani.

Kirusi hiko kilifanikiwa kuingizwa katika mfumo wa computer huko Natanz mwaka 2009 na kiliweza kukaa kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kugunduliwa na majasusi wairan. Mpaka mda huo kirusi kilikuwa kikipeleka taarifa za kuchanganya kwenye vinu vya uzalishaji nyuklia na kuathiri mfumo mzima na kupeleka kuharibika kwa vinu 1000 kati ya 5000, majasusi wa Iran na wataalamu wao wa mifumo ya computer walishikwa butwaa kwani system haikuonesha hitilafu yeyote.


KUUAWA WANAYASANSI NA WATAALAMU WA NYUKLIA

Kama vile haitoshi,Iran ilipata pigo kubwa zaidi,kati ya mwaka 2007 na 2011 wanasayansi wakubwa watano wa Iran waliuawa. Mmoja aliuawa kwa sumu ya hewa ya carbonmonoxide kutoka kwenye heater nyumbani kwake na wengine wannne waliuawa kwa mabomu.

Kati ya mauaji manne ya mabomu, matatu yalikuwa mabomu ya sumaku(magnetic bombs). Haya yalikuwa madogo lakini yenye nguvu sana, ambayo mlipuko au nishati yenyewe madhara huekekezwa upande mmoja( tofauti na mengine mlipuko huelekea pande zote) linaporushwa na kunasa kwenye gari sehemu ya mlango alipo mlengwa. Mashambulizi haya ya mabomu hutekelezwa na washambuliaji waliokuwa makini waliotumia pikipiki inayokwenda kwa mwendo kasi mkubwa, mtindo maarufu sana wa kikosi cha mauaji cha Mossad kinachojulikana kama KIDON.

Ni mwanasayansi mmoja tu aliyepona shambulio la bomu la sumaku,ambaye angekuwa mwanasayansi wa 6 mkubwa kuuawa. Mwanasayansi huyo kwa jina Fereydoon Abbas-Divani alifanikiwa kutokana na hisia zake na uzoefu alioupata kwani alikuwa mtu aliyepitia mafunzo na kuwa jasusi. Alipoteza mguu mmoja katika jaribio hilo lililoshindikana.

Mauaji haya ya mabomu yalikuwa yakifanyika asubuhi, walengwa wakiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zao. Mauaji haya ya wanasayasni yakawafanya wasayansi waalikwa kutoka nchi za China,Urusi na Pakistani kuogopa mialiko kwa ajili ya kutoa ujuzi wao.Ni wale kutoka Korea Kaskazini tu ndio waliedelea kujihusisha kwa wingi.

Pia kulitokea shambuli lingine la mlipuko mkubwa iliyoathiri kambi ya kijeshi ya kujaribia silaha za masafa marefu karibu na mji mkuu wa Tehran mwaka 2011. Watu wengi waliuawa katika mlipuko huo akiwemo jenerali wa kikundi cha kijeshi chenye mafunzo ya hali ya juu cha Revolutionary Guard ambaye alikuwa akisimamia utengezaji wa mabomu ya masafa marefu katika kambi hiyo.

Pamoja na mauaji haya ya wanasayansi, hakukuwahi kutokea kudai kwa wazi uhusika wa Mossad au Isreal kwa ujumla. Marekani na mataifa ya magahribi yalikataa kuhusika na mashambulizi hayo na Marekani ikaenda mbali zaidi kulaani mauaji hayo na kushutumu wauaji wanaharibu juhudi za kidiplomasia na mazungumzo kuhusu usitishaji wa umiliki wa silaha za nyuklia yaliyokuwa yakienda vibaya kila baada ya shambulizi.


MPANGO KUFADHILI MAKUNDI YA KIGAIDI NA KUPANGA VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE

Dagan aliweza pia kuwatumia makundi ya jamii zilizokuwa zikipingana na utawala wa Iran. Jamii hizo za kikursi,wabaluchi ,waturkmen,waarabu na waazeri yamekuwa yakilalamika kutengwa na kubaguliwa na utawala wa Iran katika fursa mbalimbali kutokana na utaofauti wa asili,dini na tamaduni. Pia Dagan alishauri kutoa sapoti kwa wanaharakati wa kudai demokrasia nchini Iran ikiwa watahitajika kuleta machafuko. Pia alikuwa na uhakika kwa kushirikiana na Marekani wanaweza kubadili utawala wa Iran.

