Mei mosi 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mei mosi 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Feb 19, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Ni udadisi tu.....
  Kwamba bado siku 60 tusherehekee sikukuu ya wafanyakazi hapo tarehe 1/5/2011.
  Najaribu kufikiria itakuwaje:
  1. Bado madai ya wafanyakazi hayajapatiwa ufumbuzi, na hakuna movement zozote zinazoashiria neema
  2.Raisi alishaapa kwamba hawataongeza mishahara hata miaka nane ijayo, je atatimiza ahadi yake
  3.Mwaka jana hakualikwa kwenye Mei mosi, je mwaka huu itakuwaje?
  4.Alishatishia juhudi zozote za kufanya maandamano akiwa na wapambe wake pembeni, Mkuu wa Majeshi, IGP, Mkuu wa intelligency...nk. kusisitiza kwamba watu wakigoma atawashughulikia vilivyo na wangine watarudi na manundu
  5.Alishawadanganya wafanyakzi kwamba amepandisha mishahara yao kima cha chini kuwa 260,000/- lakini hadi leo hakuna kitu kama hicho!
  6. Mwezi uliopita watu wamelipwa mishahara madirishani, eti kujaribu kubaini watumishi hewa, lakini wenye akili tukajua ni njia ya kuchukuwa cha juu (yaani posho au nyongeza ambazo watu hawajajua), maana ni rahisi kujichotea cash kuliko kuiba kwenye personal bank accounts
  7. Polisi wameshalizwa miezi miwili mfululizo, kwa kukatwa posho zao na wanalia na kusaga meno. Sijui moral zao za kazi zikoje hivi sasa?
  8. Je walimu wanaolaumiwa kwa kufelisha wanafunzi wanjisikiaje sasa hivi. Watasherehekea hii sikukukuu na ujumbe gani?
  9.Takwimu za wahitimu wa vyuo na takwimu ya ongezeko la ajira vina uwiano gani hivi sasa? Maana naona viwanda ndio kwanza vinafungwa, mashirika yanakufa ( rejea Reli, ATCL, Kiwira, Mgololo etc)
  10. Sioni juhudi zozote za maana za kuongeza ajira.....sasa hata kilimo kinachakachuliwa, nasikia pamba inahujumiwa kule Shinyanga na Tabora.
  11. Mfumuko wa bei? Naona hali ni mbaya mno. Watu wengi tu sasa hivi wamesahau ladha ya mkate ( kumbuka mkate mmoja ni Tzs 1000/- ule mdogo), wengi siku hizi wanasonga ugali asubuhi ili watoto wapate kifungua kinywa! Sukari bei haishikiki, sas watu ujio wa chumvi ni kitu cha kawaida....
  12.Juhudi za kuwaneemesha wabunge ndo ziko juu, wamegawiwa sasa 90M kila mbunge akanunue gari! I wapi kauli ya mtoto wa mkulima ya kudhibiti ununuzi wa magari ya kifahari?

  Hebu tutafakari na tumshauri Raisi wetu, kama anshaurika.....(maana nimeshakata tamaa)!
   
 2. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
   
Loading...