Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 33,207
- 74,806
Baada ya kuunguruma kwa takribani miezi tisa (August -May),hatimaye leo tunaelekea kwenye mwisho wa msimu wa Ligi kuu ya soka Tanzania Bara (VPL)
Leo hii viwanja 8 vitawaka moto,lakini macho na masikio ya wengi vitaelekezwa Mwanza ambapo timu iliyojihakikishia ubingwa Dar Young Africans itaumana na Mbao FC inayopambana kukwepa panga la kushuka daraja.
Ikumbukwe ya kwamba timu hizi mbili zinakutana mara 2 sasa ndani ya mwezi mmoja.
Mechi iliyopita Mbao walifanikiwa kuwafunga Yanga bao 1-0 katika mchezo wa kombe la shirikisho nusu fainali. Ushindi huo uliwapa Mbao tiketi ya kushiriki fainali,huku Yanga wakielekeza machungu yao kwenye ligi kuu ya Tanzania bara ambako walishinda mechi zao zote.
Hivyo mechi ya leo ni ya kulipa kisasi kwa Yanga dhidi ya Mbao huku Mbao wakipambana kufa na kupona kubaki ligi kuu.
Uwanja wa Taifa Wekundu wa Msimbazi watawakaribisha Mwadui FC.
Mechi hii wengi wanasubiria miujiza endapo Simba wataweza kuwafunga Mwadui mabao 15 ili kuchukua Kombe la ligi kuu ambalo Watani wao Yanga wana uhakika wa kulichukua kwa mara ya tatu mfululizo.
Viwanja vingine ni
Azam Complex Mbagala ambapo Azam wataumana na Kagera Sugar
Majimaji Ruvuma
Majimaji FC vs Mbeya City
Uwanja wa Sokoine Mbeya
Tanzania Prisons vs African Lyon
Uwanja wa Kambarage Shinyanga
Stand United vs Ruvu Shooting
Mechi zote ni Saa 10:00 Jioni,tukutane hapa kwa updates.
=====================================
Updates
Mpira unaanza Kirumba Mwanza
Yanga 0-Mbao