Swali, kama watanzania watakupa ridhaa ya kuwa raisi wa nchi atahakikishaje kwamba mapandiliko yatakuja bila kusababisha vurugu.
Anasema, Vurugu haziwezi letwa na wananchi wenyewe, vurugu zinaweza letwa na serikali, vyama n.k
Mfano, serikali ya sasa ya CCM inaleta vurugu, (vijana wao) na Polisi haiwachukulii hatua, anatolea mfano wa Green guard ambao wamepata mafunzo ya kijeshi.
Anasema, Green guard wakiachiwa wakaendelea, watanzania watachoka kuvumilia na hapo ndipo uvunjifu wa aman utatokea, kwa hiyo ni kwa sababu polisi hawafanyi kazi yao. Kama wangefanya kazi yao vizuri, pasingekuwa na vurugu yeyote.
Yeye hataki kwenda Ikuru kwa watanzania kumwaga damu.