Aliona kukosekana kwa ajira miongoni mwa makundi hayo ya jamii za watu wachache ilikuwa ni fursa kwa Mossad kupata majasusi,wapiganaji na hata kutengeneza makundi ya waasi na kigaidi.

Miaka iliyofuata dalili zilionesha kuwa makundi ya kigaidi nchini Iran ya Mujahideen e-Khlaq(MEK), Kundi la kisunni la Jundallah (soldiers of god) yalikuwa yakifadhiliwa na kutumiwa na majasusi wa Isreal. Isreal ikitaka kusambaza taarifa za kipropaganda kuhusu utawalawa Iran kwenye vyombo vya habari huko Iran iliyatumia makundi hayo kusambaza taarifa.

Pia majasusi wa Mossad waliweza kuingia na kutoka Iran kwa urahisi zaidi, hasa kupitia mpaka na nchi ambazo vyombo vyake vya ulinzi vilikuwa na ushirikiano na Israel ikiwemo sehemu ya wakurdi inayojatawala kaskazini mwaka Iraq. Isreal ilikuwa imejitengenzea ukaribu na viongozi wa kikurdi katika nchi nyingi, wakurdi wakishukuru kwa msaada wa Israel dhidi ya manyanyaso ya waarabu. Kuna msemo unasema Adui wa adui yako ni rafiki yako.

Mossad pia ilikuwa na hazina ya watu, kulikuwa maelfu ya wairan wanaishi isreal, wayahudi wairan hawa walikuwa na kila tamaduni za kifursi ikiwemo lugha. Hivyo ilikuwa rahisi kuwapata majasusi kisha wakaingizwa Iran na kuwa kama sehemu ya jamii ya wenyeji.


Mwaka 2007 wakati anazungumza na afisa mmoja wa Marekani,Dagan aliitaka Marekani kuungana na Isreal katika nguzo tano za kuwaangusha wakina Ayattollah(watawala wa Iran). Alimtajia nguzo hizo kuwa ni njia za kisiasa, mipango ya kijasusi, kuzuia umiliki wa silaha za nyuklia, vikwazo na mwisho kubadili utawala( ndio kilichobakia katika ya nguzo tano?).


MAREKANI NAYO INA MASLAHI NA MAFUTA YA IRAN


Dagan pia aliamini katika nguvu ya uchumi katika mapambano yake. Aliwaeleza maafisa wake wa Mossad kuwa Marekani imekuwa ikitengeza sera za kuwanufaisha kiuchumi na hata vita vyao mara mbili nchini Iraq ilikuwa ni kwa ajili ya faida za kiuchumi kupitia utajiri wa mafuta, hivyo Marekani nayo haiwezi kuruhusu Iran imiliki silaha za nyuklia kwa kuwa litakuwa taifa lenye nguvu kubwa miongoni mwa mataifa yanayozalisha mafuta mengi duniani (Kwanini Marekani haitaki taifa lenye mafuta hili liwe na nguvu?).

Huyo ndio Dagan, kipindi chake cha uongozi ndani ya Mossad kilishudia mauaji mengi kuwahi kutokea kwa maadui wa Isreal na kwa namna moja au nyingine alijisikia fahari kwa hilo. Kuhusu kuizuia Iran kwake suala la mauaji lilikuwa ni njia sahihi kabisa. Baada ya kustaafu alisikika akisema alifanikiwa kwa ufanisi mkubwa sana katika mikakati yake dhidi ya Iran.


Kufahamu zaidi pitia kitabu SPIES AGAINST ARMAGEDDON;Inside Israel's Secret Wars by Dan Raviv and Yossi Melman

The bold OLESAIDIMU Ndahani mossad007 de'levis MTAZAMO apakak C.T.U kabanga kadoda11 Nifah Gogo la choo busegwe idawa MSEZA MKULU Elungata kashengo Mchochezi Deception Kaa la Moto aloycious maalimu shewedy MALCOM LUMUMBA Bukyanagandi
 
Yah...Asante sana.... Km kuna vingine naomba unitumie mkuu.
Nimekutumia kingine kwa Email, ukichukua na kwenye huo uzi niliokuelekeza utakuwa na vitabu vitatu. Vyengine wadau watakuelekeza, ila kuna kimoja kizuri sana sijakipata bado kinaitwa DUET IN BEIRUT humo utawasoma KIDON, assassination unit ya Mossad inayoogopwa duniani
 
Back
Top Bottom