Medical report

Medical report

Crystal field theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
951
Reaction score
412
Wakuu habari.. naomba msaada wa hatua za kufuata ili nipate taarifa ya mgonjwa wangu pale muhimbili hospitali. Kiufupi nielekezwe kiujumla

#AHSANTENI SANAA
 
Ninachojua Taarifa za afya ni Siri baina ya mgonjwa na mtoa huduma, zinaweza kutolewa kwa mtu mwingine kukiwa na sababu maalumu...kama nakosea nipo tayari kurekebishwa
Yes it's confidential, inaweza kutolewa kwa third party kwa idhini ya mgonjwa au pale inapolazimu kwa ajili ya maslahi mapana ya mgonjwa hata kama mgonjwa hajaridhia.

So it depends na situation jinsi ilivyo.
 
Yes it's confidential, inaweza kutolewa kwa third party kwa idhini ya mgonjwa au pale inapolazimu kwa ajili ya maslahi mapana ya mgonjwa hata kama mgonjwa hajaridhia.

So it depends na situation jinsi ilivyo.
Ni maslahi ya taasisi na mgonjwa karidhia
 
Medical report ni siri ya family. Mgonjwa karidhia akiwa katika hali gani? Kumbuka kuna sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi kaisome kabla hamjatafuta hizo taarifa huyo huyo mgonjwa siku akipona anaweza kuwageuka mkamlipa mamilioni kwa ku compromise taarifa zake kwa utaratibu usiopaswa!!
 
Medical report ni confidential document, ni mali ya hospitali alipotibiwa mgonjwa.

Lakini itatolewa tu:-
1. Endapo mgonjwa ataihitaji ili kuiwasilisha mahala pake pa kazi.

2. Taasisi iliyomuajiri itahitaji taarifa ya mgonjwa ambaye ni mfanyakazi wao.

Kuhusu malipo endapo mgonjwa mwenyewe ataihitaji ni Tsh. 20,000
Na endapo Taasisi itahitaji ni Tsh. 100,000 /150,000 (Kama sijakosea).

Utaratibu wa kufuata:
1. Fika hosp. husika ulipokuwa unatibiwa, andika barua ya kuomba hiyo taarifa.
2. Utalipia kiasi cha fedha tajwa.
3. Utakuwa directed kwa daktari aliyekutibu.
4. Ukishakamilisha hatua hizo utapatiwa ripoti yako.
 
Back
Top Bottom