Mdomo mchungu sana

Mdomo mchungu sana

Misunderstood

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2020
Posts
393
Reaction score
896
Habari zenu madaktari na wadau wa afya!

Nina shida mdogo wenu week inaelekea ya pili sasa nimekuwa na mdomo mchungu mnooo, hasa nikiamka asubuhi. Saingine nasikia kama tumbo kuuma ila sina, na mdomo mchungu kuanzia ulimi, sehemu ya juu ya mdomo, kwenye koo nakua kama nakabwa na kohozi ambalo haliishi. Sasa nikiamka asubuhi ndo shida hasa hasa mdomo mchungu sana.

Nimeenda hospital nikapimwa malaria na UTI nikaambiwa sina shida wakanishauri nitumie dawa za gesi nimetumia but in vain. Napigwa mswaki karibia kila saa ila wapi! Nakula vitu vitamu vitamu ila wapi. Naombeni msaada kwa atakaejua nini shida na nitumie dawa gani.

Asanteni
 
Dawa yake ni nini?
Nenda hospital dada.

Usiende hospital za vichochoroni watakupa panadol na colgate uendelee kuswaki.

Ila angalia na vidonda vya tumbo hiyo hali hupelekea kupata vidonda.

Ukienda hospital ukampata dr mtaalam atakupa tiba ikufaayo.
 
Back
Top Bottom