Mdee na Ardhi - Je Tanzania tunaelekea wapi?

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Mh. Halima Mdee amegusa maisha ya Watanzania wengi.

Serikali ipo na inakusanya kodi ili itoe huduma kwa wananchi.

Kila Mtanzania analipa kodi, penda asipende. Ni lazima, ila watanzania wengi hawajui kuwa wanalipa kodi ya VAT.

Kila bidhaa unayonunua ina VAT.

Hivyo basi kupima viwanja na kuwagawia wananchi wake ndo huduma za serikali. Sasa kama serikali inawauzia wananchi ardhi/viwanja, je wasio na uwezo waende wapi. Njedengwa, Manyara, Mbarali, Kule kawe pugu kumetokea machafuko ya ardhi. Hiyo ni kwa sababu serikali haiwajali wananchi.

Kazi ya watendaji wa serikali ni kupima ardhi tuliyopewa bure na Mungu halafu wanaiuza. Hata Kule Burka arusha wameuzia ardhi makaburu na vigogo wa serikali na CCM.

Halima Mdee naomba ukalisemee hili bungeni kuwa serikali isiwauzie wananchi ardhi yao waliopewa na Mungu. Kwa nini Wawekezaji,Vigogo wa Serikali na CCM wachukue ardhi na kukalia wakati wananchi wanataabika.

Source: Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom