Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 994
Kuna Utaratibu wa kuvisha Medali za thamani kama za dhahabu, fedha na nyinginezo. Ni jambo zuri linamhamasisha mshindani aweze kufanya vyema zaidi. Nimezoea kuna Wakimbiaji wakipata medali hizo. Mfano Bayi, Nyambui na karibuni akina Simbu wanazipata medali hizo. Lakini pia kuna medali zinatolewa kwa wachezaji wengine kama wa mpira wa miguu, pete, tenisi, kikapu n.k. Ikamifanya nichimbe kidogo:
Maana ya Medali ni nini?
NOMINO/plural medali
Usipoteze muda na sarafu hizi za kawaida za kununua na kuuza kama senti tano (wachache tulizitumia humu), au shilingi 500 ambayo sasa unaweza kuitumia kama nauli ya daladala. Hapana, namaanisha hii inayotolewa kama zawadi au tuzo kwa mshindi wa jambo fulani na akathaminiwa (challenge coin). Ndiyo maana nimetaja hapo juu kuhusu tuzo walizopata wakimbiaji wetu maarufu.
Asili yake
Historia ya zamani sana kwa sarafu hizi ni tawala kuu kama za Misri na Rumi. Lakini mimi nataka nijikite kwa hizi zenye historia iliyoandikwa. Machapisho mengi yanaonyesha asili yake ilikuwa majeshini ambako Kamanda aliyefanya vyema kitengo fulani alitunukiwa. Polopole ikaanza kutolewa na wanasiasa hasa kwa hao wanajeshi waliofanya vyema lakini hatimaye ikaanza kutolewa hata kwa ndugu wa hao wanajeshi. Majeshi katika vita ya kwanza ya dunia yalitoa tuzo hizo. Hatimaye Rais wa Marekani (US) naye alituzwa na hata naye akaanza kuwatuza aliowapendelea tuzo hiyo miaka ya 1990.
Matumizi kwa sasa na umuhimu wake
Hivi karibuni matumizi ya sarafu hizi ni makubwa kwa majeshi, michezo na hata kwa wasomi na makampuni yakipeana zawadi ama tuzo za aina hii. Nje ya majeshi, Rais wa Marekani hutoa tuzo hizi, na tumeona zikipata msukumo zaidi utawala wa Clinton, Bush, Obama na sasa Trump. Nje ya majeshi pia hizi sarafu hutulowa ama kubadilishana kama tuzo katika Michezo, Elimu, Biashara, Siasa, Vyama vya SKauti na Syansi kwa ujumla.
Siri katika Sarafu
Kuna siri katika Sarafu hizi ambazo zinaanzia hata katika kupeana. Ukisoma mitandaoni utagundua Obama aliwahi kutoa zawadi ya sarafu kwa kwa siri wakati wakisalimiana. Sarafu hii pia yaweza kutumika kumfuatilia mtu (secret agent)...hapo sisemi sana. Lakini pia utoaji wake unahusika na alama, nembo na uwakilishi wa siri kulingana na mtoaji. Ninapenda kuachia hapa kwasasa nitaweza kuongelea zaidi katika siri za sarafu ambazo zaweza kuwa za kijasusi nikipata muda. Mimi niliwahi kupewa kwa siri sarafu hii (Jeshi la nchi moja kubwa) lakini hadi sasa sikuweza kuambua (kupata maana yake nyingine) ukiachilia niliyoambiwa kuwa ni kwasababu ya yale niliyofanya vizuri katika Sayansi
Nakutakia usomi mwema....chimba zaidi upate maarifa katika Sarafu hizi
Maana ya Medali ni nini?
NOMINO/plural medali
- kitu cha madini k.v. dhahabu, shaba au fedha kitolewacho kuwa ni tuzo kwa mshindi au kutunukiwa mtu aliyefanya jambo au kazi ya kuthaminiwa.