mdau gladys kasesela awaombea mama na watoto msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mdau gladys kasesela awaombea mama na watoto msaada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Jul 1, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Mama na watoto wake wanaoishi ufukweni ​
  karibu na hospitali ya Ocean Road jijini Dar
  [​IMG] Mdau Gladys Kasesela akipozi na mama na watoto ​
  wake baada ya kuwapa zawadi ya miamvuli na nguo leo

  Kwa wadau wa watoto wote
  Kwa wale wanaopita barabara ya Ocean Rd karibu na Hospitali ya
  Aghakhan utaomuona mama mmoja amekalia gogo akiwa na watoto wanne
  wamemzunguka, mama huyu amekuwa anaishi eneo hili kwa muda mrefu.
  Nasikitika kuwaeleza wapenzi wa watoto kuwa mama huyu amejifungua
  mtoto wa 5, ukiangalia picha utaona kama amebeba katoto. Mama huyu na
  watoto hawa wamekuwa wanaishi maisha ya hatari sana.

  Mama huyu baada ya kuongea naye aliomba wasamaria wema wajitokeze kwa
  ajili ya kulea watoto, wasi wasi wangu je sheria inasemaje, maana
  sheria mpya watoto naamini ilipitishwa hivi karibuni, na pia juzi tu
  tumetoka kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.
  Kuna uwezekano kabisa mama huyu ana matatizo ya kiakili (mimi si mtaalamu kwa hiyo sina uhakika) lakini ana kumbukumbu kwamba baba ya watoto hawa, baba wa kwanza ni mchaga (mtoto anaitwa Haika), mtoto wa pili baba yake
  Mkikuyu, mtoto wa tatu wa mgiriki , mtoto wa nne kazaa na Mkongo wa
  nne anasema ni Mfaransa.

  Leo hii nilipita ikabidi nimpe miamvuli na baadhi ya nguo, utaratibu
  ambao nimekuwa nafanya mara kwa mara, pia ameniambia Mh Batilda Burian
  amekuwa anamsaidia sana.

  Nawaomba wadau mjitokeze kumsaidia mama huyu,
  hasa watoto ambao wana kosa elimu na malezi bora.

  Ahsante
  Mdau Gladys Kasesela

  source: issamichuzi.blogspot.com

  Gladys, Hii kitu imewahi kutundikwa hata hapa, inasikitisha sana, sana sana, maneno, picha maandishi hayatoshi. Naomba kwa niaba ya wote wanaona, kuyafikiria kuumizwa na kuyahisi mateso anayopata huyu mama na watoto wake nikushukuru wewe pamoja na wote waliowahi tutoa thread humu na kuongeza machache( kama ni machache) na kuomba wengine wachangie.

  Pamoja na shukrani zangu zote nina matatizo matano:

  1. Maisha ya huyu mama ni ya siku zote ( sio dharula) utatoa miamvuli, nguo na chakula kila siku? Watoto hawasomi na wanazidi kukua je unaona umesaidia tatizo kwa mama na watoto au umetoa dawa ya maumivu tu?

  2. Una bahati unapita njia ya Aga Khan Hospital, umewahi kujiuliza Dar Es Salaam wako watu wangapi kama huyu mama na wanae, je umefika Manzese, Mwananyamala, Kigogo, Mbagala, Machimbo? Je umeenda mikoani, wilayani tarafani na kwenye kata, aina ya huyu mama wako wangapi? nani anaweza kuwapa nguo na miamvuli, kama ilivyofanyika?

  3. Umeambiwa na mhusika kuwa Waziri Buriani anajua hili Tatizo hili na amekuwa anamsaidia, ningekuwa mimi nisingesema kitu kama hicho ni aibu na fedheha kubwa sana kama waziri anamsaidia mama mwenye watoto watano kukaa barabarani badala ya kutafuta suluhisho la kudumu la huyu mama na watoto wake na Watanzania mamilioni walio na matatizo kama huyu mama na wanae.

  4. Kumbuka sheria zinazotungwa na bunge zina malengo yake hazina uhalali hata kidogo, huwezi kumlazimisha baba au mama kumlea mtoto wakati hana uwezo wa kufanya hivyo. Tuwe wakweli hakuna mama na au baba anayependa mtoto wake akae baharini toka asubuhi mpaka jioni akiombaomba, bila kwenda shule. Sheria hii ilitungwa na wafadhili na kupitshwa na bunge bila kuangalia kuwa matatizo kama hayo yanatokana na umaskini wa watanzania mamilioni. Kama bunge lingekuwa makini na wafadhili wangekuwa serious wasingeleta sheria hii.

