MCT: Serikali haikulitendea haki Mwananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MCT: Serikali haikulitendea haki Mwananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Feb 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  MCT: Serikali haikulitendea haki Mwananchi
  Wednesday, 09 February 2011 21:51

  Boniface Meena
  [​IMG]RIPOTI ya Kamati Maalum iliyoundwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), kuchunguza tuhuma na tishio la Serikali dhidi ya gazeti la Mwananchi imeeleza kuwa tishio na tuhuma hizo ni za kisiasa na si vinginevyo.

  Taarifa ya ripoti hiyo ambayo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa MCT, Jaji Dk Robert Kisanga alieleza kuwa gazeti la Mwananchi liliripoti kwa haki na usawa kampeni za uchaguzi kwa vyama vyote ikiwemo CCM.

  Kamati iliyoandaa ripoti hiyo ni ile iliyoundwa na MCT na kutangazwa Novemba 26, 2010 ikiwajumuisha wajumbe watatu wakiongozwa na Profesa Luitfried Mbunda ambaye ni profesa wa sheria aliyebobea katika sheria za uhuru wa habari.

  Wengine walikuwa katika kamati hiyo Iliyopewa muda wa siku 30 kukamilisha kazi yake ni Gema Akilimali ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kijinsia na haki za binadamu na Attilio Tagalile ambaye ni mwandishi na mhariri wa siku nyingi katika vyombo vya serikali na binafsi ndani na nje ya nchi.

  Hatua ya MCT kuunda kamati hiyo kuchunguza malalamiko ya chombo cha habari, ni ya kwanza katika tasnia ya habari Tanzania, ingawa fursa hiyo ilikuwepo kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwa chombo hicho.

  Akitoa taarifa hiyo jana, Jaji Kisanga alisema kamati ilibaini kuwa tuhuma na tishio la serikali dhidi ya gazeti la Mwananchi viliingilia isivyostahili uhuru wa habari na wa kutoa maoni hivyo tuhuma hizo zilitishia maslahi na uhai wa gazeti hilo.

  "Vilevile kamati maalum iligundua kwamba kuna baadhi ya magazeti yaliyoonywa na serikali kwa lugha isiyo kali licha ya kwamba yalichapisha madai hasi mazito,"alisema.

  Alisema kuwa kamati hiyo iligundua kwamba kuna baadhi ya magazeti ambayo yalikuwa yakichapisha tuhuma nzito lakini badala yake serikali iliwaalika kwa majadiliano.

  "Kwa hili kamati maalum iliona kwamba hakukuwa na uwiano sawa (yaani kulikuwa na double standards),"alisema.

  Kutokana na hilo Jaji Kisanga alisema kuwa kamati maalum imependekeza kwamba kabla ya kuchukua uamuzi wowote ambao unaminya uhuru wa chombo cha habari, upo umuhimu kufuata kanuni ya kumpa mtuhumiwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa.

  Alisema vilevile kamati maalum ilipendekeza kwamba sheria zinazokandamiza uhuru wa kutoa habari na maoni zirekebishwe au kufutwa kabisa na kwa upande mwingine serikali iwezeshe kuundwa kwa sheria ambazo ni rafiki kwa vyombo vya habari kama ilivyopendekezwa na wadau.

  "Bodi ya baraza imeridhika na inaridhia ripoti ya kamati maalum. Bodi inakubali hitimisho na mapendekezo ya kamati na itayafanyia kazi zaidi.Taarifa nzima ya kamati itachapishwa hivi karibuni kwa manufaa ya umma,"alisema Jaji Kisanga.

  Jaji Kisanga alisema kuundwa kwa kamati kuchunguza tuhuma hizo ilitokana na barua iliyowasilishwa MCT Oktoba 20 mwaka jana na Mhariri Mtendaji wa gazeti hili ikiwa na kichwa cha habari kilichosomeka "Vitisho vya Serikali dhidi ya Gazeti la Mwananchi".

  Alisema katika barua hiyo Mhariri alidai kuwa serikali imetishia kulisimamisha na hata kulifungia kabisa gazeti hili kama lisingesitisha mara moja kuchapisha habari zenye mwelekeo wa 'uchochezi' na 'kuidhalilisha' serikali.

