Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,792
- 31,804
Jina la Abdulwahid Sykes (1924-1968) katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sasa halihitaji kuelezwa sana.
Historia yake imekuwa ni historia ya kusisimua unapomsoma kuhusu yale aliyofanya katika kuunda chama cha TANU 1954 akianza na kubadilisha mwelekeo wa TAA alipoingia katika uongozi wake 1950.
Historia ya Abdul Sykes pia ina masikitiko pale baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 juhudi za makusudi zilipofanywa kulifuta jina lake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kwa hili si tu kuwa lilifutika jina lake peke yake bali na jina la mdogo wake Ally na la baba yao Kleist Sykes aliyekuwa muasisi wa African Association mwaka wa 1929.
Ilichukua miaka 50 kwa Abdulwahid na mdogo wake Ally kutunukiwa medali ya ‘’Mwenge wa Uhuru,’’ kama utambuzi wa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika wakiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliyemfahamu mwaka wa 1952.
Leo nimebahatika kuiona medali ya ''Mwenge wa Uhuru'' aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes (post homous) na Rais Kikwete katika Viwanja vya Ikulu tarehe 9 Desemba, 2011 katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
Kuishika medali hii kwa mikono yangu kwangu kilikuwa kitu kilichokuwa na nafasi ya pekee katika moyo wangu.
Mwenge wa Uhuru 1961 - 2011
(Picha kwa hisani ya mjukuu wa Abdulwahid Sykes Aisha Kleist Sykes)
Ingia hapo chini kuangalia picha:
Mohamed Said: MEDALI YA ABDULWAHID SYKES: MWENGE WA UHURU 1961 - 2011