Mchungaji mbaroni tuhuma kumchoma moto mwanae

Mchungaji mbaroni tuhuma kumchoma moto mwanae

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste lililopo Kongowe Wilaya ya Kibaha, Japhes Manwa (40), kwa tuhuma za kumchoma moto mwanawe.

Mchungaji huyo anadaiwa kumfanyia unyama mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka saba sehemu za mikononi na mgongoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema, tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kibaha juzi majira ya mchana.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo mwenye ulemavu (mtindio wa ubongo) mkazi wa Vikuge Kata ya Soga, ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kalabaka.

Kamanda Wankyo alisema, mtoto huyo, ambaye ni kati ya watoto wanne wa mtuhumiwa alikutwa na mkasa huo kwa madai kuwa baba yake hampendi.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wazazi na walezi wanaotoa adhabu kali kwa watoto kwa lengo la kuwakanya ambazo zinawasababishia majeraha na ulemavu.

Alisema, wazazi na walezi wanatakiwa kutoa adhabu kulingana na makosa na umri wa watoto.
 
Hii haikubaliki . muhusika achukuliwe hatua stahiki

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Harafu siku ya ibada utawakuta wafuasi wako kanisani na ibada inaendelea kama kawaida tu hapo ndio nachoka na wafrika
 
wanakwambia "fuata maneno yangu, usifuate matendo yangu" hakika wachungaji mbinguni mtaisikia tu
 
Ulemavu sio tatizo kwa kiumbe hao ni majaaliwa ya muumba.yeye aumba atakavyo .kuwepo kwa walemavu ni mtihani waja wanapewa ,cha msingi sisi tulio wazima tuwapende walemavu,tuwahurumie pia tuwenao karibu kujua matatizo yao.wewe baba mzazi Wa Mtoto unamfanyia unyama huo wengine watafanyeje ?.ni hukumu letu kuwapenda walemavu Na kuwapa kipaumbele kwani wao hawakupenda kua hivyo.
Kumbuka kabla hujafa hujaumbika .
 
Back
Top Bottom