  Jaji Kisanga alisema kwa mujibu wa Mhariri, Mwananchi halikuwa likiamini kwamba linachapisha habari za aina hiyo, hivyo walimwandikia Msajili ya Magazeti barua wakimwomba awape ushahidi au mifano ya habari na picha za aina hiyo ili waweze kujua hatua za kuchukua.

  Alisema hata hivyo, Mhariri katika barua yake alisema badala ya kupewa mifano waliyoomba, Msajili aliwaandikia onyo kali na kutishia kulifungia gazeti hilo ikiwa lisingeacha mwenendo wake hasi dhidi ya serikali.

  "Baada ya hatua hiyo ya serikali, Mhariri Mtendaji wa MCL alifikisha rasmi maombi MCT akiomba kufanyika kwa uchunguzi kwa mujibu wa katiba ya baraza na taratibu zake ili kubaini ukweli wa madai hayo mazito ya serikali,"alisema Jaji Kisanga.

  Alisema bodi ya MCT ilijiridhisha kwamba shauri hilo liligusa maslahi ya umma na uhuru wa vyombo vya habari na hivyo lilihitaji kuundiwa kamati maalum itakayochunguza madai hayo na kamati hiyo ndiyo iliyotoa ripoti baada ya kufanya uchunguzi wake.


  Oktoba 11, 2010, Serikali ilitishia kulifunga au kulifutia usajili gazeti la Mwananchi kwa madai kwamba linaandika habari za uchochezi dhidi ya serikali ya awamu ya nne.

  “Kwa barua hii unatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuandika habari za uchochezi na kuidhalilisha nchi na serikali kwa kisingizio cha uhuru wa habari na uhuru wa kutoa mawazo ulioanishwa katika katiba ya nchi yetu," ilieleza barua hiyo iliyosainiwa na Raphael Hokororo kwa niaba ya Msajili wa Magazeti.

  "Aidha ukiendeleza tabia hiyo, serikali haitasita kuchukua hatua stahiki za kulifungia gazeti lako au kulifutia usajili kwa mujibu wa sheria za nchi.”

  Hata hivyo, barua hiyo ya serikali yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/76 iliyoandikwa kwa mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, haikuweka bayana habari hizo ilizozielezea kuwa ni za mtazamo hasi dhidi ya serikali na ambazo imedai kuwa ni za uchochezi.


  Barua hiyo, ambayo ilibeba kichwa cha habari kisemacho "Karipio kali kwa kuandika habari zenye mwelekeo wa uchochezi wa kudhalilisha", Ilikuwa mwendelezo wa barua nyingine iliyoandikwa na mkurugenzi wa Idara ya Habari, Clement Mshana kwenda kwa mhariri wa gazeti hili Septemba 24, 2010.

  Katika barua hiyo ya Mshana, serikali ilidai kuwa gazeti la Mwananchi limekuwa na mtazamo hasi dhidi ya serikali na ikamtaka mhariri ajieleze.

  Barua hiyo yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/70, bila ya kutoa mifano, ilidai kuwa Mwananchi imekuwa ikiandika habari hasi tu kana kwamba serikali haina zuri linalofanywa kwa wananchi wake na kutaka maelezo.

  “Katika kipindi kirefu sasa, na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Habari hizo zimekuwa zikidhalilisha serikali iliyo madarakani ya awamu nne,” inasema sehemu ya barua hiyo.

  Katika majibu ya barua hiyo ya kwanza, Mwananchi Communications Ltd (MCL), ilieleza kuwa baada ya kutafakari kwa kina ilishindwa kuelewa msingi wa tuhuma hizo ambazo hazina mifano yoyote ya habari inayodaiwa kuwa ni hasi kwa serikali.

  “Baada ya kupitia barua yako na kuitafakari, imetuwia vigumu kuelewa msingi wa tuhuma zako kwa gazeti hili kuhusu mtazamo hasi dhidi ya serikali bila hata kutoa mifano ya habari ambazo zinabeba tuhuma zako kwa gazeti hili hasa unaposema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi,” inasema barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCL/RN/09/VOL.1.27 iliyoandikwa na mhariri mtendaji wa MCL, Theophil Makunga.

