Mechi ya waheshimiwa wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mechi ya waheshimiwa wabunge

Discussion in 'Sports' started by POMPO, Jul 5, 2012.

 1. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakuu,
  kuna matangazo mbalimbali yanaendelea hapa nchini kuwa kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu uwanja wa taifa DSM, JMosi kati ya waheshimiwa wabunge wapenzi wa YANGA dhidi ya wazao wapenzi wa SIMBA, hivyo itakuwa ni SIMBA vs YANGA.
  wana JF:

  Je ni sahihi kwa (wanasiasa)wawakilishi wetu kushiriki mchezo huo aliakuwa nchi inakabiliwa na mgomo wa madaktari? I mean watu wanapoteza maisha, wanateseka na ni miungoni mwa watu waliowachagua wakawawakilishe?
  nimeweka uzi huu jukwaa la siasa, wanashiriki wanasiasa wetu, mbaya zaidi ni wote hata wa upinzani.
  Tafakari.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  JK LAZIMA AWE REFA MECHI YA WABUNGE

  Na Haruni Sanchawa
  MBUNGE wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni lazima awe refa wa pambano la wabunge wapenzi wa Simba na Yanga litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7, mwaka huu.
  Kauli ya Nchemba aliyoitoa juzi kwa mwandishi wetu inapingana na ile ya Mbunge wa Kigoma Mashariki, Zitto Kabwe ambaye ni mchezaji wa wabunge wa Simba aliyesema kuwa Rais Kikwete hafai kuwa refa wa pambano hilo kwa kuwa ni shabiki mzuri wa Yanga na anaamini kuwa atawapendelea wabunge wa timu anayoishabikia.
  "Zitto ni muoga tu, wasubiri kichapo, Rais Kikwete hawezi kutupendelea sisi (Wabunge wapenzi wa Yanga) na ukweli huo utaonekana siku hiyo ya mchezo," alisema Nchemba.
  Pambano la Wabunge wa Simba na Yanga linangojewa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka kwani ni la aina yake na kwa mujibu wa mmoja wa waratibu wa pambano hilo, Luqman Maloto, viingilio vimepangwa kuwa shilingi 10,000 kwa viti maalum (VIP) na shilingi 5,000 kwa viti vya kawaida.
  Maloto alisema anaamini pambano hilo litakalofanyika siku ya Usiku wa Matumaini litakuwa kali na la kusisimua kutokana na kila upande kujiandaa vyema. Licha ya mpira wa miguu kutakuwa na burudani mbalimbali uwanjani hapo ambapo mwanamuziki Chamelione wa Uganda na Diamond wa Tanzania watatumbuiza na wapenzi wa ngumi watajionea mchezo huo.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nimemkumbuka Mac vivien foe.
  Kama kuongea tu huanguka na kuzimia.
  Ili kutuokoa na ccm, Mungu anatuletea ukombozi bila kugoma wala kuandamana.
  Mpeni kipyenga jk tuingie kwenye uchaguzi!!!!
  Wabunge wa upinzani nawashauri wasitie mguu uwanjani ili kuepuka kisingiziwa wamemkata mitama kwa stail ya kigaidi
   
 4. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  watu wanatafuta pesa ya kula kaka
   
 5. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mzee akilimali ndani....
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaaa!!
  Akivua kibarakhashia tu Yanga wanafungwa!!!
   
 7. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280

  Huu ndo tunauita upompompo hivi bongo timu ni Simba na Yanga tu? Hivi mnajua kinachoua soka la bongo ni usimba na uyanga? Aaa argh! Wanauzi bora wangejigawa kwa mfumo mwingine ila sio wa usimba na uyanga Sasa sisi mashabiki wa AFC, toto, nyota nyekundu, mecco, reli, mbanga FC tushabikie wapi?
   
 8. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 257
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wangelicheza CHADEMA NA CCM
   
 9. t

  thinka JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Chadema hawatoshi labda wakiongeza viti maalum
   
 10. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  kwanini wasitoshe? sugu,mnyika,wenje,heche,mdee,silinde, mbowe,msigwa,zitto,shibuda,nasary..etc sio timu hiyo?
   
 11. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acheni kukurupuka, sio kila kitu mnapinga tu. Mechi ya leo, pamoja na michezo, imeandaliwa ili kukusanya fedha za kusaidi ujenzi wa mabweni ya wasichana wanafunzi sehemu mbalimbali za nchi.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Acha upoyoyo timu ulizo zitaja ni matawi ya Simba na Yanga na wachezaji wengi wa timu hizo utakuta ni wanazi wa ama Simba au Yanga na yanga na Simba hawajaua soka nchii.. kinachouwa soka ni mfumo mzima wa soka la tanzania kuanzia TFF...
   
 13. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  Tunaomba Updates mechi ikianza:eek2:
   
 14. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Kama refa ni atakuwa wa ccm nadhani kabla ya dk90 kuisha watakuwa wamebaki wachezaji watatu wengine wote ni red card
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hasa hasa Makinda, Ndugai, na wenyeviti wao...
   
 16. m

  mob JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  wengebaki dodoma kupitisha bajeti ,hiyo mechi ina tija gani kwa taifa
   
 17. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ....ni wasiwasi na refa.
   
 18. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  nilijua wauwaji wa soka la bongo Simba na Yanga mtakuja juu! Hivi AFC ni tawi la Simba au Yanga? Wachezaji wa kibongo kipimo CHA mafanikio kisoka ni hizo timu ambazo mfumo, na serikali inazibeba lakini mafanikio yake ni madogo ila ni MAKUBWA ukilinganisha na vilabu vingine kwa Mara nyingine tena muhimili mwingine wa dola unazitangaza Simba na Yanga.... Huyo Nchemba anashabikia wakati Singida hamna timu ni muongo Sasa hivyo hivyo Zitto Kigoma hamna kitu anakalia usimba na uyanga
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Vikosi vya timu zote vikoje?
   
 20. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ndio mech kati ya wabunge wa yanga na simba
  UPDATE zitto anachezea simba ni noma kumbe na mpra anaujua . Nchemba nae yupo ft anachezea yanga
   
Loading...