Japo ni kinyume na haki za binadamu lakin kwa baadhi ya kazi ni lazima wakufanyie check kama una vvu au hauna,,na kama hauna wanakuajili na kama hauna hawakuajili,,ila kama ukianza kazi hauna maambukizi ya vvu na unapoendelea na kazi huko siku za usoni wakikukuta umeathirika na vvu hawakufukuzi kazi utaendelea na kazi kama kawaida......
lililo muhimu watu tujilinde sana dhidi ya vvu hasa hasa vijana tunaoendelea kutafuta ajira ili iwe rahisi kupata ajira pia na urahisi wa kupata nafazi za kuendelea na masomo ukiwa kazini na hasa ufadhili wa nje ya nchi ofisi inaghalimika bila kipingamizi,,,,,japo hawasemi wazi kuwa wenye vvu hawapati ajira lakin katika hali halisi ni kwamba ukishaathirika nje ya ajira ni vigumu sana kupata ajira.
Pia maofisi mbalimbali wana utaratibu wa kuwafanyia wafanyakazi checkup ya vvu ili wajue ni wafanyakazi wangapi wameathirika au hawajaathirika ili wale walioathirika waanze kupatiwa huduma zinazotakiwa dhidi ya afya zao,, na hizo check wanafanya baada ya wafanyakazi kuelimishwa umuhimu wa kafanya checkup kwa hiyo mara nyingi kunakuwa na makubaliano kati yao ya kuendelea na zoezi hilo.