  Barua hiyo ya MCL inaeleza kuwa kimsingi habari za kampeni za uchaguzi katika kipindi hiki zinahusu vyama vya siasa na kuhoji sababu za serikali kujiona inaandikwa vibaya na Mwananchi wakati ni vyama ndivyo vinavyoshiriki kwenye kampeni.

  Mhariri wa Mwananchi anaeleza katika barua hiyo kuwa kwa sasa gazeti lake linaandika habari za wagombea uongozi kutoka vyama mbalimbali na sera zao ili wananchi wafanye uamuzi siku ya kupiga kura na hakuna chama kilichoandika barua ya malalamiko.

  “Kwa taarifa yako tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Agosti 21, 2010, gazeti la Mwananchi halijawahi kupata malalamiko kutoka chama chochote cha siasa kinachoshiriki katika kampeni hizo juu ya kuandikwa vibaya. Kimsingi Mwananchi linachofanya ni kuripoti wanachosema wagombea wa vyama mbalimbali au kufanyiwa katika mikutano ya kampeni,” inasema barua hiyo ya MCL kwenda kwa Msajili wa Magazeti.

  Katika barua hiyo, MCL inaiomba serikali kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kuhusika kwa serikali katika kampeni za uchaguzi hadi gazeti hili lionekane lina mtazamo hasi.

  “Kwa msingi huo, tunaomba ufafanuzi zaidi hapa; serikali inahusika vipi katika kampeni mpaka Mwananchi ionekane ina mtazamo hasi kwa serikali wakati vinavyoshiriki katika kampeni ni vyama vya siasa na wagombea wake,” inasema barua hiyo.

  Baada ya barua hiyo, Msajili wa Magazeti alijibu kwamba majibu yaliyotolewa na MCL hayaridhishi na hivyo ofisi yake haikuridhika na utetezi huo.

  “Kama tulivyoeleza kwenye barua yetu kwako kuwa katika kipindi kirefu sasa na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Gazeti lako sasa limeamua kufanya ‘house style’ yake ya kuandika habari zenye uchochezi na kudhalilisha nchi na serikali iliyopo madarakani,” inasema barua hiyo.

  Katika onyo lake, serikali inasema kwamba picha, habari zinazopewa kipaumbele katika ukurasa wa kwanza wa gazeti zinatiwa chumvi kwa lengo la kuchochea wananchi waione serikali yao haijafanya chochote kwa maendeleo yao.

  Akiongelea hatua hiyo ya serikali, Makunga aleleza kushtushwa na karipio hilo ambalo halikuonyesha ni habari ipi ambayo gazeti la Mwananchi limekosea.

  “Msajili hakunukuu hata sheria moja ya vyombo vya habari kuonyesha jinsi gani gazeti limekosea wala habari au kichwa cha habari chenye mtazamo hasi kwa serikali,” alisema Makunga.

  Alisema Mwananchi imechukulia hatua hiyo ya msajili kuwa inatishia uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ambacho kinahitaji uvumulivu baina ya taasisi mbalimbali katika jamii.

  Makunga alisema kwa kuwa Mwananchi na msajili inaonekana kutokubaliana katika suala hilo, wameamua kupeleka taarifa Baraza la Habari Tanzania (MCT) liweze kufanya uchunguzi kwa mujibu wa katiba yao.

  Alisema msimamo wa sera ya uhariri ya MCL inasimamia kwenye ukweli na weledi pasipo kushurutishwa na vikundi vyovyote vya nje na ndani.Makunga alisema Mwananchi itaendelea kuandika habari za ukweli bila ya kumuonea mtu au taasisi yoyote kwa maslahi ya Tanzania.

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Tunachotaka sheria dhalimu dhidi ya vyombo vya habari zifutwe ili tuweze kuendana na karne ya 21..................
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ni report nzuri maana gazeti halikufanya kosa. kuna magazeti kama alhuda yalikuwa yanachochea sana dini hawakuchukua hatua ila mwananchi lililotoa habari za kweli ikawa tatizo
   
 4. A

  Anold JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Wameumbuka!
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Delay Tactics
   
 6. A

  Akiri JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  kuna kagazeti kanaitwa alhuda , sijasikia wakipewa karipio
   
Loading...