Mchungaji TAG amshauri Rais Samia, amuunga mkono Mbunge Shabiby

Mchungaji TAG amshauri Rais Samia, amuunga mkono Mbunge Shabiby

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
437
Reaction score
735
Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mbagala-Dar, Arist Bukombe amesema endapo serikali chini ya Rais Samia itaruhusu mfanyabiashara yeyote mwenye uwezo wa kuagiza mafuta toka nje, afanye hivyo itapunguza bei ya bidhaa hiyo ambayo kwa sasa imefikia Tsh. 3000 kwa Lita.

Mchungaji Bukombe aliyasema hayo jana akitoa mawazo yake ya nini kifanyike ili kushuka bei ya mafuta nchini ambayo inawaumiza wananchi kwa bidhaa mbalimbali kupanda.

"Tatizo ni kwamba, mafuta ya magari yakipanda bei, basi unga, mchele, sukari, nguo, mbao, nauli, vinywaji, mabati, simenti, vyote hivyo vinapanda bei kwa sababu vinafika kwa watumiaji kwa kusafirishwa na magari yanayotumia mafuta.

"Ipo mifano mingi ya miaka ya nyuma. Mfano leo hii ingekuwa mitumba inaingizwa Tanzania na serikali tu, bei ya mitumba isingeshikika. Bidhaa nyingi katika nchi zinazoingizwa na wafanyabiashara zina nafuu katika bei.

"Naamini hata magari haya yangekuwa yanaingizwa na serikali tu, si ajabu Toyota Vitz moja ingekuwa Tsh. 20,000 Milioni.

"Wafanyabiashara wakipewa uhuru bila idadi kama ilivyo sasa, wataingiza bidhaa kwa kila mmoja kutumia mbinu yake kuipata bidhaa hiyo nchini kwa bei ndogo ili waweze kumaliza na kuagiza tena hata kama faida ni ndogo.

"Kuna wakati Mbunge wa Gairo, Hemed (Ahmed) Shabiby alishauri jambo hili ninalomshauri Rais wangu mama Samia Suluhu Hassan, sijajua nini kinatatiza utekelezaji wake.

"Mbunge yule aliona mbali, ndiyo maana alishauri vile. Kwa hiyo sasa inatakiwa serikali kupanga utaratibu mpya. Wafanyabiashara wajitokeze, wapewe vibali kwa wingi wao, waanze kazi. Ili mradi bidhaa hiyo ipitie mikononi mwa serikali yenyewe, tutaona mabadiliko mara moja," alisema.
 
Issue ya mafuta imekaa kisiasa sana...

Kuiendesha vile ipasavyo inapswa kiongozi uwe mbabe sana maana matajiri wa huko habari zao siyo nzuri...
 
Back
Top Bottom