  5. Kabla ya kumalizia, katiba iko wazi kuwa :Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi ni jukumu la serikali kuona kuwa huyo mama na wanaye wanatunzwa na serikali kwa hali na mali. Hakika si jukumu la watanzania wachache wenye utu na huruma.

  6. Mwisho, ni ajabu hiyo ndio njia (Ocean Road) ya asilimia 70 ya viongozi wa serikali wanayopita kwenda ofisini, hivyo kwani ni wote hawajiliona hilo tatizo na kulitafutia ufumbuzi? Mpaka Gladys ajitotekeze na kuomba msaada kwa wanachi wachovu. Au tunarudia hadithi ya wanafunzi kumchangia mgombea wa CCM hela ya kuchukulia fomu za kugombea.

  Sio kwamba simuonei huruma huyo mama na wanaye, la hasha, ila kama tungegawana kidogo tulichinacho nacho walahi huyu mama na wanawe wasingekuwa wanashinda pale na kuonwa na viongozi wote wa serikali bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

  Maisha ya huyu mama ni kielelezo cha mamilioni ya Watanzania.


   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana 100% na mtoa maelezo ya nini kifanyike, hizo ndio sera za CCM tunayoipigia kura kila siku. Ila kama kuna wadau wa family planning wnaweza kufanya jambo la haraka la kumfunga kizazi huyo mama kabla hajaendeleka kuzaa bila kikomo.
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kwani huyu Mama ametokea wapi mpaka akafika hapo Ocean Road...??

  Maana kuna siku alikuwa anagombana na walinzi wa pale Gymkana Club (walitaka kumfukuza kutoka chini ya ule mti mkubwa).... akawa anasema kwamba sio kuwa amependa yale maisha, ila amelazimika... alikuwa na nyumba yake nzuri na maisha yake mazuri... but she has been ruined

  Kama inawezekana huyu mama ahojiwe chanzo cha yeye kuwa pale, inawezekana ameathirika kimawazo kwa sasa lakini anajua anachokifanya... Angalia watoto wake, ni wasafi, hawali chakula cha jalalani, anawavalisha masweta kila asubuhi na jioni...

  Anyway, huo ni mtazamo wangu tu...
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Inaweza kuleta matatizo ya litigation, umesikia Naminia majuzi ambako kuna wamama walifungwa kizazi bila ridhaa kwa sababu walikuwa HIV Positive wameitundika serikali yao mahakamani.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kama ambavyo watanzania wengi wasivyopenda kuishi wanavyoishi, ila wanalazimishwa na hali kutojaliwa na serikali. Sio yeye tu aliyekuwa ruined ila watanzania mamilioni wako hivyo yeye ni muwakilishi wa watanzania wote.
   
 6. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mi huwa nashangaa sana kumwona huyo mama akiwa hapo na familia yake yote na huku vyombo vya dola vikishuhudia. Hivi hakuna sheria inayozuia watu kuzurura hovyo mitaani na familia zao? Inawezekana kweli ana matatizo lakini nadhani vyombo vya dola vingeweza kumkamata kwa mahojiano zaidi na ikibidi arudishwe kwao maana kuna sehemu alikuwa anaishi kabla ya kuja bongo. Tukiruhusu mchezo huu wa kuwachangia watu hawa ili waendelee kukaa maeneo yasiyo rahisi tutakuwa tunafuga ugonjwa utakaoleta shida kubwa. Wako watu wenye matatizo makubwa tu na wakijua wakija kuishi mjini watasaidiwa tutakuwa tumewapa mwaliko usio rasmi na itabidi tujiandae kwa hilo.

  Mambo haya huwa yanaanza kidogokidogo na tukija kushituka litakuwa tatizo limeshakuwa kubwa (DECI style!!!). Jambo hili lisifumbiwe macho na vyombo vya dola. Mpo hapa nadhani mmenisikia
   
 7. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  huyu mama ameshasaidiwa na kuondokahapo barabarani?

  update please
   
Loading...