Euphransia
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 937
- 778
Wadau mpaka Leo nashindwa kupata jibu iwapo Mchungaji Mwasapila a.k.a Babu wa Loliendo" alikuwa Mganga au Tapeli.Maelfu ya watanzania Na majirani kutoka nje ya nchi walimiminika katika kijiji kilichopo Loliondo kwenda kupata matibabu ambayo Babu hakutaka kujua unaumwa nini yeye alitoa kikombe tu.Pamoja Na Dawa hiyo kupelekwa Muhimbili kuchunguzwa lakini bado Serikali haikutuambia inatibu magonjwa gani.Viongozi wa Nchi hii walimiminika Kwa Magari lakini nao hawakujua babu anatibu nini.Wadau naomba tumchambue Babu wa Loliondo je alikuwa mganga au Tapeli?