MCHUNGAJI William Mwamalanga aishauri CCM

MCHUNGAJI William Mwamalanga aishauri CCM

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
MCHUNGAJI wa Kanisa la Kipentekost la Kiinjili Tanzania, William Mwamalanga amekishauri Chama Cha mapinduzi (CCM) kuacha kuwatumia mawaziri katika ziara zake mikoani, kwani kufanya hivyo ni kukiuka miiko ya taifa.

Alisema kuwaunganisha mawaziri katika ziara za viongozi wa chama hicho, kinawafanya Watanzania wasiokuwa wana CCM kutotilia maanani kile kinachozungumzwa na mawaziri hao katika mikutano ya hadhara.

Mchungaji Mwamalanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuhimiza Amani, Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii Tanzania, aliyasema hayo jana alipotembelea Ofisi za gazeti hili, Sinza Kijiweni mjini Dar es Salaam.

Alisema ziara za viongozi wa CCM katika mikoa mbalimbali, zinapaswa kutenganishwa na zile za mawaziri kwa sababu viapo vyao kwa wananchi vinatofautiana.

“Mawaziri wana viapo vya utii kwa wananchi na Abdurhamani Kinana (Katibu Mkuu wa CCM), ana kiapo chake cha utii, ni tofauti watu hawa kwa kwanini wafanye hivi,” alihoji Mchungaji Mwamalanga.

Alisema mtindo wa sasa wa Sekretarieti mpya ya CCM kuzunguka na mawaziri mikoani na kuwataka wazungumze hadharani utekelezaji wa ilani ya chama, kunaweza kuwafanya wadharaulike kwa wananchi.

“Kwa mfano mambo mengine yapo nje ya uwezo wao, ufinyu wa bajeti ni sehemu ya kikwazo cha utekelezaji wa ilani ya CCM, si makosa ya mawaziri ni Serikali kwa ujumla wake.

“Tumeona maeneo mengine, baadhi ya mawaziri wanazomewa na wananchi, hili si jambo jema, wananchi wengine wasiokuwa wana CCM wanawaweka kapu moja na kauli za viongozi wa CCM ambazo mara nyingi wamezizoea.

“Sisi kama watumishi wa Mungu, hatupendi hali hii itokee, tabia ya kuwazomea mawaziri si nzuri inaweza kuwavunja moyo wa kazi, inashusha heshima yao kwa umma wa Watanzania.

“Kama chama kinaona baadhi ya mawaziri wameshindwa kasi ya uongozi wanayoitaka, basi wapeleke mapendekezo kwa Rais ili ashughulike nao kuliko aibu ya kuzomewa wanayoipata kutoka kwa wananchi.

“Mawaziri wanapaswa kuongozana na Rais au Waziri Mkuu, hata Rais anapotoa ahadi na maagizo, anajua wapi bajeti hiyo ilipo, tofauti na wanasiasa wengine

“CCM wajifunze kwa mataifa mengine, kama Marekani, huwezi kukuta ziara ya Rais inagubikwa na bendera za chama, wanaheshimu miiko ya taifa lao,”alisema Mchungaji Mwamalanga.
 
Waache waende wakazomewe na wananchi wasiojua kesho yao wakati mawaziri wanateremka na ma VX yenye viyoyozi
 
mchungaji yuko sahihi kabisa maana kweli kufanya hivyo si kuijenga ccm bali nikuendelea kuiua
 
Back
Top Bottom