Medicins Sans Frontieres (MSF) ni nani?

Sep 10, 2013
76
21
Habari wakuu!

Naomba kujuzwa mwenye uelewa wowote kuhusu hawa jamaa wanaitwa Medicins Sans Frontieres (MSF).

Wameniita kwenye usahili na nimeona juzi waliita watu kama 100 hivi kwenye written test!
nini shughuli yao hapa tanzania? Ofisi zao zipo wapi? wanafanya nini tanzania?

Nawasilisha!
 
Uliombaje kazi kama hujui wanajishughulisha na nn?
Anyway ni shirika la watoa huduma za afya lisilo na mipaka kwenye majanga na wakimbizi kwenye kambi zao..
Alafu usiwe kilaza namna hiyo ndugu hebu Google web yao usome kwa maelezo zaidi
 
Hao ni madaktari wasio na mipaka, kazi zao nyingi wanashirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na Red Cross.
Mkuu wakikupa kazi jiandae kufanya kazi popote duniani tena kwa kuanzia wanaweza wakakupangia Syria
 
Ni Madaktari wasio na mipaka na asili yao ni huko France
 
Uliombaje kazi kama hujui wanajishughulisha na nn?
Anyway ni shirika la watoa huduma za afya lisilo na mipaka kwenye majanga na wakimbizi kwenye kambi zao..
Alafu usiwe kilaza namna hiyo ndugu hebu Google web yao usome kwa maelezo zaidi

Ahsante kwa taarifa! Ndugu yangu si unajua tena ukiwa desperate! Kila post unayoona inaendana na education yako unatupia tuu! wakishakuita kama hivi ndo unaanza ku-dig ni kina nani...
 
Hao ni madaktari wasio na mipaka, kazi zao nyingi wanashirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na Red Cross.
Mkuu wakikupa kazi jiandae kufanya kazi popote duniani tena kwa kuanzia wanaweza wakakupangia Syria
Duh! Kaka Syria tena? Kwani hapa tanzania wana ofisi wapi au wanahudumia wapi?
 
Yah tulikua tunatafuta watu wa Kufanya Kazi kwenye War Zone yaani Allepo-Syria, Juba-South Sudan, na Mogadishu Kila laheri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom