Nimemsikia Mkuu akisema wanamsingizia kuwa yye Dikteta wakati analaumiwa kwa kuaachia uhuru wa ziada, ndio akasema sasa wanataka ajaribu kuwa dikteta, abakishe TBC, Daily News na Habari Leo na Uhuru la Chama? Akasema hatuwezi kurudi huko maana tulishapita zamani na kwamba hata anayemshutumu naye yuko huru ndio anaweza kusema Rais Dikteta, vinginevo Dikteta ukimuita Dikteta unakamatwa na kupotezwa. Je, kauli hii inahusiana na kitisho cha TCRA? Kwamba wanamsingizia yeye Dikteta wakati ni mpole anaachia media inafanya itakavyo?