Mdee: Najua kilichomrudisha Lowassa CCM, Serikali imembana sana kwenye mali zake na familia imebidi aombe poo

Chadema wachague kuwa na busara- issue ya ENL kurudi CCM wasiongelee kabisaaa.

Kwa nini Lowassa ndio wasiongelee lakini Waitara na huyu na yule na wengine waongelewe kwamba wacha waende wamenunuliwa?

KWA NINI Lowassa and only Lowassa anaagwa kwa unyoronyoro na mabusu ya good bye ??!!
 
Wewe unawazuia kama nani kuongea? Acha uoga wa kifisiem!

Kama alikuja kwa nini asiondoke?.

Kila mwenye akili alijua ataondoka, kwa hiyo hakuna jipya. Wanaongea kupata faida gani?.

Wakiongea wanajikaanga, kwani tuliwaonya. Wakiongea wanadhibitisha maneno ya Dr. Slaa kuhusu ENL.

Wasiwe kama CCM waliomtusi ns kumsema huyu mzee alipoondoka kwao. Watulie tu. Isije ikatokea anarudi tena wakawa na aibu kama Polepole & co.
 
Mdee amefunguka hayo wakati akijibu swali kuhusu maoni yake kufuatia aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mgombea huyo wa Urais mwaka 2015 kwa mwamvuli wa Ukawa, tangu aliposema 'amerudi nyumbani'.

"Natambua changamoto nyingi anazopitia za kifamilia na kibiashara, akalazimika kuomba po! sikuona haja ya kusema chochote nikiheshimu uamuzi wake. Najua nafsi yake inavuja damu ya usaliti kwa waliompa heshima na ‘kumrudishia uhai’"Halima James Mdee.

Edward Lowassa alirejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, ya wiki iliyopita na kupokelewa na uongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti, Dk. Joh Pombe Magufuli.

Baada ya kurejea CCM, Lowassa hakuzungumza chochote zaidi ya kusema tu kuwa, "nimerudi nyumbani".
Kwa sasa siwezi kuwa na imani na mwanasiasa yoyote bali najitaidi kujenga imani juu ya Tanzania yangu.
 
Mzee popote penye fursa ya kuupata udereva lzm apatumie,wampe ufunguo 2020.Baada ya Mbowe Kugoma kufika bei heri waondoke na Lowasa.Mzee anachoma nyama Monduli Leo vigelevigele mwanampotevu kurudi home
 
Wewe kusoma hujui ata picha lilivyochezwa hujaona tuuu,au ndo unakuja kutopoteza hapa tujue kwamba serikali ilimbana
 
Mdee amefunguka hayo wakati akijibu swali kuhusu maoni yake kufuatia aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mgombea huyo wa Urais mwaka 2015 kwa mwamvuli wa Ukawa, tangu aliposema 'amerudi nyumbani'.

"Natambua changamoto nyingi anazopitia za kifamilia na kibiashara, akalazimika kuomba po! sikuona haja ya kusema chochote nikiheshimu uamuzi wake. Najua nafsi yake inavuja damu ya usaliti kwa waliompa heshima na ‘kumrudishia uhai’"Halima James Mdee.

Edward Lowassa alirejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, ya wiki iliyopita na kupokelewa na uongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti, Dk. Joh Pombe Magufuli.

Baada ya kurejea CCM, Lowassa hakuzungumza chochote zaidi ya kusema tu kuwa, "nimerudi nyumbani".

Mkumbusheni Halima Mdee kuwa leo ni siku ya Wanawake duniani. Lowassa keshaamua hata kama Halima alidhani zamu hii angepata tena milioni 200 kama ilivyokuwa mwaka 2015. Kila jambo na msimu mama, Happy women's day!
 
Hapana huwezi kuzuiya kusichwe

Jr
emoji769.png

Wakiongea wanajizidishia maumivu na kujikaanga.

Ukarimu waliompatia wakati wa hasira zake za mkizi haukutakiwa kulipwa hivi. Mzee Kigunge alienda nae akakomaa nae hadi umauti
 
Kama waliweza kuhimili kuondoka kwa wabunge, zitto, slaa, kabouru na wengine wengi tu wapotezee.
Waendelee na yao.
 
Back
Top Bottom