Media zetu na Uandishi wa Umbeya badala ya Habari

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
Watalaam wa uandishi wa habari wanakubaliana na aina tatu kuu wa vyombo vya Habari, ambazo ni Printing Media, Electronic Media na wireless Media, kwa lugha raisi kuna Magazeti, Majarida, Machapisho nk haya uitwa printing Media, halafu kuna radio, TV, video nk haya yako electronic media na mwisho ni wireless Media ambao kiukweli ndiyo siku hizi tunayaita social Networks Media au mitandao ya kijamii, kilichonisukuma kuandika bandiko hili ni kufuatia waandishi mbalimbali wasivyoitendea haki taaluma hii laadhim ambayo kila mtu anashiriki kwa kuandika habari, ikumbukwe kuwa mwanadamu awaye yote duniani anayejua kusndika na kusoma ni mwandishi wa habari au msomaji wa habari lakini wapo kundi la watu wachache ambao ni wabobezi wa taaluma hii muhimu ktk jamii. Katika nchi yetu taaluma ya habari imepoteza sifa baada ya kutumiwa vibaya hasa na wanahabari wenyewe badala ya kuandika habari wanaandika umbeya kuanzia kwenye social network priting mpk eletronic media. Mwandishi wa habari makini uandika habari iliyoksmilika na wenye uchambuzi wa kutosha isiyo na chembe ya kumuacha msomaji na maswali lkn kwa wanahabari wetu ni tofauti kabisa. Wanahabari wa tanzania hawana muda kufuatilia habari na kuona mwisho wake wanahabari wetu wakishaandika habari wanapotea na habari yao, waandishi wa habari makini ujenga hoja na kuibua issues na kutengeneza ajenda za kitaifa lkn kwa nchi hiyo haipo waandishi wetu wanapenda kuandika umbeya usiyo na tija. Duniani kote wanahabari na idara za kijasusi ndiyo watengenezaji wa ajenda za kitaifa za kujadiliwa lkn tanzania hapa ni tofauti wanahabari wameacha kuchukua majukumu yao na kuwachia wanasiasa na idara ya ujasusi kutengeneza ajenda na media zetu wamepokuwa wapokea ajenda na kupublise bila wao kujua. Nilitegemea jukwaa la wahariri kusaidia kurekebisha hili kasoro lkn nalo limekuwa jukwaa la kutafuta deal kwa watendaji wa taasisi mbalimbali na kuwatishia kuwalipua ili tu wapewe semina limeacha kuset ajenda za kitaifa. Ushauri wangu kwa waziri anayesimamia sekta hii ndg Nape Nnauye na timu ya wizara, waziri anayesimsmia sekta mawasiliano ndg makame mbarawa kurugunzi ya mawasiliano ikulu kuangalia namna wanaweza kuokoa sekta ya habari nchini, ni vyema sheria ya magazeti, sheria ya usalama wa taifa na sheria ya mawasiliano ikasimamiwa vzr na kwa ufasaha ili kulinda tasnia hii najua kutakuwa na malalamiko kutoka vyombo vya Habari na Makundi fulani fulani kuhusu kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari lakini ni bora kulaumiwa kwa muda mfupi kwa kutengeneza kitu cha muda mrefu yenye maslahi kwa wanahabari na taifa kwa ujumla. Tutengeneze media yenye tija kwa taifa kuliko aina hizi za media tuliyonayo. Tutengeneze media inayoseti ajenda kuliko media inayosubiri ajenda toka kwa wanasiasa na idara ya ujasusi. Kuna changamoto kubwa kutumia politicals agenda ajenda za wanasiasa inaweza kuingiza nchi kwenye matatizo makubwa. Tuanze sasa kuokoa vyombo vyetu vya Habari
 
Back
Top Bottom