Inabidi wanafunzi mtambue kua course haimpi mtu pesa, ni akili ya mtu mwenyewe anaitumiaje kutengeneza pesa. Ndio maana kuna mtu analima na kupeleka nyanya sokoni kuuza bei ndogo, na mwingine anatafuta customers wakubwa anakodi shamba kubwa mno zikikua anauza zote kwa mpigo moja na kutengeneza pesa ndefu.
Its the same thing kuuza nyanya lakini akili tunatofautiana.
Mechanical au IT, zote unaweza tengeneza pesa na zote unaweza kufulia vilevile usipate kazi na ukashindwa kujiajiri. Cha muhimu ni kupenda unachokifanya na kua the best at it, in short TUMIA AKILI. Na usijilimit, unaweza somea Mechanical engineering alafu ukaenda kufanya biashara. Kutengeneza pesa kuna-involve mtu ulivyojipanga kusolve tatizo tu basi, ona tatizo watu walilo nalo, tafuta solution, tengeneza pesa, najua watu waliopiga shule chini hawajamaliza form six leo wana milioni 100 kwenye account. Tumia Akili.